Superbug
JF-Expert Member
- Jan 31, 2018
- 13,864
- 35,079
Msitufanye watoto wadogo eti kakaa tumboni miaka mitatu na anatibu kwa kutumia Sala na maji.
====
‘Mrithi’ Babu wa Loliondo aibukia Rorya
Rorya. Wiki chache baada ya kifo cha Mchungaji Ambilikile Mwasapile maarufu kama Babu wa Loliondo, mtoto wa miaka miwili na miezi tisa, Yunis Ogot ameibuka katika Kijiji cha Bukama wilayani hapa akidaiwa kuwa na uwezo wa kutibu na kuponya maradhi.
Pamoja na kutibu, mtoto huyo pia anadaiwa kuwa na uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali kwa sala na maji ya baraka. Kadri muda unavyozidi kwenda, mtoto huyo anazidi kuwa kivutio kwa watu kutoka ndani na nje ya nchi na inaelezwa wastani wa watu 100 huenda nyumbani kwao kila siku kupata huduma ya maombi na maji ya baraka.
Inaelezwa kuwa alianza kutibu kwa maji na sala akiwa na umri wa miaka miwili na kadri muda unavyozidi kwenda watu wanaohudumiwa wanaongezeka. Alianza na waumini wachache wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Karoli Rwanga Parokia ya Bukama waliofika wastani wa watu 100 kwa siku.
Mbali na kutibu, mtoto huyo ni wa aina yake kwa sababu mama yake mzazi, Agnes Ogot anasema alibeba mimba yake kwa muda wa miaka mitatu tofauti na ilivyo kawada kya miezi tisa. Maajabu mengine ya mtoto huyo Mluo ambaye hajui kusoma wala kuandika, anaweza kusali sala zote za Kikatoliki kwa lugha ya Kiswahili.
Yunis pia amekuwa na kawaida ya kufunga kila Ijumaa na ikitokea mtu akampa chakula siku hiyo hawezi kula jambo ambalo limekuwa likiwaacha wazazi wake mdomo wazi kwa namna anavyotambua siku za wiki nzima na kuitofautisha Ijumaa katika umri huo mdogo.
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, baba wa mtoto huyo, Julius Ogot anasema Novemba 16 mwaka jana akiwa amelala usiku na mkewe pamoja na mtoto huyo, ghafla majira ya saa 9 usiku alisikia kishindo kikubwa kilichomfanya adhani kuna wezi hivyo akaamka na kutafuta panga ili akabiliane nao.
“Siku hiyo mchana, nikiwa kwenye mihangaiko yangu, mwizi aliiba sola kwa hiyo tuliporudi nyumbani jioni hatukuwa na namna ikabidi tulale gizani kwa hiyo niliposikia kishindo nikajua yule mwizi amerudi tena kuiba ikabidi nichukue panga langu tayari kwa kupambana,” anasema.
Akiwa bado hajajua afanye nini, anasema ghafla alisikia sauti ya mtoto wake ikimuita na kuwataka wapige magoti wasali jambo lililomshangaza kwani sauti hiyo ilikuwa ikitokea nyuma ya pazia iliyotenganisha sehemu ya kulala na sebule katika nyumba yao.
“Nyumba yangu imetenganishwa na pazia tu na kitanda chetu ni kirefu sana kiasi kwamba mtoto mdogo kama huyu hawezi kushuka peke yake ikabidi nikunje pazia kwa kutumia panga nililokuwa nimelishika niweze kuona ilipokuwa inatoka sauti ya mtoto,” anasimulia.
Anasema alishikwa na mshangao uliochanganyikana na woga alipomshuhudia mtoto wake akiwa amelala kifudifudi huku mwili wote ukiwa unawaka moto na akiwasisitiza wazazi wake kupiga magoti wasali kwa pamoja.
Ogot anasema baada ya kuona hali hiyo haraka yeye na mke wake waliungana na mtoto wao. Yeye alinyoosha mkono wake kumshika mtoto wakati mke wake akipiga magoti kufuata maelekezo waliyokuwa wanapewa na mtoto wakati huo.
Anasema baada ya kumshika mtoto huku moto ukiwa unaendelea kuwaka kwenye mwili hakusikia joto wala dalili za kuungua na kwamba moto huo pia haukuwa na moshi hali iliyomlazimu apige magoti kwani muda wote mtoto alikuwa akimsisitiza apige magoti.
Anasema baada ya wote kupiga magoti moto ule ulianza kupungua na mtoto huyo akaanza kusali sala ya Baba Yetu, Salam Maria, na Atukuzwe Mungu Baba kwa lugha ya Kiswahili huku akirudia kila sala mara tatu.
Anasema walipigwa butwaa kusikia mtoto huyo akisali sala hizo ilhali hakuwa anajua Kiswahili kwani muda wote wamekuwa wakiongea Kiluo na mtoto huyo hakuwa anazijua sala hizo hapo awali ingawa wamekuwa na utaratibu wa kwenda kanisani kila Jumapili kama kawaida ya waumini wengi.
“Baada ya sala, mtoto alianza kuimba lugha ambayo sikuitambua hadi sasa na baada ya muda akatulia kimya kabisa tukadhani amefariki nikambeba kumtoa nje apate upepo lakini akaniambia turudi ndani tulale tukajaribu kumhoji ambapo alituambia kuwa mama yake mzuri alikuwa amemfuata akawa anaongea naye,” anaeleza.
Anasema mtoto huyo aliwaambia kuwa mama yake huyo mzuri alikuja kumchukua akiwa amevaa mavazi meupe kisha kwenda naye kwa wamama wengine wazuri wanaofanana naye na kuambiwa aweke mikono yake kwenye maji yaliyokuwapo na kuitoa ikiwa ni ishara ya kuyabariki maji hayo.
Anasema baada ya mahojiano mtoto huyo alirudi kitandani kulala lakini wazazi wake walikosa usingizi kutokana na hofu waliyoipata hivyo kulazimika kukesha hadi asubuhi.
Baada ya mtoto kuamka, anasema aliwataka wazazi wake kuandaa maji mengi na kuyapeleka kwenye uwanja wa Sekondari ya Bukama jirani na nyumbani kwao ili ayabariki na watu wayatumie kutibu magonjwa.
Chanzo: Mwananchi