Huyu mwandishi yupo field? Mbona amemkosea adabu kocha Gamond kwa swali la kiudhalilishaji alilomuuliza?

Huyu mwandishi yupo field? Mbona amemkosea adabu kocha Gamond kwa swali la kiudhalilishaji alilomuuliza?

Scars

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2017
Posts
48,055
Reaction score
116,512
Yanga kufungwa mechi mbili tayari mwandishi anamuuliza kocha kama bado Yanga wapo kwenye mbio za ubingwa.

Kwenye round ya 10 kupoteza pointi 6 tu tayari mwandishi haioni Yanga kwenye nafasi ya kugombania ubingwa.

Hii sijawahi kuiona popote pale na imenistua.

Huyu mwandishi inawezekana lengo lake lilikuwa ni kumdhalilisha Gamond, lakini out come imekuja na majibu mengi.

Ameidhalilisha ligi ya Bongo. EPL hakuna timu ambayo haijapoteza mechi na Man U tupo nafasi ya 13 tukiwa tumepoteza mechi 4 lakini bado tumesimama kwenye ambitions zetu zilezile

Kiukweli kabisa nashindwa kujua hawa waandishi wa habari za michezo ni kigezo kipi haswa kinachowafanya wapewe dhamana ya kwenda kuiwakilisha media kwenye events kubwa za kimichezo kama hizi?

Unaweza kutia shaka hata tu taaluma zao mpaka hatua ya mwisho ya kufikia kuajiriwa.

Huwenda ni kutokana na mfumo mbovu tulioutengeneza wenyewe ndio unaotuletea haya madhara tunayoyaona leo

Nazungumzia yale mambo ya kupeana kazi kwa kujuana yanayotokana na connection ndio yaliyowapa access vilaza wakajikuta wameajiriwa.

Kama ni ishu za mpira hivi inashindika kweli kwa media ku hire watu ambao wamecheza mpira na wameusomea mpira ili wakiwa field
 
Lakini hilo swali angeulizwa kocha wa KMC isingekuwa ishu, hapo ndio ujue utofauti wa mti wenye matunda na mti usio na matunda.
 
Lkn hilo swali angeulizwa kocha wa KMC isingekuwa ishu, hapo ndio ujue utofauti wa mti wenye matunda na mti usio na matunda.
KMC ambitions zao kwenye ligi ni tofauti na ilivyo kwa Yanga na Simba.

Kuna timu zipo ili ku maintain zisishuke daraja na kuna timu malengo yao ni kuipata top 4 ili walau washiriki michuano ya CAF.

Yanga haipo kwenye daraja hilo.

Lazima tuwe wakweli

Kupoteza pointi 6 sio mpaka ufungwe. Ni mapema sana kumuuliza kocha swali hilo ukizingatia muda uliobakia ni mwingi kuliko uliotumika.
 
Kuna mtu alimuuliza Pacome ile Yanga media day sijui... anamuuliza " ulijiskiaje ulipoukosa mchezo wa mamelodi" kama sitakua sahihi sana mtanisahihisha ..
Aisee swali liliniacha hoi we mambo yalishapitaga unakuja akukumbushia serious😅😅😅
 
Mbona swali la kawaida hilo au kwa sababu Gamond ni kocha mkorofi na Hana akili pamoja na watanzania walio wengi! Wewe unaulizwa Bado upo kwenye kinyang'anyiro Cha ubingwa unaanza kumzodoa mwandishi una akili kweli? Mwandishi anataka kocha aeleze msimano wake kwa mashabiki wake waliokata tamaa na matokeo. Kama unaona Hilo swali ni irrelevant kwanini Wana yanga wanataka kocha afukuzwe? Watanzania wengi ni wajinga.
 
Morinho aliwahi kuulizwa na mwandishi baada ya kuchukua kombe la FA kwamba kwanini unafurahia kuchukua kikombe kidogo tofauti na timu nyingine kubwa kama Man city au Liverpool? Morinho hakumzodoa mwandishi Wala hakupuuza swali na alijibu kitaalam yaani kiprofesssional. Morinho alijibu kuwa hakumbuki ni lini timu kubwa zingine hazikushiriki kombe la FA kisa kombe dogo. Gamond aache ukorofi kitendo Cha kupiga makocha wenzake na namna alivyo muatack mwandishi ni ishara tosha ya kutokuwa professional.
 
