Huyu jamaa angu hana hamu na UDSM kwa hiki alichokipata

Huyu jamaa angu hana hamu na UDSM kwa hiki alichokipata

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kwanza shule zina wenyewe wengine nyota zao ni kuchunga mbuzi na biashara huko tusforce mambo
Umepita mlemle utafikiri unanifahamu vizuri.
 
Huyo jamaa ako kilaza, pamoja na kuwa in service lakini niliwanyoosha class balaa.

Screenshot_20210824-154744_Chrome_resized.jpg
 
Dah udsm huwa pagumu na umri ukishaenda Plus mambo mengine ya maisha desa halipandi angeenda vyuo vya kata asinge disco
 
Miaka 38+ anaforce kusoma udsm tena undergraduate, hicho alichokipata ni stahili yake nadhani.
 
Kwema wasomi?

Kuna jamaa angu ni in service wa halmashauri moja hapa Tanzania, mwaka 2019 alinifuata kuniomba ushauri wa program na chuo cha kusoma hapa Tanzania, kwa uelewa wangu kiasi niliokua nao kwa kipindi hicho, nikamahauri ni Bora atafute chuo cha private walau huko kunakua na unafuu na angalau hatajiumiza sana ukizingatia ni mtu mzima kiasi(38+), yeye akaona kama namzibia ridhiki coz ndoto zake zilikua kusoma uchumi UDSM.

Kweli akaomba chuo akapata udsm BA ECONOMICS. Mwaka wa kwanza umeenda vizuri kiasi, mwaka wa pili umekua mbaya sana,kwani kapigwa discontinue, so hapa kanitumia matokeo yake ili nijaribu kumshauri nini cha kufanya. Anasema anaona hata aibu kumwambia mkewe kuwa kaliwa kichwa huko chuo.

Matokeo yake nitayaweka hapa ili mtoe mawazo yenu wakuu coz mimi binafsi nimemshauri aachane na mambo za kusoma kwa sasa aangalie maisha yake na familia yake tu.

View attachment 1974214
Mshauri atafute vyuo Ulaya au Amerika. Huko hakuna ujinga wa kuumizana kama kwetu ambapo maprofesa wazima wanataka waabudiwe na wapo pale kujonyesha wamesoma sana na kufelisha wenzao badala ya kuwasaidia. Ni aibu kwa chuo mwanafunzi kufeli tena mtu mzima anayejua anachofanya. Nadhani kuna aina fulani ya roho mbaya. Nilisoma pale sheria profesa mmoja mpumbavu aitwaye Kanywanyi akataka kunifelisha nikamzidi akili nikampigia na akashangaa. Kosa langu ni kwamba alisikia wanafunzi wenzangu waliokuwa wanasua sua nikawasaidia wakiniita profesa. Bahati nzuri baada ya hapo nilisomea nje na kumaliza shahada zangu zote vizuri bila pressure
 
Mwaka wa pili huwa mgumu sana sababu unafundishwa uhalisia wa course yenyewe sababu mwaka wa kwanza unafundishwa msingi wa course kwa hiyo ni pata shika nguo chanika vinginevyo uwe unasoma course ambazo unaenda kupiga paper ukitokea bar kugonga biere na huna mashaka yoyote kusoma kwao wanaita kugusa gusa au kupitia pitia notes na kufauru[emoji23][emoji23][emoji23].
 
Kwema wasomi?

Kuna jamaa angu ni in service wa halmashauri moja hapa Tanzania, mwaka 2019 alinifuata kuniomba ushauri wa program na chuo cha kusoma hapa Tanzania, kwa uelewa wangu kiasi niliokua nao kwa kipindi hicho, nikamahauri ni Bora atafute chuo cha private walau huko kunakua na unafuu na angalau hatajiumiza sana ukizingatia ni mtu mzima kiasi(38+), yeye akaona kama namzibia ridhiki coz ndoto zake zilikua kusoma uchumi UDSM.

Kweli akaomba chuo akapata udsm BA ECONOMICS. Mwaka wa kwanza umeenda vizuri kiasi, mwaka wa pili umekua mbaya sana,kwani kapigwa discontinue, so hapa kanitumia matokeo yake ili nijaribu kumshauri nini cha kufanya. Anasema anaona hata aibu kumwambia mkewe kuwa kaliwa kichwa huko chuo.

Matokeo yake nitayaweka hapa ili mtoe mawazo yenu wakuu coz mimi binafsi nimemshauri aachane na mambo za kusoma kwa sasa aangalie maisha yake na familia yake tu.

View attachment 1974214
Sasa angesoma SUA ingekuaje kama Ud ame disco?
 
Back
Top Bottom