Huyu governor aliyeamua kwenda mafichoni anastahili kupewa bail kweli?


Hapa kwa kweli sielewi ni kwanini unapingana kuhusu jambo ambalo liko kwa public domain. La kwanza, ni wapi umeona nikileta siasa? Yaani tayari ushajijazia kuwa niko biased dhidi ya DPP eti kisha nimemkosoa? Hamna warrant of Arest hapo. Ni hakimu gani aliyetoa warrant of arrest hiyo? Twitter ya DPP yenyewe inasema hapa. Soma ukurasa wa tatu unasema "Accordingly, I direct that the following be arrested". Kuna neno warrant of arrest hapo? Kuna jina la hakimu yeyote hapo?

 

Naomba unisaidie kuelewa unachobishia nini haswa, kwamba DPP hakupaswa kutoa hati ya kumkamata jamaa, au kitu gani hakikukuridhisha kwenye hili zoezi.
Binafsi sijali hata kama DPP/EACC/Uhuru au yeyote yule yupo kwenye harakati za kutafuta umaarufu, nategemea kuskia mafisadi wanapatwa na mchecheto, hofu ya pesa za umma iwaingie, na kama kufanikisha hilo itabidi wawe wanakamatwa Ijumaa ili walalie sakafu kwenye jela hadi jumatatu, basi na iwe hivyo.
Viongozi kutafuta umaarufu ni jambo la kawaida, na pia kupata uungwaji mikono na jamii kunahitaji ufanye mbwembwe za aina fulani, lakini cha msingi ni kutimiza malengo.
 
Acha tungoje Gavana Waititu afike mbele ya hakimu. Tuone kama kesi hiyo itatupiliwa mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…