Huyu kanichosha

Huyu kanichosha

Brother mbona kama comments hii inafaa Kua Uzi nimekua interested Sana nakama kuna muendelezo tupatie mkuu,how did you manage to break it up,and how many things kama job,watoto nandugu pia,hebu tusaidie Kaka tuko tunajifunza Sisi tunaopitia the same same thing!nawasilisha
Ukimuacha Mwanamke uliyekuwa umefunga nae ndoa muombee mafanikio ama sivyo hakuna rangi utaacha kuiona, utarogwa mpaka uchanganyikiwe unless ujisalimishe kwa Yesu haraka sana.

Yaani utarogwa mchana na usiku, asubuhi utarogwa, jioni, adhuruhi na magharibi utarogwa, utarogwa kwenye ridhki, utarogwa afya yako, jina lako litarogwa, nguo zako, na kila kitu, yaani ni full vita.

Cha msingi usiangalie nyuma, the darkest days precedes the bightest days.
 
What about your babies?
Nimemuachia Mungu, I mention them in my morning, day and night prayers on a permanent basis, and I hear how God is blessing them with health and laughter during the toughest time they are going through.

I have just ticked all my boxes, taking them back is the next and the last remaining. I am about to embark in the deadliest war with that witch demonic lioness. I look forward to to enjoying the battle while God is winning for me as He has been doing since that blackest day of my life.
 
Ukimuacha Mwanamke uliyekuwa umefunga nae ndoa muombee mafanikio ama sivyo hakuna rangi utaacha kuiona, utarogwa mpaka uchanganyikiwe unless ujisalimishe kwa Yesu haraka sana.

Yaani utarogwa mchana na usiku, asubuhi utarogwa, jioni, adhuruhi na magharibi utarogwa, utarogwa kwenye ridhki, utarogwa afya yako, jina lako litarogwa, nguo zako, na kila kitu, yaani ni full vita.

Cha msingi usiangalie nyuma, the darkest days precedes the bightest days.
Yesu ni funga kazi. Sina shaka nae. Umenena vema mkuu.
 
Naitwa Mr. Brian (Sio jina langu halisi). Umri wangu ni miaka 35 kwa sasa. Nilioa miaka mitano iliyopita na mke wangu hivi sasa anayo miaka 28.

Kusema kweli naipenda familia yangu na kama mwanaune najitahidi sana kuihudumia. Nyumbani kwangu tunao mabinti wawili wa kazi. Mmoja kwa ajili ya kusaidia kazi za ndani na mwingine kusaidia kulea watoto wetu mapacha wenye umri wa miaka miwili hivi sasa.

Pamoja na yote nayojitahidi kumtimizia mke wangu, yeye amekuwa mtu ambaye hatimizi majukumu yake kama mke.

Amekuwa na ile aina ya maisha ya mitandaoni, kwanza ni mtu wa kushinda sana Instagram, facebook, Watsapp, Snapchat na Jamii Forums

Katika Page zote za Umbea umbea, page za maeneo ya starehe, hoteli za hadhi hakosekani. Hana muda kabisa wa kunipikia chakula, kunifulia nguo na kazi nyingine zote wanafanya wadada wa kazi.

Nilimtafutia kazi katika kampuni fulani, alifanya kazi miezi miwili tu na kuacha maelezo yake eti mshahara ni mdogo mno ukilinganisha na elimu yake. Kumbe aliniongepea kwani ukweli ni kwamba alifukuzwa kutokana na uzembe kazini.

Sikuona tabu, nikamfungulia duka la bidhaa za nyumbani (mini-shop), lakini biashara hata ikawa haistawi, nilivyofanya uchunguzi nikaja kugundua kuwa sababu ni lugha yake mbovu kwa wateja kiasi ya kwamba ilikuwa haipiti siku bila kugombana na wateja kadhaa jambo lililofanya wateja kukimbia.

Nimechukua maamuzi mara kadhaa ya kumrudisha kwao lakini amekuwa akilia na kudai nimsamehe atajirekebisha lakini wapi, hubadilika muda mfupi na kurudi kwenye ujinga wake.

Jambo kubwa ambalo limefanya mpaka uvumilivu unishinde ni hili; Juzi kati kuna fedha Milioni mbili na nusu niliipata baada ya kuuza mazao yangu, kwa kuwa ile fedha nilipewa cash na ilikuwa siku ya Jumamosi usiku nikaazimia Jumapili baada ya kutoka Kanisani nakaiweke benki kupitia Wakala wa Fahari Huduma.

Kumbe mwenzangu aliziona, akachukua na kwenda kununua furniture, Oven, Friji na vikolombwezo vingine kwa ajili ya kumpa rafiki yake ambaye alikuwa anafanyiwa kitchen party Wiki iliyokua inafuata. Nilipomuuliza akawa akinipa stori za alufu ulela ulela. Hazina miguu wala mikono.

Nafikiri sasa nimechoka rasmi, hapo sijazungumzia masuala ya kunyimwa unyumba. Nafikiria Kutalakiana nae. Maana nahisi muda wowote naweza nikafa kwa pressure nikaacha wanangu bado wadogo.

Je , niko sahihi kwa maamuzi ya kumpa talaka nilee tu watoto mwenyewe maana sioni msaada wowote!View attachment 1094860
Pole mkuu
 
Back
Top Bottom