Huyu Koffi Olomide wana Simba SC tumemkosea nini hadi Kututusi Tusi la Nguoni katika Wimbo wake mpya wa Acquitte?

Huyu Koffi Olomide wana Simba SC tumemkosea nini hadi Kututusi Tusi la Nguoni katika Wimbo wake mpya wa Acquitte?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Naomba ewe Mwana Simba SC ingia upesi YouTube na utafute huo Wimbo wa "Acquitte' kisha tushee pamoja Maumivu ya Kuukosa Ubingwa wa NBC Mwaka huu na Tusi zito la Nguoni lililoanza na Neno Kolo (tulilopewa na Haji Manara) kisha kwa umakini wako kabisa lisikilize hilo Neno la Pili baada ya Neno Kolo.

Anzeni kusikiliza Sekunde ya 24 hadi ya 36 kisha tuanze Kumnunia kwa pamoja Mwanamuziki huyu Koffi Olomide na nahiisi hilo Tusi alilotutukana huenda Wakongo Wenzake walioko Yanga SC akina Mayele, Bangala, Djuma, Ushindi, Moloko na Makambo ndiyo wamemchomesha (wamemsakizia) alitamke hilo Neno (Tusi) lisilovumilika kwa Watanzania hasa Wanaume.

Shikamoo Koffi Olomide.
 
mtoa mada kama hauna kazi ya kufanya
free.jpg
 
Koffi bhana eti kolo.... Kolo......k.kolo....k.olo. Ila jamaa kajisifia sana kwenye huu huu wimbo
Hilo 'Tusi' Kubwa alilotutukana wana Simba SC kwa kuanza kutuita Kolo kisha likafuata nawe Umelisikia Mkuu wangu au?
 
wewe kilaza hapo kofi anasema " Kolo Kumama " kilingala " kumama " maana yake ni kupraise. sikiliza wimbo huu wa Prinx Emmanuel ;



wimbo wa koffi unaitwa " Acquitte" ni wimbo alio utoa maalumu kwa kumsifu na kumshukuru Mungu baada ya kukutwa hana hatia kwenye kesi alizo kuwa amepewa , ndio maana video ya wimbo inaanza na taarifa inayo tangaza kwamba koffi amekutwa hana hatia kwenye kesi zake.
Neno la kifaransa " Acquitte " kwa kiingereza hutamkwa " Acquit likiwa na maana kuachiwa huru na mahakama.


kwa ambao hamja usikiliza wimbo wa koffi ni huu hapa chini


# Ni bonge la wimbo.

ni one of the best song from Koffi.

Ngoma kama hizi koffi alikuwa anazitoa enzi za Andrada.
 
Back
Top Bottom