Huwezi ukawa mzinzi halafu ukawa mwanaharakati kuponda ushoga. Ushoga ipo ndani ya uzinzi!

Huwezi ukawa mzinzi halafu ukawa mwanaharakati kuponda ushoga. Ushoga ipo ndani ya uzinzi!

HUWEZI UKAWA MZINZI ALAFU UKAWA MWANAHARAKATI KUPONDA USHOGA. USHOGA IPO NDANI YA UZINZI YAANI NI SUB SECTION.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Angalizo: andiko hili limeandikwa kwa lugha na maneno magumu kidogo. Hivyo kama wewe sio mvumilivu na haupendelei maneno magumu Mtibeli anakushauri uishia hapahapa.

Kuna watu hufikiri kuna dhambi zenye afadhali. Ndicho wanachokifikiri.

Kwamba bora mimi mzinzi kuliko wewe shoga.
Bora mimi mshirikina kuliko wewe mchawi.
Kwamba bora mimi kibaka kuliko wewe jambazi.

Nimeona watu wengi wakiwaponda mashoga. Wakiwafanyia harassment ya kutosha.
Sio jambo baya kuwafanyua harassment na kuw bullying waovu na wahalifu. Lakini unapofanya hivyo hakikisha usiwe na double standard.
Pia hakikisha nawe huna maovu ya aina hiyo.

Mchawi na mshirikina hawa ni Timu moja lakini idara tofauti. Unapomwona mtu anayeenda kwa waganga wa kienyeji kufuata ulozi na mambo ya kijadi na kisha ukasikia mtu fulani ni mchawi basi jua hao wote ni kundi moja. Wote ni walewale.

Sisi Watibeli tunajuamchawi na mshirikina tunaona ni watu walewale.

Uzinzi ni neno pana lenye idara na vipera mbalimbali.
Kwenye uzinzi kuna uasherati, ulawiti, kufirana, kufira, kusagana, kupiga punyeto, kulala na midoli, kufanya ngono na wanyama , na matendo yote ya ushoga. Hao wote wapo kundi moja ni wazinzi.

Amri inayosema usizini. Kwenye ufafanuzi imeeleza hayo yote niliyoyataja hapo.

Kwamba mtu anayefanya ushoga na anayelawiti, au kufanya ngono kinyume na maadili wote ni kundi moja.

Ushoga upigwe vita hilo ni sawa. Hata sisi Watibeli tunaupiga vita.

Lakini huwezi kupiga vita ushoga wakati huohuo wewe unafanya zinaa zingine.
Unafira wanawake.
Unalawiti watoto.
Unazalisha wanawake hovyohovyo ambao hukuwaoa.
Umesababisha watoto haramu kibao. Alafu leo unanyanyua mdomo kama filimbi kupiga kelele. Hatutaki ushoga.

Ushoga ni mtoto wa Uzinzi. Kwamba wewe mzinzi ni Baba wa mashoga, wafiraji, walawiti, watoto haramu.

Alafu zaidi lazima tuyaweka haya mambo sawa kabisa.

Ili ushoga utokee lazima uzinzi uwe umekomaa.
Kwamba watoto wamezaliwa hovyohovyo, watoto haramu, watoto wa zinaa.

Sasa hawa watoto wa zinaa hawa wanaishi bila misingi ya maadili. Hawana malezi bora ya baba na Mama.

Ukifuatilia mashoga wengi, au waliobakwa, au waliolawiti wengi wao msingi wao mkuu ni kutokea familia zenye wazazi wafanya zinaa.

Uzinzi unasababisha broken families. Na familia zikishakuwa broken ndio haya unayoyaona sasa.

Wewe unapinga ushoga. Upo sahihi.
Lakini umefanya uzinzi, umezalisha wanawake huko. Watoto huwalei wewe. Watoto wa zinaa. Hujui mtoto wako huko anaishije. Mtoto anaanza kufirwa na kujifunza tabia za hovyo kama za wazazi wake(wewe) unakuja kumlaumu baadaye.

Unaposema hutaki ushoga, ni vizuri zaidi kuzuia mzizi wa ushoga ambao ni zinaa.

