Huyu Jamaa Hakuna Rekodi Atakayoiacha Salama!

Huyu Jamaa Hakuna Rekodi Atakayoiacha Salama!

Naye si mwingine bali ni Meddie Kagere a.k.a MK14. Mpaka sasa katika ligi zote dunia hii hakuna kama yeye. Kwanini? Ungana nami.
Huyu mnyama mpaka sasa kafunga goli 10 peke yake. Mchanganuo wa hizo goli ni kama ifuatavyo;
1. Goli 3 kafunga kwenye ligi kuu
2. Kombe la Kagame katupia goli 4
3. Katika michezo ya kirafiki katupia goli 2
4. Timu ya Taifa Rwanda huko katupia goli 1, ambalo naamini mwakani FIFA watamkabidhi tuzo yake ya goli bora la mwaka.
Just imagine, September hii tu jamaa ana goli 10, ikifika mwakani mwezi wa 5 ambapo ligi zitakua zinaisha si atakua katupia goli zaidi ya 107?
Huyu jamaa hakuna rekodi yoyote ambayo ataiacha salama, mfano;
1. 30/09/2018 jamaa anaenda kuvunja rekodi ya King Kibaden ya kutupia Hat-Trick dhidi ya Ndala iliyodumu miaka na miaka.
2. Si mpaka ligi iishe, ni hapo mwakani mwanzoni tu, Meddie Kagere atakua ni mchezaji pekee aliyewahi kufunga goli nyingi katika ligi kuu ya Tanzania.
3. Messi (Eeeeh, huyo huyo wa Barcelona) naye hataachwa salama. Ifikapo May mwakani, Kagere atakua ni binadamu pekee aliyewahi kufunga goli nyingi ndani ya msimu mmoja.
Huyo ndo Meddie Kagere.

"Aminini Nawaambia 30/09/2018 Baada ya Shoo ya Kagere Taifa.. Kuna Watu Watasahau Makwao" - sembo

Nikiripoti toka viyunga vya Kigali hapa Rwanda.. Ni Mimi sembo wa Simba TIIIIIIIIVIIIIIIIIIIIIIIIII (in George Malatu Voice)
Ni mapema sana, kuna msimu moto kama huu alianza nao Anelka kule darajani mwisho wa siku kiatu wakabeba wenye nacho.
Tulia tu, kuna ishu za majeruhi pia, huwa zinavunjaa mipango kama hii, akamuulize Neymar
 
medie kengele
Age :40yrs
Halafu anawaambia ana miaka 31!!..ina maana hata yondani ni mkubwa kwake!
Sio huyu
IMG-20180920-WA0017.jpeg
 
Avunje kwanza zile rekodi za Mavugo ulizokuwa unatuambia miaka 2 iliyopita ?
Mikoani kuna suala la ubora wa viwanja.
Kagere atakata pumzi mapema tu kama Dan Sserunkuma..mark my words
Umehamia Kwa Kagere tena? Vipi Okwi?

Huyo Magere wako usimwamini asbh hiii, ndio mech mbl kacheza.lig ndio imeanza.

Huyo Kagere wa kawaida sana
Leo kacheza utumbo mpaka kocha kaona amtoe tu
Ndio anaanza kupotea hivyo
Ni mapema sana, kuna msimu moto kama huu alianza nao Anelka kule darajani mwisho wa siku kiatu wakabeba wenye nacho.
Tulia tu, kuna ishu za majeruhi pia, huwa zinavunjaa mipango kama hii, akamuulize Neymar
Hana lolote ni wa kawaida sana anakabwa mpaka na mabeki wa Ndanda!!!
Huyu ndugu yangu tayari atakuwa katika eneo korofi kuhusu suala zima la mtandao.
medie kengele
Age :40yrs
Halafu anawaambia ana miaka 31!!..ina maana hata yondani ni mkubwa kwake!
Na sisi tunakutunzia rekod yako hii tutakukumbusha
Watani zangu.. Nawatakia maandalizi mema ya J3.
 
Back
Top Bottom