Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwizi huyo Nenda PoliceWaungwana habari!
Direct to the topic.
Kuna mtu nilimlipia deni polisi akanipa simu yake 'smart' nishike ili nimrudishie siku alinilipa pesa niliyomlipia.
Sasa hapa mtaani kuna mwanamke nimekuwa natembea naye, wiki mbili zilizopita huyu mwanamke aliniambia ana mimba lakini akawa anasisitiza nimpe hela akaitoe, basi mimi nikaona dalili za kupigwa tu na mimba hana.
Sasa juzi Jumapili asubuhi alikuja geto tukawa na mazungumzo halafu akasepa, aliposepa nikawa simu ya watu siioni, ikabidi nimtafute huyu mwanamke lakini alikataa katakata kwamba haujachukua na hakuiona.
Usiku huu nimetumia mbinu ya kujishusha kwamba nipo tayari nimpe hela anirudishie simu. Amekubali kwamba alichukua simu lakini bila laki harudishi.
Sasa wakuu naomba busara zenu ili nitatue changamoto hii.