Huyu ndio gwiji, jabali na Mfalme wa muziki nchini Tanzania

Huyu ndio gwiji, jabali na Mfalme wa muziki nchini Tanzania

Na tuelewe kuwa nyimbo zao zilitungwa kiustadi hasa, mpaka wimbo unapigwa mbele ya stage elewa umeiva maana ni zaidi ya 15musicians wakionyesha talents zao kwa umakini wa ajabu, vocalist wataimba, midomo ya Bata itasindika na magitaa na piano watapeana muda kusindikizana,tafuta wimbo wa Juwata Jazz wa Etee(ndugu yangu etee pole kwa yaliokifika...)mwimbaji ni Marehemu Shabaan Dede, baadaye solo la marehemu Said Mabera linakabana koo na piano na kupeana nafasi...ardhi ardhi wewe umemeza watu muhimu mno, Nina hasira mno na hawa kenge washika mapumbu, eti yeye pekee na stage show 6 hivi na back up ya vyombo tayari anavutia wavuta unga kibao, DDC Mlimani park orchestra Kuna nyimbo wapo zaidi ya 18 talented musicians kwenye jukwaa, kumbuka Mfaume waniliza, Fikirini, Dada Asha, etc etc
 
Da mkuu umenikumbusha mbali sana mpaka nimejihisi kulengwa lengwa na machozi. Hakika udongo hauli mmea bali hula binadam. Ukifukia shina la kisamvu udongo unacheuwa na mwisho kisamvu kinarudi tena kuota, ukifukia shina la mchicha udongo unacheuwa tena na matokeo yake mchicha unarudi tena kuota. Ila ukifukia mwili wa binadam ndio bye bye udongo haurudishi kitu. Sijui kama tutapata tena burudani kama tulizopata miaka ile ya 80s, 90 hadi 2000.
 
KUTOKA KWA : MSANII, JOTO LA MOTO.

Nimekaa na kuwaza, kuhusu huyu jabali.
Ni mengi ametufunza, kwa tungo zenye akili.
Inabidi kuitunza,heshima ya huyu nguli.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Hebu tuje na mpango,kazi zake tuzienzi.
Tusambaze na mabango,tuwajuze wanafunzi.
Kwamba aliishi bongo, gwiji fundi wa utunzi.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Kongole kwa Waandishi,mfanyao kumbukizi.
Kwa picha na maandishi,dumisheni hiyo kazi.
Sifa zake zinaishi,zisomwapo zake nyuzi.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Wasanii wa kisasa,yawapasa kukumbuka.
Maneno kama msasa, ujumbe aliusuka.
Alionya na kuasa, kwa tungo zisizochoka.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Aliimba ya siasa, furaha mapenzi pia.
Tungo tamu kama pesa, thamani kama rupia.
Kisa baada ya kisa,jabali alitupia.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Nitazitaja baadhi,vijana mzikumbuke.
Nyimbo kali zenye hadhi,aliimba na wenzake.
Zenye ya kwetu mahadhi,hakumuiga Maneke.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Naanza na Mwanameka,wimbo tuliusikia.
Dada mwingi wa vibweka,Musa kamchepukia.
Kidume kaweweseka,ndoa haikubakia.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Akaja kwa Matilida, wimbo ulijieleza.
Ulezi ulimshinda, binti aliyeteleza.
Starehe alipenda, mwana akatelekeza.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Alimuita Mayasa,ushauri akapewa.
Aache mwili kutesa, ngozi yake kuchubuwa.
Asichome bure pesa,uzuri ni kuzaliwa.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Nguli pia aliimba, kuhusu Masudi nunda.
Mwizi fundi wa kukomba,kijana aliyepinda.
Jabali alimuimba, mpaka Sudi akasanda.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Alikumbusha wanywaji, pombe sio chai ile.
Wasiinywe kama maji, walewe kama Masele.
Wanywe wanachohitaji,sio bilauri tele.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Na Wasanii wa leo,yawafaa mfahamu.
Muziki sio wa leo, zilikuwepo awamu.
Kabla kuwepo video, tulifaidi utamu.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Kiba Fidi Dayamondi,Mpoto na Jide dada.
Simtafuti mshindi, nawaita kwenye mada.
Hiki ni chenu kipindi,semeni bila husuda.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Wasanii wa miaka, mlikuwa enzi zile.
Makassy Zoro Bitchuka, Kitime na Jumbe yule.
Maoni yenu twataka,Mumtaje mteule.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Nimefika ukingoni, ila ujumbe ubaki.
Baraza na wizarani,ushauri muucheki.
Hebu mje hadharani,mawazo muyaafiki.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.
 
1. Marijani Radjab
2. Bitchuka
3. Maneti
4. Shaban Dede
5. Muhidin Gulumo
6. Tx Moshi
7. Mbaraka Mwinshehe
Ongezea na hawa ingawa wanaweza kutokuwa magwiji ila walikuwa waimbaji wazuri sana.
1. Muhina Panduka
2. Hussein Jumbe
3. Lovy Longomba
4. Nico Zengekala
5. Tx Moshi William
6. Jerry Nashon Dudumizi
7. Eddy Sheggy
8. Athumani Momba
9. Suleiman Mbwembwe
10. Cosmas Chidumule
11. Max Bushoke
12. Mapacha wawili kyanga songa, na kasaloo kyanga.
13. Issa Nundu
14. Tshimanga Asosa
15. Kasongo Mpinda
16......
Dah kulikuwa na watu wanaimba jamani. List inaweza kuwa ndefu
 
Nashukur mkuu kwa kuongeza list ya waimbaji wetu bora waliowahi kutamba miaka hiyo, na wengine bado wanatamba hadi leo.

Lakini pia kuna hawa wasanii wetu wa varda arts mara nyingi wamekuwa wakisahaulika katika tasnia ya muziki wetu nchini, na wakati enzi zao walifanya mambo makubwa katika kuutangaza mziki wetu, lugha yetu na taifa letu.

Pia kuna mwamba Hamza Kalala nae tumesahau kumuweka kwenye list.
 
Ongezea na hawa ingawa wanaweza kutokuwa magwiji ila walikuwa waimbaji wazuri sana.
1. Muhina Panduka
2. Hussein Jumbe
3. Lovy Longomba
4. Nico Zengekala
5. Tx Moshi William
6. Jerry Nashon Dudumizi
7. Eddy Sheggy
8. Athumani Momba
9. Suleiman Mbwembwe
10. Cosmas Chidumule
11. Max Bushoke
12. Mapacha wawili kyanga songa, na kasaloo kyanga.
13. Issa Nundu
14. Tshimanga Asosa
15. Kasongo Mpinda
16......
Dah kulikuwa na watu wanaimba jamani. List inaweza kuwa ndefu
Huyo namba 4 Niko Zengekala nyimbo zake za mtoto jack na solemba huwa nazielewa sana.
 
Back
Top Bottom