Huyu dogo kanishangaza sana, hata mimi nilikuwa hivi ila yeye kazidi

Buffet

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
639
Reaction score
1,571
Mapema wiki hii nilikuja kijijini kuwaona wazee huku Bariadi, sasa siku ya Jana asubuhi nilitoka na mzee tukaenda mjini,tulirudi mida ya jioni saa kumi na mbili,ule muda mifugo inarejeshwa nyumbani toka machungani.

Aisee tumekaa pale tumetulia ng'ombe wakiwa wanaingia zizini kuna dogo ana umri wa miaka kumi na mbili (mtoto wa dada) anakaa pale home, wakati ng'ombe wanaingia zizini yeye anawacheki kwa makini sana,mwishoni kabisa akaja pale tulipokuwa tumekaa akasema uncle kuna ng'ombe watatu hawapo kwenye kundi lote hili,akawataja kwa majina wale ng'ombe waliomiss,kweli walipohakiki hawakuwepo,na walipoenda kutafutwa porini walipatikana.

Kilichonishangaza ni kwamba huyu dogo anawafahamu ng'ombe 860 kwa majina (kuna ng'ombe wengine wana majina ya viongozi),nilitaka anifundishe majina ya ng'ombe wote,alianza kunionesha na kuwataja majina alipofikisha ng'ombe mia nikamwambia inatosha,nilielezwa kuwa yule dogo katika kundi lote la ng'ombe wa babu yake ndiyo pekee anaweza kunotice kwa haraka sana kama kuna ng'ombe hata mmoja atamiss,nilishangaa sana ule uwezo wake,nikawaza huyu atakuja kuwa Kiduku LILO
 
Vitu vya kuona ni tofauti na vitu vya kufikili, na kwa tulio wengi tunaamini akili za darasani.

Hiyo ni experience tosha kwamba dogo anaakili ya utambuzi, tuambie darasani anafaulu kwa kiwango gani.?
 
Sio kawaida kichwa chake kina uwezo mkubwa wa kuprocess na kuhifadhi data zaidi yenu..ila kwakua amezaliwa bara la giza imebidi atumie kipaji chake kukariri ng'ombe wakati kwa wenzetu NASA na CIA wangepiga hodi mapema kujichukulia Asset yao
 
Ng'ombe 860? Mbona wengi sana.
Pengine hao ng'ombe huwa ni wasumbufu, au anawapenda sana au hawapendi.. Yaani namaanisha hao ng'ombe waliopotea lazima wana sifa fulani ambapo ilimfanya dogo kuto notice uwezo wao.
usikute ni chai tu
 


Kila mtu ana kipaji chake hapa duniani. Wazazi wangu wana shamba boy kama huyo dogo, yaani fogo anajuwa kila aina ya ufugaji kuanzia kuku wa kienyeji, kuku wa mbolea (kizungu), mbuzi na ng'ombe. Tuna mifugo mingi sana na huyo dogo is only 16 yrs old lakini siku akikosekana atatafutwa kwa udi na uvumba aede kusimamia mifugo. Wenzake ambao ni wakubwa kwake wanamuonea wivu wakati hawajuwi chochote zaidi ya kulisha tu hiyo mifugo,
 
Hua siamini katika namba tatu.

Yaani mfano mtu aseme 'Basi akampiga ngumi ya kwanza, ya pili, ya tatu chali' au 'Nilivyomchunia nikakaa siku ya kwanza, ya pili, ya tatu mwenyewe akapiga'

Na hapo mifugo iliyokosekana mitatu au siyo? Hii stori ina chembechembe za uongo.
 
Ng'ombe 860? Mbona wengi sana.
Pengine hao ng'ombe huwa ni wasumbufu, au anawapenda sana au hawapendi.. Yaani namaanisha hao ng'ombe waliopotea lazima wana sifa fulani ambapo ilimfanya dogo kuto notice uwezo wao.
Naamini inawezekana. Kutokana na yeye kukaa nao kwa muda mrefu Basi amezoea sifa ya kila ng'ombe kuanzia rangi yake mpaka tabia zake. Maana hata hayo majina yao lazima tu yanaakisi sifa/tabia zao. Nikiwa nasoma nilikuwa na uwezo wa kufahamu wanafunzi shule yote kwa majina yao. Hii pia imenifanya nikumbuke nikiwa O-level mkuu wangu wa shule alikuwa ni mhindi, amefika hapo shuleni hata hajamaliza wiki, unaokutana naye njiani anakusalimia kwa kutaja jina lako pasipo hata wewe kumtajia jina lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…