Kwa levo aliyokuwa amefikia pale Simba hakufanya maamuzi sahihi kwenda Yanga tena kwa mbwembwe zile na kulazimisha kwiiingi. Mara agomee mazoezi mara achelewe kambini mara abishane na kocha wa viungo, mara atupe mpira chini kwa hasira mbele ya watazamaji ili mradi visa tu kama mke anayelazimisha talaka. Kila wakati afanye makosa yeye tena makusudi halafu viongozi wambembeleze yeye. Kwa kiasi fulani yeye na Mkude waliharibu nidhamu ya timu kwa ujumla.
Sasa huko Simba anakotaka kurudi si tayari kumeshajaa. Kweli uwezo bado anao lakini kitendo cha kumrudisha kitawakatisha tamaa vijana walioanza kujipata kama Ahoua ambao kiasi wamewafanya wanasimba waanze kumsahau Chama taratibu na mashabiki sasa wameanza kukubali uhalisia kuwa Simba inaweza kwenda mbele bila ya Chama.
Anyway maamuzi tuwaachie viongozi wa Simba na Mo.
Ni mtizamo tu.