Huyu ndie mume anayekufaa

Huyu ndie mume anayekufaa

Kichwa cha habri kinakera... Huyu ndyo mume anayekufaa kwahyo ni wote au..?
 
Mtu watu, siyo mtu wa watu hapo ushafanya jina liwe tofauti.

Kwani ulishndwa kuandika wadada huyu ndye mume anayewafaa?
Nimeandika hvyo kwasababu wadada pekee kuendana na tamaduni za tanzania ndio wanaolewa sio wanaume.
 
Habari wanajamvi,

-Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 28.

-Mfanyabiashara

Natafuta mwanamke wa kuishi nae na kuniletea watoto duniani.

Ninapenda sana watoto.

Mwanamke awe na utayari wa kua na familia na ndoa.

Ushirikiano. Na malezi bora kwa watoto.

Ningependelea mwanamke awe na sifa zifuatazo;

1. Awe mcha Mungu Mkristu/Mwislamu/ Mlokole etc.

2. Umri; 20-60.

3. Anaejitambua (asiwe mswahili sana)

4. Mwaminifu kwenye ndoa.

5. Rangi' yoyote tuu.

6. Awe na urefu kama Wastara hivi au Recho wa kipepeo. ( waigizaji)

7. Awe tayari kwa ndoa.

8. Anajituma.

9. Asiwe na historia ya kosa la jinai.

10. Elimu ya kawaida tuu. Ila ajue kusoma na kuandika.

11. Awe msikivu

12. Asiwe mbaguzi

Karibuni PM. Kwa moyo mkunjuvu uliojaa shauku ya kumuona mwanamke atakae ishi na mimi mpaka pale kifo kitakapo tutenganisha.

Nb: - Mjane/ mke ulie achika njoo tushauriane na tuyajenge pengine tutaendeleza safari hii ya upendo pamoja.

- Napenda watoto alie na mtoto/watoto tutazungumza pia.

Karibuni sana.
huu mtego utagombaniwa sana PM
 
Back
Top Bottom