Huyu kaka ana jinsia gani?

Huyu kaka ana jinsia gani?

Madam X Huyu Sio kichwa desktop kweli?





Habari zenu wakuu, nina mtu wangu wa karibu hali yake inanipa utata. Yeye yuko late 30's amelelewa kilokole na pia hivyo nyumbani kulikuwa na maadili mazuri yaani it was very strict family, mambo ya ujana kwao yalikuwa hayana sehemu, kwahiyo mambo ya watoto wa mjini kwake yalikuwa hakuna.


Sasa yeye ni mtu mzima, mamake na nduguze wamepiga dau la kuoa wamechoka maana kihali na mali inamruhusu (anaishi peke yake). Kitu cha kushangaza huyu mtu hajawahi kuwa wala kuonekana na GF kama kawaida ya wanaume. Hana hata mtoto wa kusingiziwa, yaani urafiki na wanawake hana hata ule wa platonic hakuna zaidi ya sisi jamaa zake. Nimejaribu kumconnect na sister fulani hivi poa, kwa kuhisi labda atakuwa domo zege nalo halikufaa maana ni muda wako pamoja lakini mazungumzo hayaendi next level.

Kuwa ni mlokole si mlokole...jamani kuna jinsia gani zaidi kwa mwanaume kama mtu si gay or straight kuna 3rd option?
 
Mvua hua inatoka juu na kunyea ardhi, unapokuwa unataka itoke chini iende juu unakuwa unabishana na asili.

Ndo jambo linalomkumba huyo mlokole.

Hakuna kinachoanzia juu kuja chini kiasili. Vyote vinavyoonekana kuanzia juu kuja chini vina asili ya kuanzia chini.

Na kwa kweli juu na chini ni concepts zinazotokana na umasikini wa mawazo yetu kutokana na ufinyu wa maono yetu tu.

Rekebisha analogy yako.
 
lakini hata katika dini kuna kitu wanaita 'mseja'

ni mtu anaamua kuishi single kwa sababu zake mwenyewe.
 
kulingana na imani yangu ya dini...jamaaa anapata thawabu kwa kutooa.....mtume (s.a.w) alisema mwenyenye uwezo wa hali na mali basi na aoe..sasa madamex jamaa umesema ana mali inawezekana hana hali kwa maana ya uwezo wa kumridhisha mke......sasa ya nini kuoa afu asubuhi mwanamke kafungasha na kuondoka?? Au anavumila lakini anakuwa anatafuta liziko la nafsi nje ya ndoa??? Hapo si unakuwa unamfanyisha dhambi mwenzio?...

Mie niko karibu na makomredi kuliko mitume.

Lakini kuna kauli nyingi tu za mitume kama hizi zenye mantiki siwezi kuzipinga.

Kimsingi logic ya maneno yako inazunguka palepale nilipopiga mara nyingi tu katika uzi huu.

Kama mtu kajiona hawezi kuishi na mwanamke, tuheshimu oni hili.

Kwa maana hakuna mtu anayeweza kumuelewa mtu mwingine zaidi ya mtu mwingine huyo anavyoweza kujielewa mwenyewe.

Full stop.
 
lakini hata katika dini kuna kitu wanaita 'mseja'

ni mtu anaamua kuishi single kwa sababu zake mwenyewe.

Watu kwa kawaida wanapenda mno kufuatilia undani wa maisha ya watu.

Halafu kimakosa wanadhani mwanaume akioa ndiyo kama vile inamuondolea yeye uwezekano wa kuwa gei.

Ila sielewi kwa nini watu wazima na maisha yao wahangaike na kutaka kujua maisha ya undani ya mtu mzima mwingine. Kwangu huo nauona ni uafkani tu.
 
lakini hata katika dini kuna kitu wanaita 'mseja'

ni mtu anaamua kuishi single kwa sababu zake mwenyewe.

Si ndo hapo utashangaa watu wanapotaka kupiga vita vitu ambavyo hata kimapokeo na kidini vimehalalishwa? Kwa misingi ya kufuata proprieties zote za ustaarabu!
 
mademex watu wa namna hiyo wapo, tatizo kubwa linakuwa lipo kisaikolojia.

1.0 Endapo mtu huyo alikuwa anajihusisha na mchezo wa kupiga kunyeto basi inaweza kuwa hayo ni madhara yake. Watu waliokubuhu katika kupiga nyeto wana sifa ya kuwachukia wanawake kwa mantiki eti wanawake si wasafi na ni wasumbufu kuliko kupiga nyeto.

