Huyu kaka kabila la Mkurya alinishangaza!!!!

Duuuuu....! Sisi wakurya ni wapole sana mtoa mada anatusingizia
 
NAHUJA Kuna mwingine mwanaume wa dar lakini anafungulia kiganja soda/bia sasa sijui ungekua unazimia ukienda nae bar!.
 
Duuuu hapana so kwa hasira hizo kushika mkaa wa moto
 
Mwaka 2005 nilipokuwa namalizia form4 Tarime Secondary, siku hiyo tupo Buhemba tunapiga piga stori na wana mida ya saa moja jion wakaja wakurya wawili wanalumbana, kumbe wanalumbania kipande cha spring ya gari, huyu mmoja akidai ni chake huyu mwingine hataki kumpa, sasa sauti zikawa kubwa katika kulumbana kwao. Kidogo, yule aliyekuwa na kile chuma akampiga nacho kiunon mpaka tukasikia mshindo kutoka kiunoni, mpigwaji akatoa ukelele wa uchungu akamwambia narud Muraa. Jomba aliyepigwa alirudi na chupa za kutosha, akaanza kuzirushia mbali kuelekea aliko mbaya wake. Watu tulisambaa center nzima kila mtu akikimbia kujinusuru.

Analolizungumza Nahuja hata sishangai
 
Ulipoamka ukakuta umejikojolea
 
Waoga tuu
 
Hawa wakurya ndivyo walivyo,ukimuudhi ugomvi hauishi kirahisi hata ipite miaka minane.....wakimaindi wanaweza kukata hata miguu ya ng'ombe yote zizini
Kinachonipa mashaka ni hawa wakurya wa dar kina Mwita waitara wasiojielewa kama wakurya wa Tarime
 
Wakuria hatutaki dharau,fanya yote ila dharau kwetu ni mwiko,tunang'oa roho ya mtu kwa sekunde
Siku moja nilishuhudia kitu cha ajabu sana,kuna jirani yangu mkurya alimpeleka mwanae kwa bibi yake huko tarime dogo akiwa na miaka 3,dogo akaishi huko kwa muda wa miaka 2,baba yake akaenda likizo akarudi naye.
Siku kama mbili hivi toka dogo arudi ,tulikuwa tunapiga stori nje nyumbani kwao ,dogo alikuwa anacheza na wenzie mtaani ,nadhani akagombana na mwenzie akapewa kichapo,tulimuona dogo anarudi mbio analia ,moja kwa moja ndani akatoka na panga anakimbia kurudi huko alikopigwa ,yaani bila kumkimbiza na kumnyang'anya panga sijui ingekuwaje.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…