Simba ilipopoteza mechi moja na sare moja watu wa Yanga walikuja hapa na kusema simba wasahau ubingwa, Leo wao wanapoteza two matches conservatively wanaulizwa Bado mpo kwenye kinyang'anyiro wanaanza kuwaambia waandishi wametumwa! Hii ni aibu kwa Gamond
 
Mwandishi anajua maswali ya kuulizia ulitaka aulize swali Gani wakati wana yanga wanataka msimano wa kocha kama anataka ubingwa au hautaki. Scars wakati mwingine muwe mnaheshimu taaluma za watu. Kazi ya mwandishi ni kucover maswali ya watu na kwa mwenendo wa Yanga watu wengi wameanza kusema kocha ameshindwa aondoke, mwandishi anataka kumpa nafasi Gamond ya kuwaambia waajiri wake wanachama mipango yake lakini kwa bahati mbaya Gamond anaishia kutukana na anakosa fursa muhimu ya kuweka mipango na kuwatuliza mashabiki.
 
Nazungumzia yale mambo ya kupeana kazi kwa kujuana yanayotokana na connection ndio yaliyowapa access vilaza wakajikuta wameajiriwa.
Kazi za kupeana Kwa kuangaliana usoni na rushwa ndo tatizo la madudu unayoyaona Kila sector. Welevu wanaachwa. Kwa akili ya kawaida huwezi uliza swali la hivyo Tena unaulizwa una uhakika Bado unakazia hata hujishitikii!!
 
Nyie ndiyo hamuelewi mwandishi anauliza Nini, ulitaka ampongeze au amuulize kwanini amefungwa?
 
Mathalani, mwandishi anaweza kumuuliza Rais Samia swali kwanini unakopa sana pesa awamu Yako? Wewe kwa upeo wako mdogo ukamshangaa kwanini ameuliza swali la kitoto Ina maana hajui kwanini tunakopa? Ila kumbe swali ni dynamic linamtaka Rais aeleze mipango yake ya maendeleo kupitia mikopo hiyo na kumjengea uaminifu zaidi kwa wananchi. Swali hili kwa Gamond lilikuwa very favorable kwake kuwaambia wana yanga how the team will improve and how it will adjust the form to remain in the races. Sasa wewe Scars na baadhi ya mashabiki wa Yanga mnamwijia juu mwandishi na kuanza kumzodoa taaluma yake! Serious?
 
Waandishi wengi wakibongo hawajui maswali sahihi yakuuliza.Anauliza swali kama hilo kwenye timu yenye kiwango kikubwa na ndo kwanza imepoteza mechi mbili na kazidiwa point moja tu.haya maswali yanatakiwa yaje kuanzia mwezi wa tatu mwakani kama yanga itakua nafasi ya nne kwenye msimamo.
 
Yanga kufungwa mechi mbili tayari mwandishi anamuuliza kocha kama bado Yanga wapo kwenye mbio za ubingwa.
View attachment 3146583

Kwenye round ya 10 kupoteza pointi 6 tu tayari mwandishi haioni Yanga kwenye nafasi ya kugombania ubingwa.

Hii sijawahi kuiona popote pale na imenistua.

Huyu mwandishi inawezekana lengo lake lilikuwa ni kumdhalilisha Gamond, lakini out come imekuja na majibu mengi.

Ameidhalilisha ligi ya Bongo. EPL hakuna timu ambayo haijapoteza mechi na Man U tupo nafasi ya 13 tukiwa tumepoteza mechi 4 lakini bado tumesimama kwenye ambitions zetu zilezile

Kiukweli kabisa nashindwa kujua hawa waandishi wa habari za michezo ni kigezo kipi haswa kinachowafanya wapewe dhamana ya kwenda kuiwakilisha media kwenye events kubwa za kimichezo kama hizi?

Unaweza kutia shaka hata tu taaluma zao mpaka hatua ya mwisho ya kufikia kuajiriwa.

Huwenda ni kutokana na mfumo mbovu tulioutengeneza wenyewe ndio unaotuletea haya madhara tunayoyaona leo

Nazungumzia yale mambo ya kupeana kazi kwa kujuana yanayotokana na connection ndio yaliyowapa access vilaza wakajikuta wameajiriwa.

Kama ni ishu za mpira hivi inashindika kweli kwa media ku hire watu ambao wamecheza mpira na wameusomea mpira ili wakiwa field
Waandishi wengine jau sana, tena Gamondi anamuuliza na yeye anarudia swali lile lile.
Waandishi wengi hawana akili kabisa.
 
Back
Top Bottom