Huyu kijana Goodlucky Gosbert anajua sana

Huyu kijana Goodlucky Gosbert anajua sana

Haha kuna ule wimbo wake unaitwa Mimi ni muujiza kama sikosei, kuna sehemu anaimba na mdada hivi ana lishepu kama lotee halafu amevaa suruali ya jeans imembanaa basi yule dada hakuna anachofanya zaidi ya kujigeuza geuza kuonyesha shepu lake....nikiangaliaga aibu huwa naona mimi
kabadilika sana hadi havutii tena
 
Haha kuna ule wimbo wake unaitwa Mimi ni muujiza kama sikosei, kuna sehemu anaimba na mdada hivi ana lishepu kama lotee halafu amevaa suruali ya jeans imembanaa basi yule dada hakuna anachofanya zaidi ya kujigeuza geuza kuonyesha shepu lake....nikiangaliaga aibu huwa naona mimi
waimbaji wa dini siku hizi wanaimba bongo fleva
 
Naomba jinsi ya kubarikiwa kwa kusikiliza wimbo wa kidini. Naona kila mtu anasema wimbo umembariki.
 
Anamuimbia BWANA.....

Really?

A big lie!

Mnajiimbia wenyewe kwa enjoyment yenu wenyewe!

There must be a performer and a receiver of that performance,there is no such receiver!

Receivers ni wanadamu wanaemzunguka performer!

There is no BWANA anywhere to receive the performance!
Mkuu kwann umechagua kuwaumiza wenzako kihisia na kiroho. Utaki wabarikiwe ?
 
Ktk uimbaji nawakubali watu wanaoimba kwa staili ya Upendo nkone, Martha mwaipaja, Shusho (wa zamani) na kwaya zote. Waimbaji wengi wa sasa wanazingua ktk uimbaji. Huwezi kufananisha Mabibo Lutheran, au LuLu Mtoni, Kijitonyama, AIC ( zote) na hawa wa kisasa....
Sasa hii inatofauti gani nasi tukisema hakuna bongo flava tamu kama iliorekodiwaga na P.Funk majani iliokuwa imesheheni ujumbe na ala za kusisimua. Ila haimaanishi kwamba bongo flava ya sasa ya kina Wasafi ni nzuri sana au mbaya ni kwamba zama zimebadilika. Gospel za mistari ya bibilia sahivi hazina mvuto ndio maana tumeamia kwenye Sweet Gospel za akina Joel Lwaga, Mercy Masika, Goodluck Gosbert, Angel Benard na kiukweli zinanibamba mno japo mie ni muislam kiasili.
 
Ndio mana Isaka akasema Sauti au audio ni ya Yakobo (Mcha Mungu)..lakini ngozi au muonekano ni wa Esau (asiyemcha Mungu)...kwa kweli utunzi na kuimba yupo talented...Tatizo lipo kwenye Haiba ya kimungu Hana kabisae...mi namshaur aachane na ladha za Bongofleva...unless ahamie huko pia nako kuna fungu nono tuu
Sasa jamaa ana shida gani mbona yupo smart tu mzee baba, au ulitaka avae suti za Lesi Wanyika na Tai pana kama Panga ndio awe na muonekano wa mcha mungu?
 
Me napenda nyimbo zake ila kuna style fulani hivi anaongea siipendi kabisa..in short sielewi kwa nn anaongea hivo yaan mkenya si mkenya dah...apunguze
Hio si ni effect ya studio, inaitwa "auto tune" inaremba sauti tu ila sometime ikizidi ndio inakera!
 
Sasa hii inatofauti gani nasi tukisema hakuna bongo flava tamu kama iliorekodiwaga na P.Funk majani iliokuwa imesheheni ujumbe na ala za kusisimua. Ila haimaanishi kwamba bongo flava ya sasa ya kina Wasafi ni nzuri sana au mbaya ni kwamba zama zimebadilika. Gospel za mistari ya bibilia sahivi hazina mvuto ndio maana tumeamia kwenye Sweet Gospel za akina Joel Lwaga, Mercy Masika, Goodluck Gosbert, Angel Benard na kiukweli zinanibamba mno japo mie ni muislam kiasili.
To me naangalia ujumbe na staili ya uimbaji. Lengo la kuimba ni nini? Jibu lipo ktk staili unayoimbia...hivi mwangalie muimbaji anachoimba na maisha yake anayoishi.....unakuta mtu anachokiimba hakiishi ila anaburudisha tu. Nafkiri ktk misingi ya uimbaji nyimbo za kikristo siyo kuburudisha bali ni kuhubiri kupitia uimbaji.
 
Back
Top Bottom