Huwezi tegemea wawekezaji wa kigeni ndiyo waendeleze nchi

Pana mashirika ya wabongo aliyapa tenda nyingi za ujenzi wa akachemka,akaona Bora awape wachina tu
 
Tatizo ni sisi wenyewe waswahili serikali inatamani sana kuwapa kazi waswahili lakini shida upigaji,ujanja ujanja mwingi,kazi chini ya kiwango,visingizio kibao.
 
Shida ni udhaifu wa wasimamizi wa Sheria zetu wameweka njaa mbele ukiwa na pesa upo juu ya Sheria,human rights sio kwa uvunjifu wa sheria.
 
Huo ndo ukweli
Angalia uwepo wa geita gold mining iliyopo geita hakuna chochote kile walichofanya mji wa hovyo yaan kuna mambo yanatia hasira

Wakiulizwa wanasema wanapata hasara mwaka wa ishirini huu
Shida sio mgodi ni halmashauri kula pesa zitolewazo na mgodi
 
Kwani kinachosababisha kutafuta muwekezaji si baada ya watumishi wameshindwa kuendesha mradi kwa sababu ya rushwa mkuu.

Hivi wangekuwa wangekuwa wanafanya kazi kwa uadilifu wanatoa huduma vizuri unafikiri kungekuwa na haja ya kuleta wawekezaji?
Maslai duni,mishahara mbuzi Tena ya ubuguzi wanaovaa suti hawawanyi kazi sana wanavuta nyingi,uadilifu na tija vitoke wapi
 
 

Attachments

  • 0B54B1AA-1561-4237-ACB5-8A4D39156675.png
    4.7 MB · Views: 1
Akina Pengo wengi.
 
Naunga mkono hoja. Ni kweli ukiona umeshaingiza mambo ya siasa kwenye shughuli za kiuchumi ambazo huwa zina Formula zake ujue kwa uhakika ww kwisha habari yako.
Mnaletewa dawa ya Chanjo ya Malaria, sijui ni mpaka tugundue wenyewe. Yaani Afrika nzima imeshindwa Kutafuta suluhisho la malaria, licha ya kujua kuwa ni ugonjwa hatari ktk bara la Afrika. Subiri miaka 60 mingine upate akili.
 
Mnaletewa dawa ya Chanjo ya Malaria, sijui ni mpaka tugundue wenyewe. Yaani Afrika nzima imeshindwa Kutafuta suluhisho la malaria, licha ya kujua kuwa ni ugonjwa hatari ktk bara la Afrika. Subiri miaka 60 mingine upate akili.
Ni humuhumu kwenye vya kupewa/misaada tunapigiwamo. Kwani Malaria haitibiki kwa dawa za kawaida?? Ni mpaka chanjo? Yan vitu vingi tunajitakia tuu kwa matamanio yetu ya kuishi peponi (kwa raha bila mahangaiko) tukiwa bado hapa duniani. Tutachezewa sana aisee.
 
Hakuna Mzungu anakuja Afrika kuwekeza ili awasaidie Waafrika.

Tunaibiwa tu. Fukuza hawa wazungu tuchimbe madini yetu wenyewe. Tukishindwa bora yabaki ardhini vizazi vijavyo vitajua chakufanya
Uwekezaji sio msaada, ni biashara. Mwekezaji yeyote, awe mzungu au mweusi mwenzetu anawekeza ili apate faida, sio asaidie watu.
 
Uwekezaji unaleta Maendeleo sema sisi ndio tunajiibia wenyewe ninakumbukuka Barrick walipoingia walikuwa wakitoa Mishahara minono sana Serikali ikawaambia wapunguze kwasababu Watumishi wa Umma wataacha kazi na kuhamia Migodini.
Sahihi
 
Huu wizi una mahusiano na uongozi. Kama viongozi wapatikana kwa wizi wa kura, unategemea watapata wapi nguvu ya kuzuia wizi? Kama viongozi wangekuwa wapatikana kwa njia halali, wangekuwa na moral authority ya kushughulikia wezi.
Umeongea point ya muhimu sana mfumo wa kupata viongozi ni mbovu sana
 
Uwekezaji sio msaada, ni biashara. Mwekezaji yeyote, awe mzungu au mweusi mwenzetu anawekeza ili apate faida, sio asaidie watu.
Hiko ndo kitu ambacho watu wwngi hawakijiu
Nchi za gulf rasilimali zao zote hawakumpa mwekezaji walisimamia wao wenyewe
 
Kipi cha mswahili kilichofanyika kwa ufasaha.
Mswahili huyu huyu anaeamini ndumba kwenye business ndio aweze endesha uchumi wa nchi.
Africa nzima uchumi unaendeshwa na wahindi au waarabu.
Labda useme wapewe wazawa ambao ni wahindi au waarabu.
Basi umaskin utaendelea afrika mpaka watakapo jitambua
Muhindi mwenye fikra za dewji ndo utegemee aendeleze nchi
 
Hakuna Mzungu anakuja Afrika kuwekeza ili awasaidie Waafrika.

Tunaibiwa tu. Fukuza hawa wazungu tuchimbe madini yetu wenyewe. Tukishindwa bora yabaki ardhini vizazi vijavyo vitajua chakufanya
Mna uwezo huo wa kuchimba wenyewe? Siwa support wazungu natamani waondoke lakini alternatives ikoje? Angalia track record ya watanzania ku run tu mashirika makubwa machache yote yameishia kufanya vibaya na kuletahasara, kama kujisimamia ni shida unadhani kuchimba mtaweza? Na mkiweza mtafaidika nyie au wanasiasa?

Dunia inaenda mbele haisimami, masuala ya kuacha rasilimali chini eti kisa wazawa hawajaweza ku extract ni ushamba. Maendele ni sasa
 
Hiko ndo kitu ambacho watu wwngi hawakijiu
Nchi za gulf rasilimali zao zote hawakumpa mwekezaji walisimamia wao wenyewe
Sawa kabisa. Sasa tujiulize , Je, sisi wabongo tunazo rasilmali kibao Tunakwama wapi lakini??
 
Miaka 20 tokea hao wazungu warusiwe kuchimba madini kila siku wanasema wanapata hasara In short hiyo migodi hawana msaada wowote kwa nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…