Huyu Dada kaongea ukweli wa kutisha kuhusu Familia za Kiafrica

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Dada anasema muda pekee ambao, Familia nyingi za Kiaafrica huwa pamoja ni wakati ambao wanajiandaa na msiba, Ila Hata siku moja Familia haiwezi kukaa pamoja ili kuanzisha biashara au project itakayo saidia ndugu zao ambao ni unemployed.

Ndungu wengi sana hupenda kuona baadhi ya ndugu zao wanapata shida ili waendelee kunyenyekewa.

Hii ni tofauti kwa Wahindi, Wachina na hata Waarabu, ingawa pia Wasomali wanajitahidi sana kwa hili.

Cha Kushangaza unakuta ndugu wana compete kwenye the same biashara, wote wana milik Mabasi, au wote wana Maduka ya Hardware.
 
Jamani wekeni qualifiers kwenye hizi posts zinazotujumuisha waafrika wote kuwa fungu moja.

Tukianza kufunguka ukweli wetu wengine hapa mtaona tunajitapa kama posts za Pedejee Kidukulilo.
 
Usilolijua sawa na usiku wa giza hakuna watu wanaochukiana kama wachina tena afadhali waafrica wanaedit kidogo chuki!unajua unaweza kusema fulani yupo vizuri ni kwa vile hujui tu anachopitia
 
Huyo Mdada ameigusa family yangu km anatujua nnakumbuka nilimaliza chuo nikakaa mtaani miaka kibao kila nikiomba support niongezewe mtaji kidogo watu wanakausha au wanasema mambo magumu huku watu wanafulumusha mijengo tu Mimi nnakaa Saa nyengine hata vocha Inakua mtihani halafu mbaya zaidi ukiwa na ndugu wenye uwezo na wanajulikana ukoo mzima Hakuna atakaye kusaidia, ukimlilia mtu shida anacheka Anaona utani akiangalia status ya ndugu zako.
 
Kuna ugumu sana familia zetu kuendelea maana kila mtu chake anawaza akaanze kujenga nyumba yake kivyake, biashara zake kivyakeee na menginge kibao.
 
Hatuwezi kulazimishana, wahindi hawawezi kuwa waafrika na waafrika hatuwezi kuwa kama wahindi, sisi waafrika ndiyo tunaishi maisha halisi ya mwanadamu anavyotakiwa kuishi.
 
mwogope sana mtu mwenye njaa..
 
Ni ukweli wote. Na hii imeniamsha hata mimi binafsi. Tatizo la wafrika tabia mbaya sana. Wana familia wengine hata uwanyanyue vipi hawanyanyuki. Wewe wakati unataka kupanga familia ili kuboresha maisha mwenzako kila mwaka ni mjamzito. Sasa huyu tutsafiri naye dumila kufungua mashamba ya mahindi kweli?
 
Familia nyingine ni za kishenzi kweli kweli. Ukijichanganya kuwaunganisha, wanaungana kukumaliza kwanza wewe.
 
Kuungana sawa, lakini unaungana kibiashara na mtu mwenye mtaji, sasa kama mtu hana mtaji unamsaidiaje ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…