Mungu ni wa ajabu sana, unaweza usikute asifulie..
Kwa imani yangu mimi mungu anapokupa ama kukunyima huwa vyote ni mitihani na katika mitihani yote aidha umshukuru ama umkufuru..
Wapo wanaopewa wanamshukuru mungu na wengine wanamkufuru mungu
Wapo wasiopewa wanamshukuru mungu na wengine wanamkufuru mungu. Najua nimeeleweka japo kwa uchache.
Mtu anapewa anashukuru anajua mali zinatoka kwake mola wetu mlezi na wala hazitumii vibaya, anatumia kwa njia ile inayompendeza allah huyu ni mwenye kufaulu, wapo wenye mali wanatumia kwa njia mbaya huyu ni mwenye kufeli
Na ndio maana tunafundishwa tunapoomba mali, tumuombe mungu atupe mali ambazo hazitakuwa mtihani kwetu, mali ambazo hazitatushinda nafsi zetu, mali ambazo hazitotupelekea kukufuru.
Kuna kisa kimoja cha nabii nadhani ni musa(a.s) alimuomba mungu yeye mussa ndio awe mgawa rizik allah akamkatalia musa akang'ang'ana, allah akataka kumuonesha kitu akamwambia musa aende akasimame sehemu hapo ndipo atakabiziwa hiyo kazi rasmi basi musa akaenda pale, muda si mrefu baada ya kufika eneo lile wakatokea watu wamekuja kuzika, walipomaliza Wakaondoka, muda si mrefu wakaja watu wakaifukua ile maiti wakaizini mussa aligadhabika mnoo, ila hakwenda kufanya kitu sababu alikuwa anasubiri jambo la msingi ambalo akikabidhiwa kirungu watu watamkoma, walipoondoka baada ya muda kupita mungu akamuuliza musa je watu wale unafanyaje, musa akajibu km akipewa yeye hyo kazi watu wale hawapati abadani asilani, mungu akamjibu kuwa hyo kazi haiwez, sababu yeye mungu anawapa wenye kumshukuru, wenye kumkufuru wacha mungu n.k.
Sasa wewe ndugu yangu unaweza ukaomba mwenzio afulie ndio akazidi kupiga mpunga, inakera ila ndio maisha yake.. [emoji23][emoji23][emoji23]
Sent using
my nokia ya tochi