Huyu mwanamke inapoelekea nitampiga nifungwe bure

Huyu mwanamke inapoelekea nitampiga nifungwe bure

Poleni kwa kumpoteza mama,

Japo uchumi wako umevurugika kwa changamoto ulizopitia, ila nakuona kama kijana mpambanaji na mwenye kibali...Hulioni hilo? huoni mambo yako yanaanza kurudi kwenye mstari na ikiwezekana kustawi?...Unataka kumpa shetani nafasi akurudishe nyuma tena?...Huyo mwanamke ni kama agent wa shetani. Mema yote uliyomtendea na familia yake acha Mungu akulipie, mtenda mema hulipwa mema.

Msamehe kwa faida yako, mwambie humhitaji ukiwa umetulia bila hasira...Jipe muda wa kufanya mambo yako na jipende zaidi. Kwa muda sahihi utakutana na ubavu wako
.
 
Pole Sana Mkuu. Uzuri uhai na pumzi bado unavyo! Songa mbele. Haikuwa riziki Kiongozi, tambua hivo, afu songa mbele.

Usimuendekeze huyo dada! Maamzi yako yawe No turning back
 
Kwa jamaa flani alikua na duka pale mhimbili nikamuomba simu nikaweka namba ya demu nikakuta wako na jamaa flan,nikacheki status nyingi wakiwa wanapika pmj,

Kwani demu anae namba ya jamaa mwenye....Duka muhimbili?
 
Kunywa mipombe na kubeba Malaya unajikomoa mwenyewe na familia yako mwishowe upate maradhi bure. Acha hasira, hasira hasara. Ukiua jela inakuhusu, acha mawazo kwa kusikiliza Gospel naamini utakaa poa na maisha yatasonga.
Huyo mwanamke dunia imeanza kumfunza, acha kisasi maana dunia imeanza kukulipia hicho kisasi.
Fikiri kesho yako Mzee baba. Mwombe Mungu atakusaidia

Pole kwa msiba wa Mama
 
Dah pole sana bro kwa masaibu yaliyokupata
Yote ni sehemu ya maisha huna budi kunga'ng'ania kutengeneza mabalaa mengine yatakayo kuathiri wewe na familia yako.........muhimu ni kutemana naye na kukaza buti maisha yasonge mbele
 
Achana nae mkuu, wala usiweke chuki...pita hiviii ukikutana nae msikilize kisha mwambie asahau hicho kitu hakipo tena...kwanini uharibu maisha yako kwa mtu ambaye hana impact tena kwenye maisha yako?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya kama ni hasara umepata acha maisha mengine yaendelee nakuomba tafadhal hayo n makosa ya kawaida inachowaza hakiwez kukusaidia zaid unaongeza matatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana kwa kumpoteza mama ndugu Jimmy.

1. Nakushauri sana jaribu kuacha "chips funga" kuna magonjwa na pia hasara za kifedha na muda. Lakini pia watu wa kiroho watakueleza na hasara nyingine nyingi.

2. Usikubali hata iwaje kurudiana nae. Matokeo yake ni mabaya sana. Mimi yalinikuta twice. Nashukuru Mungu nimefanikiwa kuvuka hizo changamoto japo after effects zinaonekana mpaka leo kwenye maisha yangu ya kila siku.

3. Usimdhuru kwa kisasi. Najua kiu ya kisasi inavyotesa ni kama alosto ya ngada. Jitahidi sana. Jaribu kujenga tabia nyingine upatapo muda huru kukwepa kuwaza kisasi. It takes 21 days to build a habit and 90 days to create a life style. Sio muda mrefu sana.

4. Kama ameshindwa kukuelewa kiraia basi fuata taratibu zingine za kumzuia yeye kukuzoea na kukifuatilia. Naamini wanasheria wataweza kukusaidia juu ya hili.

5. Jijali zaidi wewe na ndugu zako mlioambatana na kubebana wakati wote wa kumuuguza mama. Wacha kumuwaza huyo binti aliekusotesha maisha. Usiwachukie mabinti wote, lakini uwe nao kiakili sana.


Pole sana ndugu Jimmy

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom