Huyu ndie Raymond

Huyu ndie Raymond

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Paulina Official Video - Madee ft Raymond - YouTube.Still001.jpg
Paulina Official Video - Madee ft Raymond - YouTube.Still002.jpg
Paulina Official Video - Madee ft Raymond - YouTube.Still007.jpg

Yule wa WCB. Kiukweli naye huyu sikjua katokea wapi, mara nikamwona kasajiliwa na Wasafi. Nikimsikiliza nasikia kile ninachopenda kusikia, yaani sauti nzuri ya uanamuziki. Nikajisemea kuwa Diamond hakukosea.

Sasa kuna hii music video ya Madee inaitwa Paulina. Sio maarufu sana kwenye redio au tv bali you tube. Nilikutana tu na huu wimbo nikaupenda na nikawa nautazama mara nyingi. Aliyenivutia sana ni huyo kijana aliyeshirikishwa na Madee. Kaimba vizuri sana. Nikawa najiuliza sasa huyu katokea wapi? Na baada ya hapo mbona sijawahi kumsikia au kumwona tena? Nikajisemea hakika vipaji vinapotea. Maisha yakaenda. Nikawa nausikiliza hasa wakati huyu dogo anaimba. Nikawa nasikitika kipaji kimepotea.

Sasa leo tena napitia nyimbo hizi nakutana na huu wimbo. Ilipofika zamu yake nikamtazama sura vizuri nikajisemea huyu si Raymond? Nikajiaminisha hivyo. Hakika niliposoma jina lake kwenye Madee ft Raymond nikajisikia faraja kuwa kipaji hakikupotea. Kumbe ni Rayvanny huyu wa WCB. Hakika kipaji hakimtupi mtu. Huyu Raymond wa Paulina sio wa Natafuta kiki. Big up Ray. Big up Diamond.
rayvanny.jpg
 
Raia wakipata maisha mazuri wanabadilika
 
~~~~>>>Muziki wa zama hizi ni makelele tu......... Ila kwakuwa jamii yenyewe inahitaji makelele hapo wamepatia
 
Raymond ni almasi iliokuwa inamsubiri DIAMOND aiokote.
 
~~~~>>>Muziki wa zama hizi ni makelele tu......... Ila kwakuwa jamii yenyewe inahitaji makelele hapo wamepatia
Na kwa mbaaali utasikia majina ya watu zaidi ya matano kama unavyosema ni wakati wao
 
hahahaha naipenda san iyoooo mkuu pia kuna nyingne inaitwa upo mwenyew dgo alikuwaga fundi kitambooo ase
 
Dogo yupo vzr sn. Binafsi nilimuona Mbeya akiwa mdogo mdogo wkt nakaa mtaani kwao pale Nzovwe. Safi sn. Aongeze juhudi.
 
Back
Top Bottom