Dudu baya anaweza kuchukizwa na ushoga lakini asichukizwe na zinaa. Ndio maana ni nadra sana kumkuta akiongea na kupiga kelele kuhusu ushoga.
Mtu kama Dudu Baya sio ajabu anawatoto aliowazaa kiharamu, kwa zinaa, hajui wanaishije huko, Hanalei yeye. Na kutoa hela sio kulea.
Huyo mtoto akijifunza ushoga, au akifanyiwa matendo ya kishoga kwa sababu hana ulinzi wowote. Baba hayupo. Alifanya zinaa akiwa amelewa ndio wakampata mtoto huyo. Huo ujasiri wa kumwambia mtoto aache ushoga utatoka wapi?

Mtibeli sio kwamba naunga mkono ushoga. Hapana. Sisi kama Watibeli tunapinga uhalifu na uovu wa aina yoyote ule. Kwa lugha ileile na kwa nguvu hiyohiyo.

Tatizo la ushoga ni tatizo ambalo mzizi wake umeanzia ngazi ya mtu binafsi na familia.
Kijana yupo kwenye foolish age, anajinywea Mapombe, anakutana na wanawake wahuni kama yeye. Wanafanya umalaya na uasherati. Anazaliwa mtoto ambaye ni zao la uasherati.

Baba na Mama wanalaumiana. Hatukupanga tuzae. Tulikuwa kwenye starehe. Mimi siwezi kukuoa. Binti naye anasema sitting mimba. Tayari nishafanya umalaya siwezi kufanya dhambi nyingine ya kuua kitoto cha zinaa kisicho na hatia.

Baba anasusa hataki kulea mtoto. Anaondoka. Mtoto anakua bila malezi ya baba. Bila ulinzi. Mbaya zaidi ukute mama ni maskini kabisa na hana elimu. Hali inakuwa mbaya zaidi.

Serikali inataka kuokoa jahazi. Inamshinikiza Mwanaume atunze mtoto. Lakini kutunza mtoto sio kulea. Kumpa malezi bora yenye maadili na kumuandaa kuw mtu bora.
So mtoto anatunzwa na kuhudumiwa kama mfugo vile. Lakini Anakosa upendo na malezi ya wazazi wawili.
Madhara yake ndio hayo. Wengine wanageuka machoko, wengine, vibaka, wengine hivyohivyo ilimradi wanajiendea.

Kinachosikitisha, yule mtoto wa zinaa ambaye ni mhanga, asiye na kosa lolote. Amejikuta na status ya uharamu au mtoto wa zinaa. Anabeba tena lawama na athari za matendo ya wazazi wake waovu.

Ndio ule msemo unasema, nawapatiliza maelfu maelfu ya wanichukiao hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao.

Unakuta mwanaume kulea mtoto hajalea. Alafu anakuwa wakwanza kutoa lawama kama chizi.
Oooh! Mtoto hujafundishwa adabu sio. Nani afundishe toto lako adabu kama sio wewe Baba?
Wakati anatakiwa kufundishwa adabu wewe mwenye huo wajibu ulikuwa wapi? Hiyo inakuwa sio haki.

Oooh! Umelishwa sumu na Mamaako. Mara wanawake wanalisha sumu watoto.
Hivi Kuna sumu kali zaidi ya kuzaa watoto kwa njia ya zinaa?
Kitendo cha mwanaume na mwanamke kufanya zinaa na kuleta viumbe waliokuja kimagendo. Ndio sumu kubwa kuliko jambo lolote.
Kuzaa mtoto kwa matamaa badala ya upendo.

Alafu majitu yalivyo manafiki, wabaya, wabinafsi, wanakuambia mtoto ni mtoto. Napenda mtoto wangu. Ungekuwa unapenda mtoto ungemzaa kiharamu haramu?
Ukamtelekeza au huyo mwanamke mliyezaa naye mkaendeleza jambo lenu mlilolianzisha kufanya mambo kiharamu, kibinafsi, kitamaa mkashindwa kumlea mtoto wenu kwa pamoja mwa upendo.
Leo unajifanya Baba mtakatifu. Wakati ni mpuuzi tuu.

