Huyu bibi enzi za usichana wake nadhani alikuwa kama tractor

Huyu bibi enzi za usichana wake nadhani alikuwa kama tractor

'Hobby' ya wanaolalamika hawana kazi , maisha yanawapiga ni nini? Kufuga kuku nimetolea mfano, kuliko kuaibika huna hela ya kula 'hobby' ya kufuga kuku au kulima mchicha haiwezi kusaidia?
Kama 'hobby' zingekuwa zinaingiza kipato,, dunia ingekuwa peponi.
Hujui unachokiongea, ila jua tu kitu chochote ukifanya kwa kusukumwa na njaa huwezi fika popote
 
Ni bibi Mzee
Kapinda mgongo na dental formula imebaki nusu.
Mvi kichwa Kizima.

Leo nimemfuatilia nimeshangaa

1: anafuga Kuku na kuwahudumia mwenyewe. Sio Kuku tu Bali hata mzinga na kanga. Anatotesha na kuvilea vifaranga mwenyewe bila msaada.

2: Anaamka asubuhi anafagia Nyumba nzima. Anafuta vumbi na kudeki.

3: Jioni anakimbia kanisani mazoezi ya kwaya kwa wakati na hachelewi.

4: Anajaza Maji kwenye matank na kuhakikisha choo na bafu ni visafi.

5: Anapata Muda wa kusoma kutanua ubongo. Vitabu mbalimbali.

6: Saambili anapata muda wa kuangalia Habari ili asiachwe nyuma.

7: Anapata Muda wa kupigia Simu watoto wake na wadau mbalimbali kusocialize.

8: Anaamka mapema SAA kumi na moja kuanzia siku.

9: Analimisha Mashamba na Bustani za mbogamboga.



Wako wapi mabinti wenye Viwango angalau vya bibi
Picha tafadhali
 
Weka picha basi
Nimekuona kwenye nyuzi nyingi unaomba picha ziwekwe,kwa bahati mbaya watu wengi hawafahamu namma ya kuweka picha.Ninaomba ikikupendeza ufungue thread ya kueonyesha jinsi ya kuweka picha JF ingependeza ungetumia picha zako kufundishia
 
Mabinti njooni PM. Niwalink mkapate kitcheni party za Maana kutoka kwa huyu kunga.

You will never be the same again
 
Back
Top Bottom