Huyu aliyeelekeza magari ya serikali kupaki saa kumi na mbili ana maana gani?

Sasa kama muda wa kazi umekwisha na huna dharula yoyote ya kikazi kwanini usipaki gari la serikali.......kuna ugumu gani kulielewa hili......??

Hebu jenga kama ni gari lako....baadae ya muda wa kazi kuisha utamuachia tu dereva azurure nalo tu bila kuwa na sababu za msingi.......mimi sioni haja ya malalamiko ukizingatia hayo magari ndio yanayokamatwa kwenye mambo haramu
 
Yupo sahihi ingawa madereva wamecharuka, muda wa ofisi za serikali ukiondoa baadhi ya taasisi Kama Tra ni saa 9.30 na ulienda baada ya muda huo hawakupi huduma.
Kama gari linakuwa nje ya saa kumi na mbili linapaswa liwe na kibali maalumu.
Nafikiri angeoogezea hata kutumia siku za mapumziko kuwe.na kibali maalumu kudhibiti matumizi mabaya ikiwemo matumizi mabaya ya mafuta.
 
Nyie watoto mliomaliza kunywa maziwa ya mama majuzi tu, hamjui kuwa kupaki magari saa 12, ni kanuni ya matumizi wa hayo magari toka enzi ya mkoloni.
Isipokuwa kwa kazi maalum au kwa sababu maalum inayofahamika !
Wahenga tunaifahamu hiyo Amri !
 
Serikali ina masaa ya kazi Acha hizo .Muda wa kazi ukiisha nenda kwenu au kalale na gari kapaki
 
Tuambie nani huyo na kasema hayo wapi
 
Kwahyo wakuache utumie hadi usiku ili uendelee kubebea mikaa na abiria
 
Mimi naamini kila gari linasimamiwa na Kiongoz aliyepewa dhamana na serikali. Likitumika vibaya kiongozi anapaswa kushughulikiwa lakini siyo waovu wachache warudishe juhudi za serikali kutoa huduma saa ishirini na nne.
Usipanic, hii nchi ni matamko tu hakuna utekelezaji
 
Mwisho, najiuliza hao watakaotembea usiku na gari za serikali watakamatwa na polisi na kuzuiwa?
Yes, utahojiwa unaenda wapi saa hii na gari la serikali kama kuna kazi maalum itajulikana tu, tena ilitakiwa hiyo kazi ya kukamata hayo magari baada ya saa za kazi wapewe polisi wa doria, askari anapoona gari la serikali mahali ambapo sio sahihi awe na uhalali wa kuhoji, dereva akishindwa kutoa maelezo gari linaperekwa kituoni.
 
Kwani gari ya serikali unaloliongelea ni ipi? Make naona unaondoa gari ya polisi kwenye list ya magari ya serikali. Inaonekana mtoa mada hajaeleweka vizuri.
Mtoa mada yeye shida yake ni huyo Mbunge kutoa kauli jumuishi kwa magari ya serikali bila kuangalia kuwa kuna magari mengine yanafanya kazi katika mazingira yanayosababisha masaa ya usiku yafike kabla hawajafika sehemu yao ya kupaki magari.
 
Watakachofanya sasa watakuwa wanabandua namba za serikali wanaweka za kiraia na bata wanakula mpk asubuhi na hakuna kitu mnacheweza kuwafanya
 
Kenya wana sheria kari sana za Magari ya Serikali na nahisi yote yana GPS hivyo yanafuatiliwa, Tanzania gari la Serikali ni mali ya Dereva
 
Tanzania wajinga ni wengi hivyo hawawezi kuwajibishana.Anayetakiwa kuwajibisha naye anafanya mambo yale yale anayofanya anayetakiwa kuwajibishwa.Unakuta kitu bila aibu limebeba nyasi za ng'ombe mchana kweupe but nobody cares.polisi wanaona,ras yupo na dada wake yupo.ukimwona RPC ni kama DC,ras,das,nk
 
Hapo wameipu tatizo la wizi wa mafuta kwa sababu dereva hatakubali kuliacha gari lina dizeli wakati wanapewa na serikal
 
Hivi najiuliza hii nchi kuna shida gani? Majuzi tu naona mkwara kuwa magari ya serikali baada ya saa 12 jioni hayaruhusiwi kuwepo nje. Cha kushangaza, madereva kama kawaida wapo wanakula nayo bata na hawaogopi.

Alafu ghafla unaona tena eti serikali inaagiza magari mengine ya sijui wakuu wa wilaya blah blah. Hivi mpaka watanzania wafanye nini ndio hawa wezi waelewe watu wamechoka na mambo ya hovyo?
 
Kausha basi ,,yanatusaidia jioni kupata utelezi,,,yani mwajuma akiona vieiti hachomoi
 
Siku utakapomkuta Dereva wa Serikali ameegesha gari kwenye eneo la starehe kwa muda ambao unakatazwa nakushauri jiridhishe kwa nini yupo maeneo hayo kwa wakati huo naamini utapata jibu zuri la swali lako.Pia ni vizuri ukafahamu kwamba baadhi ya Watumishi wa Umma wanawajibika kufutilia sehemu za starehe kwa wakati wanaona ni sahihi ili kutimiza wajibu wao.

Aidha, kuna baadhi ya Watumishi ambao huwa wanakuwa safarini mbali na vituo vyao vya kazi na kulazimika kupitia maeneo haya kwa ajili ya kupata chakula hasa nyakati ambazo migahawa ya kawaida huwa imefungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…