Haya wanawake nao. Oooh! Hakuna mapenzi sijui upendo kama upendo wa mama kwa mtoto.
Ungekuwa unaupendo kweli. Ungempata huyo mtoto kimagendo? Kitamaa? Kinyege nyege?
Nyege zilikuendesha, tamaa zilikuzidia ukakikuta umebeba mimba usiyoipanga. Mtoto akazaliwa katika hali mbaya ya kusikitisha. Na sio kwamba ulikuwa hujui. Ulijua na ulifanya kwa ubinafsi wako.
Leo unasema unampenda mwanao?

Unampenda mwanao ungekubali umlete duniani bila makubaliano ya upendo na Baba yake?
Sasa huo upendo ndio unamlea bila Baba. Mtoto anaita kila mtu Baba kama mtoto wa mbwa? Kweli! Hapana!

Sisi Watibeli tunajua nini maana ya upendo. Wengi wanausema upendo kwa mihemko bila Akili. Wakiongozwa na tamaa na ubinafsi wao. Wakiongozwa na chuki.
Unasema unampenda mtoto wako alafu muda huohuo ulimzaa kimazabe, kwa nyege?
Haya sikulaumu. Kuna kukosea kama binadamu.
Haya umekosea umetubu. Haya unasema unampenda mtoto uliyemzaa kimazabe na sasa umeomba toba lakini muda huohuo unamzuia Baba au Mama yake asiwasiliane na Mtoto. Unafanya tukio lilelile la kinyege nyege, tamaa na ubinafsi. Unajiangalia wewe tuu.
Mtoto anakuwa Kilema wa malezi.

Alafu unakuja kuimba hapa, oooh! Watu hawana upendo. Upendo upi huo unaoutaka?

Unakuja kupiga kelele kuhusu mashoga. Mimi mashoga niliowahi kuwaona asilimia 90% wamezaliwa kwenye zinaa. Asilimia kubwa wanatokea kwenye broken Family. Familia zisizo na Baba na Mama.
Na kama Baba na Mama wapo. Basi hakuna Upendo na Haki.

Nataka kumaliza kwa kusema, unapotaka kutoa kibanzi cha jirani angalia boriti kwenye jicho lako.

Wewe ni mzinzi, huna mamlaka yoyote ya kumponda na kumnyoshea kidole Shoga. Kwa sababu ushoga ni moja ya matokeo ya uzinzi uliokomaa. Ni sub section za zinaa.

Chakufanya,
Watu waache uzinzi.
Wanawake waolewe bikira.
Wanaume wasioe mwanamke asiye bikira. Hiyo kanuni watu wenye upeo mdogo hawawezi kuijua na kutafakari.

Mimi nimemaliza.

TaikonMaster
Kwa sasa Kahama, Shinyanga.
Nilichogundua ni kuwa Kuna wazinzi wengi sana humu jf maana wanavyo utetea huo uzinzi duuh.
Anyway Mimi binafsi ni heri nikawa mzinzi kuliko kuwa shoga
 
Lengo kuu la huu uzi ni kutaka Ushoga uonekane kua ni jambo la kawaida tu kama yalivyo mambo mengine tu,

Dudubaya shikilia hapo hapo tupo pamoja

Y B W Y B
 
Kwa nini uzinzi sio jinai kwenye sheria za Tanzania kama ilivyo ushoga??
Hajaandika kwa refer ya sheria za Tanzania, ameandika kwa uhalisia wake. Sheria inaweza kusema kuwa na bangi ni kosa, kesho yake ikawa sio kosa. Lakini ukweli wa uhalisia huendelea kuishi
 
Uzinzi na uasherati(kwa Wagalatia) na Zinaa(kwa Kobaz) ni mambo yaliyokatazwa na mungu wa Wakristo na Waislamu. Kama uko kwenye dini hizi lazima upige vita uzinzi na uasherati, kwenye dini hizi mbili hizo sio dhana tu bali maagizo ya mnyazi mungu.

Kwa Wagalatia Uzinzi ni mke au mume kuchepuka, uasherati ni kufanya ngono kwa mtu asiye na ndoa.

Kwa Kobaz zinaa ni matendo yote ya ngono nje ya ndoa.

