Huyu jamaa, namshangaa sana!

Huyu jamaa, namshangaa sana!

mathsjery

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2015
Posts
2,249
Reaction score
1,813
Okay, Kuna jamaa yeye huwa anafanya kazi akiwa na shida ya hela akipata hafanyi mpaka ziishe yaani anaweza nunua tv, sofa na kitanda lakini pia akanunua mahitaji ya nyumbani, basi anaweza kaa, kaa bila kufanya kazi na king'amuzi chake cha Dstv mpaka yakaisha na ikikaribia mwisho wa mwezi anauza tv au godoro analipia pango kisha anaanza kutafuta tena



Hii imekaaje?
 
Anafanya kazi gani?

Hii kitu hutokea kwa watu wanaopiga deal moja linaingiza pesa nyingi kwa wakati mmoja!!! Wachimbaji, wavuvi, wazee wa kubet, n.k Ila kazi hizi za kuganga pesa ya kula lazima upige kazi kila siku la sivyo hutakula.
 
Anaiga maisha ya marehemu TUPAK huyo, alikuwa akipata hela anaitumbua hadi iishe ndio anaingia mzigoni kutafuta tena
 
Anajua kuishi wakati uliopo huyo jamaa
 
Okay, Kuna jamaa yeye huwa anafanya kazi akiwa na shida ya hela akipata hafanyi mpaka ziishe yaani anaweza nunua tv, sofa na kitanda lakini pia akanunua mahitaji ya nyumbani, basi anaweza kaa, kaa bila kufanya kazi na king'amuzi chake cha Dstv mpaka yakaisha na ikikar ibia mwisho wa mwezi anauza tv au godoro analipia pango kisha anaanza kutafuta tena



Hii imekaaje?
Laana za ukoo
 
Nikajua ni mwizi kumbe anatafuta akipata anatumia akikosa anaviuza vitu vyake.Katengeneza life zuri sana.
 
Maisha ya watu wa mawe hayo..
Akiotea korongo ananunua asset za kutosha.hata nyumba au viwanja kisha chenji zikibaki ndio anakula bata.siku zikiisha zile asset anauza kwa hasara tena pungufu mara 2 ya bei alizonunilia.

Mmoja aliwanunulia wazazi wake nyumba wakampa na baraka kwamba mtoto wetu ss amekuwa na akili.

Siku hela imekata akauza nyumba akatokomea kusikojulikana.wzazi wakarudi kijijini.
 
Haeleweki kama hii picha
FB_IMG_16357685162739964.jpg


Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Huyu anawaza maisha ya Akhera dunia tunapita,🤣🤣🤣

Watu kama hao wanajiamini mno
 
Tunaendana nae kabisa nikikosa hela ndo akili inapata Moto nagiza kamzigo changu China uturuki au Dubai fumua Bei natulia zangu mpaka zikiisha maisha Yana stress sana
 
Watu wa aina hii wapo na n wale ambao hawana malengo na wanaamin kuwa mda wwte wakitaka kupata pesa wanapata...

Kuna kipindi nlishakuwa mvuvi, tukipanda chombo tunatokomea siku 3 hadi 4 ndan ya maji tukipiga kazi... Hapo tukitoka kila mmoja wetu anakuwa na mgao usiopungua 500k...
Tulikuwa tukipata siku 2 za kupumzika, then ya tatu tunapanda chombo tena.

Kuna watu ambao walikuwa wakisepa, wanatokomea hata wiki 2, akirud n kaishiwa pesa na ana madeni kibao.

Ataingia, atatoka na 500k na atapotea tena.

So n aina flan ya watu wanaotafuta pesa ili waitumie. Hawana malengo.
 
Back
Top Bottom