2.0 Kuwa shoga kwa mazingira uliyosema siyo rahisi, na kama ingetokea hivyo ni lazima tabia hiyo isingejificha maana kuna kipindi angekuwa anahitaji kupigwa nao na kwa mantiki hiyo angekuwa ameshawahi kumsumbua mtu yoyote hapo mtaani na stori kujulikana.

Nina uzoefu na hawa wanaitwa gay person kama mkilala wanaume kwa wanaume wengine hushindwa kujizuia na kuanza kuonyesha dalili za kike na hivyo kujikuta hata kama ushahidi wa 100% haupo lakini hisia za kuwa fulani ni shoga zipo.

Tatizo kubwa la huyo ndugu yako ni hilo tu la kisaikolojia, labda hajiamni katika mambo hali pia inayopelekea kukosa confidence katika mambo yake hasa ya kimahusiano.

Al last mama mtu anaweza kuwa anajua siri ya mwanae kubwa maana nasikia ingawaje sina uhakika eti kama mtoto hasimamishi tokea akiwa mdogo mama hujua. Endapo itakuwa basi jamaa huyo labda inamuathiri japokuwa wengine wenye asili kama hiyo hutongoza sana ili waonekane wazima kumbe hakuna.

Achanane na mambo ya hisia wazazi wa huyo jamaa wamuite waseme na mwanae ili wajue nini tatizo.
 
Last edited by a moderator:
wakati mwingine jamii tunawalazimisha watu kuwa wasichotaka kuwa na labda hawawezi kuwa hivyo.

Imagine huyu kaka wamlazimishe kuoa na kupata watoto.

Akija kuwa mme mbaya na baba mbaya tutashangaa??

Je tutakuwa na haki ya kumlaumu?

Na familia yake tutai-compasate vipi kwa taabu wanayoipata?

Kweli vitu vingine tunajitwisha mizigo isiyo yetu.

Si ndo hapo utashangaa watu wanapotaka kupiga vita vitu ambavyo hata kimapokeo na kidini vimehalalishwa? Kwa misingi ya kufuata proprieties zote za ustaarabu!
 
Nina uzoefu na hawa wanaitwa gay person kama mkilala wanaume kwa wanaume wengine hushindwa kujizuia na kuanza kuonyesha dalili za kike na hivyo kujikuta hata kama ushahidi wa 100% haupo lakini hisia za kuwa fulani ni shoga zipo.

Akhi huo uzoefu na hao watu umeupata wapi?
 
kuna mmama mmoja mmarekani (almost 70) alikuwa ananisimulia, kaka yake ni gay na familia haikuwa inajua maana aliamua kufanya siri, he was miserable.

Huyo kaka kuficha zaidi akaamua kuoa ili kuwapotezea, lakini alikuwa mlevi ana the worst husband, alifanikiwa kuzaa watoto wawili lakini maisha yalikuwa taabu sana ya ndoa.

Akaamua kuachana na mkewe na kuendelea na maisha yake. Baada ya wazazi wao wote kufariki yule kaka akamfuata dada yake na kukonfesi yeye ni gay.

Dada yake akamjibu, hakuna shida, bado nakupenda kama kaka yangu wa zamani. Yule mama akaniambia kaka yake alipata 'relief' kubwa sana kupata acceptance ya dada yake pamoja na kuwa kamwambia yeye ni gay.

Na amejitahidi hata kuacha pombe na kuwa useful citzen wa nchi.

So kama una ndugu gay, nyie wa karibu yake mkamtenga, sisi wa mataifa unategemea tutamfanya nini?
Maana hatuna upendo huo kwake kama walio karibu naye.

Watu kwa kawaida wanapenda mno kufuatilia undani wa maisha ya watu.

Halafu kimakosa wanadhani mwanaume akioa ndiyo kama vile inamuondolea yeye uwezekano wa kuwa gei.

Ila sielewi kwa nini watu wazima na maisha yao wahangaike na kutaka kujua maisha ya undani ya mtu mzima mwingine. Kwangu huo nauona ni uafkani tu.
 
Watu kwa kawaida wanapenda mno kufuatilia undani wa maisha ya watu.

Halafu kimakosa wanadhani mwanaume akioa ndiyo kama vile inamuondolea yeye uwezekano wa kuwa gei.

Ila sielewi kwa nini watu wazima na maisha yao wahangaike na kutaka kujua maisha ya undani ya mtu mzima mwingine. Kwangu huo nauona ni uafkani tu.

Wabongo kwa kujitia pambani kwani utawaweza?!

Wanajua vizuri sana kuwa kuoa hakumaanishi kuwa mwanamme si gay, lakini wao wanahiari mtu aendeleze u-gay wake akiwa kwenye ndoa kwa kile wanachoita kuficha "aibu"

Hapa Madame X tayari ametuonyesha kuwa kwake ni bora huyu ndugu yake angekuwa mhuni akazaa ovyo ovyo kuliko kuwa na heshima yake na kutulia bila ya mwanamke.