Ni sawa; mimi sio mwamini wa dini na ugalatia. Naamini katika nature na bailojia. Hizo ni dhana tuu wamaejijengea hao. Dhana hizo hazina uhalisia. Uhalali au uharamu wa kitu kwa imani yangu ni pale kotu hicho kinapokwenda kinyume na nature na bailojia. Hakuna mtu haramu, hakuna mtu halali ni dhana tuu za kupandikizwa.
 
Umenena ukweli mkuu hakuna dhambi ndogo wala kubwa huwezi kuonja sumu kwa kidole ukadhan haita kuua
 
maelzo yako nilitaka nisome yote ila uliposema kwamba sio jambo Baya Kuwafanyia Bullying Waovu nikaona tu niache kusome Nicoment niendelee na mambo zingine.Kichaa anachekesha akiwa sio ndugu yako.Shoga anaudhi usipokuwa ni wewe,ni mtoto wako au ni ndugu yako.Maovu ni mabaya ila waovu ni watu.Ukishaelewa hili utajifunza kutokuhuku ili usihukumiwe.
Aisee
 
Nijuavyo uzinzi ni kushiriki tendo kabla hujaoa au kuolewa,

Ni sehemu ya ukweli kwa kiasi.

Kufanya tendo la ndoa mnyama n uzinzi. Jina lake ni ufuska
Kufanya tendo la ndoa na jinsia moja ni uzinzi. Jina lake ni ushoga
Kufanya tendo la ndoa na Mzazi, mtoto, na ndugu wote walioharamishwa ni uzinzi. Jina lake ni uasherari

Kufanya tendo la ndoa bila ridhaa ya mtu ni uzinzi. Jina lake ni ubakaji.

Kufanya tendo la ndoa kinyume na maumbile. Ni uzinzi. Inaitwa ufiraji na ulawiti.

Kufanya tendo la ndoa na kiungo kisicho cha uzazi, kama mkono, vifaa vya teknolojia kama foldout, n.k. huitwa Punyeto. Ni uzinzi pia.
 
Shoga anaudhi usipokuwa ni wewe,ni mtoto wako au ni ndugu yako.Maovu ni mabaya ila waovu ni watu
Maana yako ni shoga haudhi ikiwa ni wewe,ni mtoto wako au ni ndugu yako.(UKAMALIZIA KUSEMA)Maovu ni mabaya ila waovu ni watu.
BILA SHAKA WEWE NI SHOGA.
 
Maana yako ni shoga haudhi ikiwa ni wewe,ni mtoto wako au ni ndugu yako.(UKAMALIZIA KUSEMA)Maovu ni mabaya ila waovu ni watu.
BILA SHAKA WEWE NI SHOGA.
Hutaelewa.Ila fahamu tu kwamba kuna mengi nimeyaona.Wapo mashoga wengi sana ambao wanajificha kwa mtindo wako wa kuwaona wengine mashoga ila wakiwekwa kati ni wale wale.Sisi tunaofahamu hili tunawaambia tu kwamba Usifikiri ushoga ni ubunifu,ni janga ambalo linaakisi malezi na maadili katika namna ambayo huwezi kuielewa kama utafikiri unavyofikiri
 
Hutaelewa.Ila fahamu tu kwamba kuna mengi nimeyaona.Wapo mashoga wengi sana ambao wanajificha kwa mtindo wako wa kuwaona wengine mashoga ila wakiwekwa kati ni wale wale.Sisi tunaofahamu hili tunawaambia tu kwamba Usifikiri ushoga ni ubunifu,ni janga ambalo linaakisi malezi na maadili katika namna ambayo huwezi kuielewa kama utafikiri unavyofikiri
Asante kwa kunichulia mimi kuwa ni shoga,(Ila MIMI na MUNGU TUNAJUA)
Ubarikiwe,


Usifikiri ushoga ni ubunifu,ni janga ambalo linaakisi malezi na maadili katika namna ambayo huwezi kuielewa kama utafikiri unavyofikiri
Kwani mbona unaongea kama mtu aliyekata tamaa mkuu?

Copied:”Shoga anaudhi usipokuwa ni wewe,ni mtoto wako au ni ndugu yako.Maovu ni mabaya ila waovu ni watu” Masokotz

Ulikuwa na maana gani mkuu?
 
Back
Top Bottom