Huwezi tegemea wawekezaji wa kigeni ndiyo waendeleze nchi

serikali ingejitahidi kufanya mabadiliko ya sheria kwanza alafu hayo mashirika wangeyaongoza wenyewe sisi hapa wananchi,ila kwa wanavofanya ni serikali na viongozi wanafaidika kwa kupewa chajuu ila wananyima sisi fursa imagine serikali ingekuwa inaoperate yenyewe je wangeajiri watu wangap?ila inapoajiri sekta binafsi wao wapo kwenye maximizition of profit watajitahidi sana kutumia watu wachache kwenye kazi kubwa .
 
Sawa kabisa. Sasa tujiulize , Je, sisi wabongo tunazo rasilmali kibao Tunakwama wapi lakini??
Serekali ya ccm mtu akiiba anahamisiwa sehemu nyingine hapo unategemea kutakua na ufanisi

Report ya CAG inataja watu ni waizi lakin wanaendelea kufanya kazi na wengine wanahamishwa
 
Hivi watu wanashindwa kutofautisha mwekezaji na watoa misaada? mwekezaji anakuja kufanya biashara kupata faida, kazi yake kuhakikisha faida inapatikana na kazi ya serikali kukusanya kodi zake kwa mujibu wa sheria sasa shida iko wapi. Uwekezaji unaleta ufanisi sababu mashirika yanakuwa private yanakuwa na nidhamu ya kazi huku serikalini tume fail sana, hakuna shirika la serikali tunaweza kujivunia leo. Chukua mfano TTCL walivyo oza sasa TTCL mpe mwekezaji utaona kitakachotokea, shirika la Railway ona madudu. Mimi nilishawahi kuandika humu ukitaka SGR ifanikiwe usiruhusu shirika likaendeshwa kama shirika la uma weka private operator utaona ufanisi na ushindani. Hiyo mifano yako ya KSA na UAE lazima uje mfano UAE mashirka ya kutoa huduma za simu ni mali ya serikali Du la Dubai na Etisat ni Abudhabi hawaruhusu ushindani lakini kizuri wanaendesha kama private lakini ni la serikali hata Emirates airline own na Dubai lakini linaendeshwa kiprivate. Sisi tume fail tumeuwa mashirika yote.
 
Wazungu, Wachina na Waarabu hawatuibii kwa nguvu au kutulazimisha. Dili zote za upigaji katika mikataba zinatengenezwa na kulazimishwa kwa hao wawekezaji wa nje na watawala/watumishi wa Africa. Watoa tenda, mikataba na vibali wakinyooka hata hao wawekezaji lazima watanyooka tu.
 
Serekali ya ccm mtu akiiba anahamisiwa sehemu nyingine hapo unategemea kutakua na ufanisi

Report ya CAG inataja watu ni waizi lakin wanaendelea kufanya kazi na wengine wanahamishwa
Ndo hapo sasa.
 
Rasilimali ziwe chini ya serekali maboss waajiriwe wazungu au mtu yeyote ambaye ni competent sio lazima awe chawa anasifia sifia
Yeah! Vigezo na masharti kuzingatia. Kigezo cha Uchawa marufuku kisiwepo kabisa.
 
Serikali ya mama ina affinity kubwa sana na UAE hasa Dubai. Hivi kwanini tunaamini hatuwezi? JPM alikuwa akiamini tunaweza.
 
Hatukatai wawekezaji lkn waje na vitu vikubwa. Sio kuendesha mradi wa dala dala.
 
Serikali ya mama ina affinity kubwa sana na UAE hasa Dubai. Hivi kwanini tunaamini hatuwezi? JPM alikuwa akiamini tunaweza.
Hivi kuna Serikali ya mama au kuna Serikali yetu? Kuwa na ukaribu au affinity na nchi fulani sioni kama ni kosa au kasoro kwani Juliasi alikuwa na ukaribu na China na Cuba na walipanza kumlalamikia eti hana msimamo aliwaambia (Black n White) kwamba sio sahihi kutuchagulia marafiki.
 
Kuna wakati unakuwaga huna akili? Nenda marekani almost 70% ya wawekezaji ni wachina
 
Kuna wakati unakuwaga huna akili? Nenda marekani almost 70% ya wawekezaji ni wachina
Unafananisha marekani nchi ambayo rais anastakiwa na nchi ya Tanzania mbayo hadi speaker wa bunge ana kinga hivi una akili kweli

Unawezaje kuiweka marekani na Tanzania kwenye sentensi moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…