Habarin wa jf natumaini mko powah kabisa
Huyu fundi simu amenishangaza sana mbaka nimeona nilete uzi huu kwa wale wa hanga wa simu mbovu mnao shinda kwa mafundi iko hivi mimi nina jamaa angu fundi simu wa hapa town maeneo flani iv sasa huwa nakuja hapa mara kwa mara kupiga story na mambo mengine
Nimekaa hapa kama dk 30 iv hakaja mama mtu mzima age 38+ kaleta simu yake imezima haipeleki chaji sasa fundi akamwambia basi ngoja niishugulikie baada ya nusu saa uje uchukue ukiangalia ofisi yenyewe sehemu ya kuka mteja aseme asubiri amna ko lazima aeende arudi basi kama baada ya dk 10 iv simu ikawaka fresh ndo jamaa kunishtua oyah plus njoo uone vitu iv daha jamaa akaanza kunionesha video za utupu ambazo kazikuta kwenye trash ya google photo, watu wengi watumiaji wa simu wanafutaga video kwa mazoea kumbe video zinaeenda trash na kule zinajifuta baada ya siku 60 kwa google photo kama sijakosea
Baada ya kunionesha video na picha jamaa angu akaamia kusoma message aisee hapa nikabaki hoi sasa jamaa mbaka message nikawaza na mimi simu yangu ikiharibika itakuaje na sina tabia ya kufuta message kabisa na kwa huyu jamaa angu inaonekana ni tabia yake maan kanisimulia mambo aliyo yaona kwenye simu ya mzee fulani ninae mfahamu aliyeenda kurekebishiwa simu yake
Niwashauri tu kama unatengeneza simu simamia simu yako ikamilike izo tabia za kumuamini fundi itawa gharimu fundi haaminiki ikiwezekana simu ikiharibika weka ndani nunua simu nyingine