Huyu kaka kabila la Mkurya alinishangaza!!!!

Huyu kaka kabila la Mkurya alinishangaza!!!!

Muraaa hawapendi maskhara kbs,
Kuna siku moja mkurya alikuwa kainama sasa mstari wa bonde matako ukawa nje!
Kuna jamaa akamtania oyooo muraaa mbona unaacha mali nje!wengine tukiona ivyo hali inabadilika.
Aroo mkurya aliinuka na kisu akaishindilia hapo kifuani kwa jamaa na muvi ndo ikaishia hapo
Walitangaza radio gani maana hili tukio ni la kutangazwa redioni mkuu
 
Mkuu sio uongo yaani mie mwenyewe nilishangaa japo sikukimbia. Nilijiulizani bangi au ni kitu gani. Nilitamani nimuombe nione mikono yake, lakini kwa jinsi alivyokuwa amefura kwa hasira nikaogopa!!!!
Huyo mkurya mwanafunzi wangu, hayo ndiyo mambo yangu kushika na kumeza makaa ya moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jana nikiwa kwenye ofisi za kampuni za mabasi za Adventure na Saratoga jijini Mwanza niliona kituko cha kumalizia mwezi wa Julai, 2018 kutoka kwa kaka ambaye alijigamba kuwa ni mkurya na kweli lafudhi yake ni ya kabila la kikurya.

Kaka huyu ambaye alikuwa maeneo hayo ya ofisi waligombana na mwenzake (wote 2 wanaonekana shughuli zao sio mbali na ofisi hizo). Katika ugomvi huo yule kaka mwingine ambaye sio mkurya akamtukana yule mkurya tusi la kuhusu viungo vya siri vya mama yake mzazi, tusi ambalo wengi wanapenda kulitumia.

Kaka mkurya, alighadhibika sana kusikia tusi lile. Hapo pembeni alikuwepo muuza kahawa, amewasha jiko la mkaa na juu yake kabandika birika la chuma anachemsha kahawa kwa ajili ya wateja wake ambao walikuwa wamekaa kwenye benchi wakiwa wanaongea story zao hasa za kuhusu mheshimiwa Waitara kujivua ubunge.

Ghafla kaka yule mkurya aliyetukaniwa mama yake, akaepua lile birika la kahawa, AKACHOTA MKAA KWA MIKONO YAKE, AKAUSHIKA ULE MKAA MIKONONI KWA SEKUNDE KADHAA, HALAFU KILICHOFUATA AKAMFUATA YULE ALIYEMTUKANA, AKAMGANDAMIZIA ULE MKAA MGONGONI MWAKE, yaan sio kwamba alimrushia ule mkaa bali aliushikilia na kumgandamizia yule mgomvi wake mgongoni kwa mikono yake kwa sekunde nyingi!!!

Du! wateja waliokuwa wanakunywa kahawa walitimua mbio (wanaume wa Mwanza).

Nahuja mie nikasema hapa sitoki hadi nione mwisho wake, hapo kumbuka wanaume wamekimbia pamoja na muuza kahawa. Basi yule aliyekuwa anachomwa alipiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyemsogelea aliyekuwa ameshika moto nikiwemo na mimi.

Nililala usiku naota ndoto mbaya ya lile tukio.


Wewe mwanamme wa Dar ulimsaidiaje yule jama aliyechomwa moto?
 
Back
Top Bottom