Huyu aliyekuwa mtangazaji maarufu Radio Deutsche Welle Swahili Service yuko wapi?

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,129
Reaction score
7,321
Ni Wajih Sheikh,..., namumiss sana. Allikuwa ni favourite wangu mkubwa sana. Ilikuwa waki-team up na Othman Miraji, utapenda kuwasikiliza bila kikomo. I really miss him!
 
Hawa wazee wamesha staafu..... nawakumbuka sana maana wakianza kutangaza taarifa ya habari lazima usikilize iishe yote.... walikuwa na mvuto sana na weledi wa hhali ya juu katika tasnia ya habari. Sijui kama tutapata watangazaji kama hawa ambao walikuwa wakiipenda sana kazi yao.

Wengi wamestaafu kama vile Ben Wazir, Abdul Wajih Sheh, Othmani Miraji, Ramadhan Ally....... aliye baki ambaye namfahamu ni yule mama aitwaye

Ni kama vile walivyokuwa akina David Wakati, Abdul Ngalawa, Jacob Tesha na wengine wengi wa R. T. D. ya enzi za mwalimu.
 
Wapi Othman Miraji!
nilikuwa napenda akiwahoji watu kwa discussion
 
Naelewa kaka anga zako wewe ni kwenye udaku, huko ndiyo huwa huchelewi kutoa majibu muafaka,... news za muhimhu na wewe wapi na wapi!

Sasa udaku uko wapi hapo? Wewe umeuliza huyo mtangazaji maarufu wa redio Dochi Velle yuko wapi. Nami nikakwambia waandikie Dochi Vele uwaulize alipo. Sasa kukwambia utafute taarifa za huyo mtu kutoka kwa mdomo wa farasi ni udaku? Hujitambui wewe!
 
Hawa wazee wamesha staafu..... nawakumbuka sana maana wakianza kutangaza taarifa ya habari lazima usikilize iishe yote.... walikuwa na mvuto sana na weledi wa hhali ya juu katika tasnia ya habari. Sijui kama tutapata watangazaji kama hawa ambao walikuwa wakiipenda sana kazi yao.

Wengi wamestaafu kama vile Ben Wazir, Abdul Wajih Sheh, Othmani Miraji, Ramadhan Ally....... aliye baki ambaye namfahamu ni yule mama aitwaye

Ni kama vile walivyokuwa akina David Wakati, Abdul Ngalawa, Jacob Tesha na wengine wengi wa R. T. D. ya enzi za mwalimu.

Nadhani anaitwa Oumilkheir Hamidou, Acha kabisa. Yaani nilikua nachelewa sana vipindi vya mchana shule ya msingi kwa kusikiliza DW. Ramadhani Ally akikuchambulia michezo, Othman Miraji akikupa darubini haubanduki redioni mkuu.
 
Wapi Othman Miraji!
nilikuwa napenda akiwahoji watu kwa discussion

0,,15713054_302,00.jpg

Kutoka Bonn, hiki ni kikosi cha Idhaa yako ya Kiswahili kinachokuletea moja kwa moja taarifa za habari, ripoti, uchambuzi na makala motomoto zilitafitiwa vyema, zilizopimwa na zisizoegemea upande wowote. Kutoka kushoto: Samia Othman, Nina Markgraf, Amina Abubakar, Pendo Ndovie, Sudi Mnette, Andrea Schmidt, Salma Said, Caro Tsuma, Othman Miraji, Abdu Mtullya, Oumilkheir Hamidou; Sekione Kitojo, Mohamed Abdulrahman na Daniel Gakuba.
 
Amestaafu mwaka jana october. Kweli alikuwa ana mvuto sana. Nilikuja fahamu baadae kuwa ni ndugu na marehemu prof Haroub Othman aliye kuwa UDSM.
 
Ni Wajih Sheikh,..., namumiss sana. Allikuwa ni favourite wangu mkubwa sana. Ilikuwa waki-team up na Othman Miraji, utapenda kuwasikiliza bila kikomo. I really miss him!

It's so sad, mkuu Wajih Sheikh alishatangulia mbele ya haki, nadhani kwenye 2008 kama sikosei. Umenikumbusha mbali sana ubarikiwe.
 
Nadhani anaitwa Oumilkheir Hamidou, Acha kabisa. Yaani nilikua nachelewa sana vipindi vya mchana shule ya msingi kwa kusikiliza DW. Ramadhani Ally akikuchambulia michezo, Othman Miraji akikupa darubini haubanduki redioni mkuu.

