Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Habari wakuu
Kuna dada mmoja nilisoma naye zamani, miaka mingi kidogo iliyopita. Katika mazingira ya shule tulikuwa tukionyeshana hisia kwa mbali ingawa mpaka tunamaliza hatujawahi kuwa wapenzi.
Baada ya kuhitimu kila mmoja aliendelea na maisha yake, yeye aliolewa na bwana x, aliyekuwa akimiliki kampuni y ya kupeleka watu mbugani. Maisha kwao yalikuwa mazuri sana na walifanikiwa kupata watoto wawili ambao kwa sasa wako chuo kikuu.
Maisha hayatabiriki, kile kipindi cha majanga, wageni wakapungua na kupelekea kampuni kufilisika, na kujikuta jamaa anaanza sifuri. Ilibidi jamaa aame mkoa na kwenda kujaribu shughuli zingine, ambazo kwa sasa zinampa hela tu ya kula.
Kutokana na mwanamke kupenda maisha ya juu, kwake ikawa ni mtihani, kwa sababu yale maisha alioyazoea hayapo tena. Ndipo siku moja, nikapokea simu yake kwa mara ya kwanza, na kunijulisha amenitafuta sana muda mrefu, anataka niwe mshauri wake afanye biashara ipi.
Nikamwambia hakuna shida tutakuwa tunashauriana abc pale panapo wezekana; ndipo akanieleza mkasa wake na kutaka kujua mimi niko na familia au vipi.
Basi tukawa tunawasiliana hapa na pale, ila yeye akawa ananipigia simu ata usiku, nikimuuliza humuogopi mzee wako? anasema yeye ni mtu mzima afuatilii haya mambo.
Baada ya kuumiza kichwa na kutafakari sana, nikagundua huyu anataka anitumie kama daraja ili afanikishe lengo lake kisha anibwage.
Nikaona kabla sijafika mbali, inabidi tubadilishane joto kwanza; tukaweka mikakati ikawa imepangilika vizuri.
Kuna siku nilikuwa nimeenda nchi jirani, wakati wakurudi nikafikia kwenye mkoa aliopo, nikampa taarifa tuonane, akasema haina shida; baada ya dakika 20 ananitumia meseji ametembelewa na mama mkwe kwa hiyo atutaweza kuonana.
Nilipiga mahesabu kiutu uzima, nikagundua nimepigwa chenga; nami nikamjibu sawa. Nikaendelea na shughuli zangu na hatimaye nikarudi mkoani kwangu.
Baada ya kufika mkoani sasa amekuwa akinisumbua sana, mara mwezi ujao nimtumie nauli aje anitembelee, mara ninachangamoto kidogo ya salio naomba unitumie; kwa huruma nilimtumia kiasi kidogo kama 50 hivi.
Kibaya zaidi kwa sasa, amezidisha hali ya kuomba omba; sasa najiuliza haya ni mapenzi au anatafuta mteremko wa maisha?
Sasa hivi kuna 'missed call' zake tatu, na sitaki kupokea; kwa sababu nimeshagundua anataka kunitumia kama daraja.
Equation x mzee wa michepuko nimeshastaafu.
Karibuni kwa ushauri.