Huyu mchungaji anayedharau walimu na kudhalilisha waumini akemewe

Maticha wamevurugwa usishangae kumuona ticha katwanga pigo private

Waalimu Wana miongozo yao ya kuvaa. Mmoja wa miongozo mwalimu wa kike hatakiwi kuvaa suruali au nguo ya kubana. Sasa baadala ya kuwalaumu walimu nenda ukailaumu wizara ya elimu.

Halafu mahuburi ya kuonesha kundi la watu fulani halifai huo ni ujinga. Mambo ya mavazi ni personal choice. Mbona wanawake wa kiislamu wengi huenda msikitini wamejivika kanga?. Tusilazimishe lifestyle ya njee ikaingia kanisani.
 
...Mkuu, hujatuambia alichosema! Umelalamika TU! Alisemaje?...
 
Kama kweli huyu Ni mchungaji na kuna waumini wataendelea kwenda kumsikiliza watakuwa waajabu itokee ndio nimehudhuria hiyo ibaada ningekatisha kwa kweli hakuna mahubiri ya hivyo huyo atakuwa Ni kungwi wa makahaba na sio mchungaji. Hapo hajadhalilisha walimu na huyo mdada tu kawadhalilisha wachingaji wote ulimwenguni
 
Mimi mwenyewe ni mchungaji na hiyo clip nimeiona kwakweli siyo nzuri ila tunaifanyia kazi huyu mtumishi hakutumia hekima kabisa katika mahubiri yake.

Maana mtumishi unapo hubiri neno la Mungu tunatarajia katika kinywa chako kutoke maneno ya kufariji, kuponya, kujenga, kupatanisha, matumaini, na kuelimisha watu ila katika maadlili mema ya mpendezayo Mungu, na siyo maneno ya kashfa na fadhaa kama aliyoyatamka yeye.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
Kama ningekua Hugo mwanamke ningempiga kofi moja la uso nikawe maarufu, unaona kabisa roho Wa Mungu hayumo ndani mwake.
 
kwanza yeye mwenye hapaswi kusimama mbele kuhubiri. Amekosa sifa anamipasho kama waimba taarabu!. Na wanaoshangilia huenda waoga, hawajuwi au wanajipendekeza.
 
Mtu mishi anacheza na minds za wanawake.
Mwanamke hapendwi kwa makorokoro ila anapendwa kwa vile alivyo smart na vile anajiheshmu na kusimamia mambo yake.
Wanawake wetu wanajipamba wakitoka ila si wakiwa ndani so hayo mapambo si kwetu ila kwa watu wa nje ambao wanaishia kuwataman tu ila si kuwa na upendo nao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…