Huyu ndio Dr. Emmanuel Nchimbi ninayemfahamu

Peter Dafi

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
392
Reaction score
272
Anaitwa Dr Emmanuel John Nchimbi, Moja Kati Ya Masenior Comredi Ndani Ya Chama Cha Mapinduzi Ni Mtu Mahiri Katika Kile Anachokiamini Na Hafundishwi Punda Kumwita Farasi.

Ni Mwanasiasa Mwenye Nguvu Ndani Na Nje Ya ccm katika Ushawishi na Ukubalikaji wake.

Wasifu wake kiuongozi ni mpana sana Ameanza Kuwa Raisi Wa Chuo Kikuu Mzumbe Akaja kuwa Mwenyekiti Wa uvccm Taifa Akagombea Ubunge jimbo La songea mjini akirisi mikoba ya Laurensi gama.

Amekuwa mbunge kwa miaka kumi na amekuwa waziri kamili katia wizara mbili tofauti Wizara Ya Nyumba Na Makazi Na Wizara Ya mambo ya ndani pia Amekuwa naibu waziri katika wizara mbili tofauti wizara ya habari tamaduni na michezo pamoja na wizara ya mambo ya ndani.

Anasifika kwa uwelewa mpana wa mambo ya kitaifa katika nyanja mbali mbali kijamii kisiasa na kiuchumi.

Ameweza kuwatenegeza wanasiasa wengi mashughuli wakiwemo madc na wabunge wabunge lijalo katika baraza la vijana taifa la mwaka 2008

Makatibu wa uvccm na wa wilaya na mikao ni product yake pia ni mjumbe kamati kuu kwa miaka isopungua 17 anajua ajenda za chama na kitaifa

Kijana na msomi mwenye uwezo wa kulimudu Bunge lijalo la 11

#Twende na Nchimbi Uspika

 
Twende na Nchimbi
Ni msomi
Ni kijana
Ana uwezo
Ana uzoefu mkubwa
Anaweza kuunganisha watu wa mitizamo tofauti
Ni mwanadiplomasia
Ana kipaji cha uongozi
Ni rika la wabunge waliowengi ktk kipindi hiki
Anaijua ccm ndani nje
Anaijua nchi yetu
Anaweza tumsaidie atalisaidia bunge.
 
Tatizo kwenye u-doctorate wake wa P.hD thesis yake hakui-disseminate kama inavyotakiwa kwa watu wenye kufanya maandiko kama hayo. Kufanya research ngazi ya andiko hilo bila kufanya dissemination ni sawa na kuandika report ya mradi na kuiweka kabatini bila kuwapa watu wasome.Je! alikuwa anaficha nini? Hivyo hivyo na Mery Nagu;

Halafu muda wa masomo ya Bachelor then Master halafu PhD haushabihiani, hakuna andiko la PhD thesis yake ukaandia kwa mwaka mmoja.
 
mnasafishana eee!!!!

Magufuli anachagua majembe kama yeye kuunda Serikali, longolongo no chance!!
 
Hujasema sifa zote, hujasema ukanjanja na unafiki.
Ni hawa ndio Magu alizungumza atawatimua Lumumba.
Bond yake na Lowasa haileti Afya kwa Taifa.
 
hakugombea ubunge kwa sababu ya uspika .


atakatwa tu kama rafiki yake alivyokatwa kwenye urais.
 
hakugombea ubunge kwa sababu ya uspika .


atakatwa tu kama rafiki yake alivyokatwa kwenye urais.

Ubunge alikatwa na kitengo, baada ya kulalamika kukatwa Lowassa!
 
Mimi ukiniambia anasimamia anachokiamini sikuelewi maana tumeshuhudia hapa majuzi katoka nje ya kikao cha kamati kuu akisema CCM hawajatenda haki, halafu baada ya mwezi mmoja anapanda jukwaani kumnadi huyo mtu aliyesema hakupitishwa kwa haki, huu msimamo wa kinafiki umenifanya nimshushe vyeo
 
Jamani Sita hafai kabisa.Tungekuwa na katiba mpya sasa hivi na hii matatizo ingekuwa hakuna.afadhali ya polepole kuliko sita.huku Jusa haingii...Polex2 ajaribu.
 
fisadi wa elimu,hii ni kwa mujibu wa kaenerugaba
 
Spika wa bunge lijalo hatakiwi kabisa kuwa mtu wa mhemuko kama Ndugai, hebu tulieni kutafuta spika anayefaa ndani ya bunge au nje ya bunge. Daktari fake Emmanuel Mchimbi anamheko sana na aliunyesha wazi wakati wa kifo cha Mwangosi akiwa waziri wa mambo ya ndani , pia alivyolipokea suala la kukatwa Lowassa.

Katiba inawaruhusu Kikwete na Lowassa kuomba U-Spika
 

Pia ni TEAM LOWASA!
 
Dr. Emmanuel Mchimbi akiwa spika wa bunge lijalo litamshinda saa 4 asubuhi tu, bunge litakuwa na mavuvuzela kama Nape, si mnakumbuka walivyokuwa wanapalulana wakati wa kugombea uenyekiti wa vijana. Bunge lijalo Emmuel Mchimbi uspika hatoshi.
 

Ungeongeza pia kuwa hatakiwi kuwa mtu wa mabavu kama Zungu. Tunataka mtu wa kanuni na logic
 
Huyu sina imani naye hata kidogo kwanza alikuwepo katika ile list ya mafisadi wa elimu sijui kwanini hakumpeleka mahakamani mtunzi wa kile kitabu.
 
Hivi watanzania mtaacha lini tabia ya kuabudu watu na hatimaye kuanza kuwauza au kwa swahili cha mtaani kuwapigia debe.Amelaaniwa yeye amtegemeaye mwanadamu kuwa kinga yake na huku amemwaacha Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…