Huyu binti atanifanya niwe masikini

Huyu binti atanifanya niwe masikini

Nimetembelewa na mdada mrembo (pisi kali kweli), kwa sasa anakaribia wiki kukaa hapa kwangu. Anategemea by jumapili ijayo aweze kuondoka.

Tangu amefika kwangu, hela imekuwa haitulii. Kila siku hela inatoka tu, na mbaya zaidi anaujauzito wangu unaokaribia mwezi.

Leo atakuambia, naomba hela ya kusafisha kucha, mara hela ya kunyoosha wigi, mara nipe hela kidogo nitume nyumbani, mara hela ya mafuta ya kung'arisha ngozi yanagharimu elfu 60, mara nipe hela nikanunue chakula, na akishanunua hicho chakula hali; mpaka nyumba imekuwa na mabaki ya vyakula ambavyo havijatumika.

Mbaya zaidi, majuzi aliniomba twende 'club' kwa sababu ni mtu anayependa sana mziki; kwa upande wangu nikawa sijisikii vizuri, nikamwambia siwezi kwenda. Akanilazimisha, ikabidi nimruhusu yeye mwenyewe aende.

Alipoenda huko kwenye starehe akajisahau kurudi nyumbani; nikawa nampigia simu mpaka saa saba usiku hajarudi; kwa hasira, nikachukua nguo zake nikaanza kuzichana chana, kwa kuhisi labda yuko na mtu mwingine.

Asubuhi, akarudi huku anamajeraha mkononi; kwa sababu alipata ajali ya boda boda usiku wakati akirudi nyumbani. Wasamaria wema, wakambeba na kumpeleka hospitali kwa sababu alikuwa amezimia.

Baada ya kunipa hayo maelezo; ilibidi niende hospitali pamoja na kulipa bill. Lakini roho ikawa inaniuma, kwa kusababisha uharibifu kwenye nguo zake.

Ikabidi niingie gharama ya kumnunulia mavazi upya; hapa natamani hata leo aondoke, kutokana na hasara anazonipa.
Pole sana mkuu. Ila ID yako tu inaonyesha wewe ni mwana mahesabu. Hutaki hasara.
 
We pesa unayo mzee au una mbwela mbwela hapa kutafuta misifa ,mr misifa.

Masikini ndio huwa wanajiona wana hela na tambo za kijinga sababu hawajui thamani ya pesa na kazi yake.

Matajiri hutulia kimya wakikusoma 60k ni mtaji wa tosha

Acha ngendembwe

kk kama huna pesa ww ndo wote pole usinifikilie vbaya,bcoz,uliniazma,nikakuambia sina pole yako
 
We pesa unayo mzee au una mbwela mbwela hapa kutafuta misifa ,mr misifa.

Masikini ndio huwa wanajiona wana hela na tambo za kijinga sababu hawajui thamani ya pesa na kazi yake.

Matajiri hutulia kimya wakikusoma 60k ni mtaji wa tosha

Acha ngendembwe jibaba
KK kama huna pesa ww ndo woteee au kwa vile uliniazma,pesa nikakuambia sina polee sana huna pesa find your level simple advise
 
Bro kama unazo hizo tuliza kitenesi acha mbwembwe na ngendembwe

Unaleta dharau kisa wewe unazo hela

Wewe unanijua mimi !?

Unanijua naingizia kiasi kwa mwezi!?

Yawezekana wewe una hela za kuchezea hii haina maana wengine wachezee hela zao.

Kila mtu na priorities zake

Jifunze kuhesheme misimamo ya wenzako katika pesa
 
Namjua huyo msichana anaitwa Soreiya ni shombeshombe fulani hivi anasoma chup cha diplomasia.
 
Nimetumia hii mbinu, ameweza kuondoka
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] umeona mkuu nilijua tu Kwa hii mbinu niliyokupa hawezi kuchomoa wauni sio watu wazuri big up sana kamanda[emoji120][emoji123][emoji123]
 
Kuwa makini na hii ndoto yako usije ota kwa hasira unakata kikojoleo chako. Maana vijana wa siku hizi hamueleweki

Back
Top Bottom