Huyu abiria wa Mwendokasi kanikera sana, Wabongo tutaacha lini hizi tabia za kueleza mambo binafsi kwenye "public"?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Leo asubuhi wakati nimepanda mwendokasi kuna mwamba mmoja nimekutana naye siyo mara ya kwanza mimi kumkuta kwenye gari, nadhani kama sijakosa itakuwa mara ya pili au tatu.

Sasa huyu mwamba alikuwa akipiga stori na mtu aliyekuwa amesimama naye karibu, nadhani wanafahamiana, sasa huyo jamaa ninayemzungumzia hapa akawa ndio msemaji mkuu, yule mshkaji mwingine akawa anaitikia tu au kuchombeza kidogo kidogo.

Kwa kuwa asubuhi kulikuwa na utulivu na asilimia kubwa ya abiria tukawa tunawaza mishe zetu tunazoenda kuzifanya kwenye purukusani zetu, jamaa akawa anazungumza kwa sauti kubwa, siyo kubwa kiasi cha kukera, Hapana ila ilikuwa kubwa kiasi ambacho wote waliomzunguka ni kama wanamsikiliza yeye.

Jamaa akaanza kuwa anazungumza kuhusu maisha yake binafsi, mara yeye na mkewe mara majirani zake, mara fulani kafanya hivi na ningekuwa mimi ningefanya hivi.

Yaani kwa ufupi ni kama alikuwa anawasimulia watu ambao hata hawamjui kuhusu mambo yake binafsi, kibaya zaidi stori nyingine zikawa unaona kabisa hii ni uwongo ila anaongeza chumvi ili aonekane mwamba, ni ushamba tu.

Hii michongo ya kuzungumza mambo yetu binafsi Watanzania sijui tumeitoa wapi, yaani likitokea tukio kidogo tu mtu anadakia na kuanza kuelezea “Mimi ni hivi…” mara utasikia “Achana na hiyo, mimi yalinikuta…”

Wabongo tuache ushamba, kwani mtu hauwezi kuzungumza kwa sauti ya chini tu na ukasikika na huyo uliyenaye karibu yako, unaongeza sauti ili watu wakusikilize wewe ili iweje, tena wengine wanaenda mbali na kuzungumza kuhusu maisha yao binafsi kabisa na kuhisi ni sifa.
 
Siku nyingine weka headphones 🎧 na maisha yako yatakuwa rahisi.

Usafiri wa umma wanapanda watu wa kila aina wengine wanapenda kuongea sana,wengine wanapenda kutongoza sana wengine wanapenda kusali/kuswali sana wengine wanapenda kujamba sana nakadhalika tuvumiliane tu ndio hali zetu na nchi yetu.
 
Mkuu, jamaa hana kosa sema ww unakisirani. Nunua airpods mzee unakua unasikiliza habari za magazeti ile asubuhi. Au kuna Earpods zina ANC ukiweka masikioni ata hauplay kitu hausikii makelele ya pembeni.
Umemshauri vizuri azikilize magazeti siyo kuja kutaka kusikiliza watu

Kama hujui 89:3 Ni rfa au radio asikilize nipashe 12:30 am au saa 1:3am asikilize wasafi fm na siyo kuja kuwasikiliza wafu wanaongeaa mambo yao
 
Hapo kwenye kujamba ungemshauri avae bakora....

Umesahau na uvaaji wa baadhi ya abiria ....hapo ungemshauri anunue mawani ya mbao kabisa
 
Mkuu, jamaa hana kosa sema ww unakisirani. Nunua airpods mzee unakua unasikiliza habari za magazeti ile asubuhi. Au kuna Earpods zina ANC ukiweka masikioni ata hauplay kitu hausikii makelele ya pembeni.
Jamaa hakupenda story za watu tena waliooa kuzipeleka mwendo kasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…