Kufuatiliana hivi ndiko kunakosababisha stress zisizo msingi.
 
Kauli yako haina mantiki yoyote, nadhani umejiona kua unachemka..

Of coz nyoka haezi kung'ata mkia wake mwenyewe..nilitegemea jibu kama hili

my true colors ni kuita spade a spade, hamna haja ya kupindishapindisha wala kukwepeshakwepesha wakati tunajua majibu.

Asante,

Kwa kusema "tunajua majibu" kwa kesi ya mtu tusiyemjua - indeed ambaye anaweza kuwa wa kufikirika tu, asiyekuwepo kwa mfupa wala nyama, kwa maana ya kwamba hakuna ushahidi zaidi ya mineno ya jamvini hapa- unazidi kuthibitisha wazimu wako.
 
Habari nzima ya kumuuliza mtu "kwa nini huoi" inawezekana kwa watu waliokosa ustaarabu tu. Kwa sababu inaingilia privacy ya mtu. Halafu swali lina assume kama kuoa ni lazima wakati si lazima. Swali lina betray ignorance ya muulizaji.

Pengine mtu ana matatizo ya kiafya, let's say si gay wala nini, lakini kashajulikana kwamba ana kifafa kikali sana ama kichaa ama ugonjwa wowote ambao akioa ama atampa kazi mke wake ambayo si ya lazima au kuuendeleza kwa watoto wake.

Kwa hiyo kaamua kuuchuna kivyake kwa kuwa considerate kwa watu wengine, hataki kuwapa mzigo.

Wabongo watamshikia bango "kwa nini huoi?" swali ambalo ni cumbersome kwa sababu linaingilia undani wa mambo yake ya kiafya.

Kwa hiyo utaona hapo kwamba hili swali si la kistaarabu, linamchimba mtu na linaweza kuibua mengi ambayo ni ya faragha ya mtu binafsi.

Lakini wapi.

Kwa tamaduni za nchi masikini ambapo faragha ni kitu adimu swali hili (pamoja na lingine "unafanya kazi wapi/gani?") linaonekana ni rahisi tu.

Ni umasikini wa mawazo tu ndio unaoweza kuwafanya watu washupalie maswali kama haya.

Kiranga povu la nini sasa?
 
Utampaje msaada mtu ambaye hataki msaada? Na pengine process nzima ya kumpa msaada itamuondolea privacy yake anayoitaka mwenyewe?

Hapo ndipo mnapoanza umbea na kuufunika kwa vazi la kujali na msaada.

Hamna lolote zaidi ya umbeya tu.

Call it whatever you wish, unahakika gani kama the whole process will invade the his privacy or just merely making assumptions.
 
Habari zenu wakuu, nina mtu wangu wa karibu hali yake inanipa utata. Yeye yuko late 30's amelelewa kilokole na pia hivyo nyumbani kulikuwa na maadili mazuri yaani it was very strict family, mambo ya ujana kwao yalikuwa hayana sehemu, kwahiyo mambo ya watoto wa mjini kwake yalikuwa hakuna.Sasa yeye ni mtu mzima, mamake na nduguze wamepiga dau la kuoa wamechoka maana kihali na mali inamruhusu (anaishi peke yake). Kitu cha kushangaza huyu mtu hajawahi kuwa wala kuonekana na GF kama kawaida ya wanaume. Hana hata mtoto wa kusingiziwa, yaani urafiki na wanawake hana hata ule wa platonic hakuna zaidi ya sisi jamaa zake. Nimejaribu kumconnect na sister fulani hivi poa, kwa kuhisi labda atakuwa domo zege nalo halikufaa maana ni muda wako pamoja lakini mazungumzo hayaendi next level.Kuwa ni mlokole si mlokole...jamani kuna jinsia gani zaidi kwa mwanaume kama mtu si gay or straight kuna 3rd option?
Kwani kuoa lazima? tatizo watu wengi mkifika umri wa miaka 12 mmeshaanza kuzini. Watu kama hao huwa wananunuaga kwenye madangulo we tembelea mida ya usiku kwenye night clab unaweza ukamkuta. Mbona mie mapenzi nilianza baada ya kumaliza chuo nikiwa na miaka 25. Hii ni kawaida mwacheni anamipango yake pengine Mungu anataka kumtumia.
 
Madame X

Huyu kama ni mtu wako wa karibu sana kama ulivyotueleza hapa, unaonaje ukaenda moja kwa moja ukamuuliza mwenyewe kuliko kumsimanga hapa?
 
Back
Top Bottom