Mapema wiki hii nilikuja kijijini kuwaona wazee huku Bariadi, sasa siku ya Jana asubuhi nilitoka na mzee tukaenda mjini,tulirudi mida ya jioni saa kumi na mbili,ule muda mifugo inarejeshwa nyumbani toka machungani.
Aisee tumekaa pale tumetulia ng'ombe wakiwa wanaingia zizini kuna dogo ana umri wa miaka kumi na mbili (mtoto wa dada) anakaa pale home, wakati ng'ombe wanaingia zizini yeye anawacheki kwa makini sana,mwishoni kabisa akaja pale tulipokuwa tumekaa akasema uncle kuna ng'ombe watatu hawapo kwenye kundi lote hili,akawataja kwa majina wale ng'ombe waliomiss,kweli walipohakiki hawakuwepo,na walipoenda kutafutwa porini walipatikana.
Kilichonishangaza ni kwamba huyu dogo anawafahamu ng'ombe 860 kwa majina (kuna ng'ombe wengine wana majina ya viongozi),nilitaka anifundishe majina ya ng'ombe wote,alianza kunionesha na kuwataja majina alipofikisha ng'ombe mia nikamwambia inatosha,nilielezwa kuwa yule dogo katika kundi lote la ng'ombe wa babu yake ndiyo pekee anaweza kunotice kwa haraka sana kama kuna ng'ombe hata mmoja atamiss,nilishangaa sana ule uwezo wake,nikawaza huyu atakuja kuwa Kiduku LILO