Umenikumbusha mbali sana mkulu...... teh....teh..... kuna mmoja Abdul Wajih Sheik alikuwa akituletea kipindi cha Afya yako, na pia huyu mama Oumilkheir Hamidou alikuwa mbiu ya mnyonge..... na pia sura ya Ujerumani.....Pia Manase Lukungu, Petra Schitain (sijui kama jina nimelipatia, alikuwa mama mmoja wa kijerumani alikuwa akitangaza kiswahili)du hii timu ilikuwa kamili pale DW redio...... kila mmoja alimudu vilivyo namba yake.......

DWredio imechangia sana kunifanya niielewe dunia na siasa, sayansi, mazingira, jamii, uchumi, n.k........ nimeanza kuisikiliza tangu nikiwa kijana mdogo mnamo mwaka wa 1982. Kipindi hicho nakumbuka walikuwa wakitumia alama fulani ya kipindi (ala ya muziki ambayo hupigwa kabla ya kuanza matangazo-taarifa ya habari) ambayo ilikuwa ikinisisimua sana na kunifanya nisitoke kusikiliza vipindi vyote vya siku hiyo (yaani muda wa dk 50 hivi).

Nakumbuka pindi hiyo nilikuwa nikiwasiliana nao sana kwa barua..... pia no DW walinitumia zawadi nyingi..zikiwemo kalenda, picha za watangazaji, picha za majengo, pindi hiyo walikuwa mjini Munich kabla ya kuhamia Bon.

Kwa kweli nilifurahia sana redio DW.

It's so sad, mkuu Wajih Sheikh alishatangulia mbele ya haki, nadhani kwenye 2008 kama sikosei. Umenikumbusha mbali sana ubarikiwe.

Hapana mkulu, sijasikia kuwa Abdul hatunaye tena....... mbona utafikiri alistaafu mwaka 2010? Ngoja nifuatilie zaidi......
 
0,,15713054_302,00.jpg

Kutoka Bonn, hiki ni kikosi cha Idhaa yako ya Kiswahili kinachokuletea moja kwa moja taarifa za habari, ripoti, uchambuzi na makala motomoto zilitafitiwa vyema, zilizopimwa na zisizoegemea upande wowote. Kutoka kushoto: Samia Othman, Nina Markgraf, Amina Abubakar, Pendo Ndovie, Sudi Mnette, Andrea Schmidt, Salma Said, Caro Tsuma, Othman Miraji, Abdu Mtullya, Oumilkheir Hamidou; Sekione Kitojo, Mohamed Abdulrahman na Daniel Gakuba.

Nimefurahia sana mkulu..... kama unaweza tupe kikosi cha akina

Manase Lukungu

Abdul Wajih Sheikh

Ben Wazir

Othman Miraji

Umilkheir Hamidou

Shaban Muhamad Shangama

Erasto Mmbwana

Mohamed Dahaman

Mohamed Abddulhaman

Martin Mule

Kalenga Ramadhani (ambaye baadaye alikuja kuwa waziri wa habari wa Burundi)

Richard Madete.

Ni Wajih Sheikh,..., namumiss sana. Allikuwa ni favourite wangu mkubwa sana. Ilikuwa waki-team up na Othman Miraji, utapenda kuwasikiliza bila kikomo. I really miss him!

Mkulu ikiwezekana badilisha kichwa cha habari kisomeke Marafiki wa DW Radio
 
It's so sad, mkuu Wajih Sheikh alishatangulia mbele ya haki, nadhani kwenye 2008 kama sikosei. Umenikumbusha mbali sana ubarikiwe.

Naweza nikakubaliana na wewe, maana kapotea ghafla tu! Too bad!
 
Mkulu ikiwezekana badilisha kichwa cha habari kisomeke Marafiki wa DW Radio

Hivi kwenye system hii kuna permissions za ku-edit heading ya thread uliyoanzisha? Sijawahi kuwa previledged nazo
 
Nimefurahia sana mkulu..... kama unaweza tupe kikosi cha akina

Manase Lukungu

Abdul Wajih Sheikh

Ben Wazir

Othman Miraji

Umilkheir Hamidou

Shaban Muhamad Shangama

Erasto Mmbwana

Mohamed Dahaman

Mohamed Abddulhaman

Martin Mule

Kalenga Ramadhani (ambaye baadaye alikuja kuwa waziri wa habari wa Burundi)

Richard Madete.

Hapo kwenye red: Jamaa ana sauti nzito halafu nzuri utadhani ni ya malaika. Yaani hawa jamaa watangazaji wao ni mahiri hakuna mfano. Halafu Abubhakahar Liongo naye walishamchukua ila nina siku kadhaa sijamsikia akisoma news, bado wako naye kweli?
 
Back
Top Bottom