Nimeona video ya huyu dada ambaye anaonekana kuwa ni mchungaji akiwa anahubiri kanisani. Jambo lililonisikitisha ni kitendo cha kudharau taaluma ya ualimu hasa walimu wa kike wa shule za Msingi.
Kiongozi ni kioo cha jamii hivyo inatarajiwa kuwa maneno unayoyatoa yatakuwa ya kujenga na si kubomoa au kudhalilisha. Ajabu ni kuwa mchungaji huyo ambaye amesahau kabisa fadhila ya elimu aliyopewa na walimu hadi leo anaweza kusimama na kuhutubia watu malipo yake anatolea mfano usiofaa.
Dada huyo kaenda mbali zaidi kumdhalilisha muumini kwa kutaka kumpaka lipstick kanisani akiamini wanaofanya hivyo ndio huolewa. Hajui muumini huyo kama kaolewa au la. Hizi style za mahubiri zinakoelekea sio kwema kabisa. Imagine mme wa yule dada aliyedhalilishwa angekuwa pale church au yule dada angeamua kutoa unyonge si angemchapa ngumi na kusepa zake.
Tuwe tunachagua maneno ya kuhubiri na sio kuwadhalilisha watu wengine.
Natarajia TUCTA na CWT hata viongozi wa serikali watakemea tabia hii