Mwizukulu mgikuru
JF-Expert Member
- Oct 21, 2021
- 5,715
- 13,739
Wakuu hivi na nyinyi mna wazazi wenye tabia kama hii ya huyu wa kwangu..pindi akiomba msaada utakapomuambia huna kitakachofuata hapo ni kashfa na kejeli..mfano ohhoo wewe mwizukulu kwanza umechelewa kimaisha wenzio wenye umri kama wa kwako wameishajenga..kwanza umebakisha miaka michache ufikishe miaka 40 na huna kitu..😁 na hali ya kuwa hata kitanda anacholalia ni mali yangu. Ukiwa unampa ushauri hakubali inafikia muda mnakuwa kama mnashindana kwa maneno au mnabishana...ukimpa ushauri unapitia sikio la kushoto unatokea la kulia.. ni mbinafsi balaa yeye anachojali ni kuona mambo yake yanafanikiwa..wewe hata ungefirisika ukakosa hata nauli ya kukurudisha ulipotoka utajua mwenyewe..