Tutawapigia kura kama kawaida. Kwasababu, tunajua fedha za kuongeza mishahara ndo zimejenga zahanati na vituo vya afya ambavyo wazee wetu, wake zetu na watoto wetu ndo wanapokwenda kupewa huduma kila wanapougua.
Tunajua pia fedha za kuongezea mishahara ndo zinatumika kugharamia Elimu Bure ili watoto wetu waweze kupata elimu bila vikwazo.
Tunajua pia fedha za kuongeza mishahara ndo zimejenga Miundombinu ya barabara katika kila kona ya nchi hii ambazo hata Tundu Lissu anazitumia sasa hivi kwenda kuomba wadhamini na kufanya mikutano ya hadhara.
Tunajua pia fedha za kuongeza mishahara ndo zimenunua ndege, kujenga SGR, Bwawa la Umeme, Flyover ambavyo hivi vyote vitakuza uchumi na kutuwezesha kuongezewa mishahara mara dufu huko baadae kuliko tungeongezewa sasa hivi.
Kwa maana hiyo, tumekubali nyongeza ya mishahara yetu itumike kuwanufaisha watanzania wote na siyo sisi kundi la watu wachache. Tunakataa UBINAFSI tunatukuza UZALENDO kwa nchi yetu.