Huyu ndio gwiji, jabali na Mfalme wa muziki nchini Tanzania

Huyu ndio gwiji, jabali na Mfalme wa muziki nchini Tanzania

KUTOKA KWA : MSANII, JOTO LA MOTO.

Nimekaa na kuwaza, kuhusu huyu jabali.
Ni mengi ametufunza, kwa tungo zenye akili.
Inabidi kuitunza,heshima ya huyu nguli.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Hebu tuje na mpango,kazi zake tuzienzi.
Tusambaze na mabango,tuwajuze wanafunzi.
Kwamba aliishi bongo, gwiji fundi wa utunzi.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Kongole kwa Waandishi,mfanyao kumbukizi.
Kwa picha na maandishi,dumisheni hiyo kazi.
Sifa zake zinaishi,zisomwapo zake nyuzi.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Wasanii wa kisasa,yawapasa kukumbuka.
Maneno kama msasa, ujumbe aliusuka.
Alionya na kuasa, kwa tungo zisizochoka.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Aliimba ya siasa, furaha mapenzi pia.
Tungo tamu kama pesa, thamani kama rupia.
Kisa baada ya kisa,jabali alitupia.
Tumuenzi Marijani,ni jabali la muziki.

Nitazitaja baadhi,vijana mzikumbuke.
Nyimbo kali zenye hadhi,aliimba na wenzake.
Zenye ya kwetu mahadhi,hakumuiga Maneke.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Naanza na Mwanameka,wimbo tuliusikia.
Dada mwingi wa vibweka,Musa kamchepukia.
Kidume kaweweseka,ndoa haikubakia.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Akaja kwa Matilida, wimbo ulijieleza.
Ulezi ulimshinda, binti aliyeteleza.
Starehe alipenda, mwana akatelekeza.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Alimuita Mayasa,ushauri akapewa.
Aache mwili kutesa, ngozi yake kuchubuwa.
Asichome bure pesa,uzuri ni kuzaliwa.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Nguli pia aliimba, kuhusu Masudi nunda.
Mwizi fundi wa kukomba,kijana aliyepinda.
Jabali alimuimba, mpaka Sudi akasanda.
Marijani wa Rajabu, heshima yake apewe.

Alikumbusha wanywaji, pombe sio chai ile.
Wasiinywe kama maji, walewe kama Masele.
Wanywe wanachohitaji,sio bilauri tele.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Na Wasanii wa leo,yawafaa mfahamu.
Muziki sio wa leo, zilikuwepo awamu.
Kabla kuwepo video, tulifaidi utamu.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Kiba Fidi Dayamondi,Mpoto na Jide dada.
Simtafuti mshindi, nawaita kwenye mada.
Hiki ni chenu kipindi,semeni bila husuda.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Wasanii wa miaka, mlikuwa enzi zile.
Makassy Zoro Bitchuka, Kitime na Jumbe yule.
Maoni yenu twataka,Mumtaje mteule.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.

Nimefika ukingoni, ila ujumbe ubaki.
Baraza na wizarani,ushauri muucheki.
Hebu mje hadharani,mawazo muyaafiki.
Tuziite Marijani, tuzo zetu za muziki.
Hili bonge la tungo. Unapaswa kupongezwa.
 
Ongezea na hawa ingawa wanaweza kutokuwa magwiji ila walikuwa waimbaji wazuri sana.
1. Muhina Panduka
2. Hussein Jumbe
3. Lovy Longomba
4. Nico Zengekala
5. Tx Moshi William
6. Jerry Nashon Dudumizi
7. Eddy Sheggy
8. Athumani Momba
9. Suleiman Mbwembwe
10. Cosmas Chidumule
11. Max Bushoke
12. Mapacha wawili kyanga songa, na kasaloo kyanga.
13. Issa Nundu
14. Tshimanga Asosa
15. Kasongo Mpinda
16......
Dah kulikuwa na watu wanaimba jamani. List inaweza kuwa ndefu
Umenikuna sana kwa post hii. Yani umenifanya nikumbuke mbali sana aloo.
 
Safi sana mkuu kwa Kuja na mada hii ili watanzania wasisahau watanzania wenzetu ambao kwa kutumia talent zao wakituelimisha,walituburudisha na mwisho mwa yote Wali make sure kuwa mila na desturi zetu zinainziwa duniani, miaka hiyo wimbo ukipigwa radioni hujiulizi ,moja kwa moja unajua hiyo ni TZ music ,sasa hawa kenge wa sasa wametuvuruga mno ,wameharibu muziki wetu kila wakati ni kushika mapumbu yao



Shem Karenga, wema Abdallah, Joseph Mulenga.....nchi hii tumepoteza kabisa vocalists na soloist
Juma Kilaza (Qubqn Malimba), Peter Kinyonga,Malanga Thom (Jamhuri Jazz baadaye Simba wa Nyika)
 
Ndugu nawasalim kwa jina la yule alieumba mbingu, ardhi na vyote vilivyomo ndan yake.

Ndugu zangu nakumbuka marehem babu yangu aliwahi kuniambia kwamba, kama mwanamuziki mkongwe nchini Tanzania hayati Marijani Rajabu aka Jabali la muziki angejaaliwa elimu katika maisha yake ya dunia, basi angekuwa msaada mkubwa sana kwa taifa letu. Marijani Rajabu alikuwa mwanamuziki mwenye maono na upeo wa hali ya juu ktk tasnia ya muziki wetu, hali iliyopelekea nyimbo zake nyingi kupendwa na watu wa rika mbali mbali wakiwemo wazee, vijana na hata watoto pia ukiwapigia jojina leo watakatika mauno mpaka mwisho wa wimbo.

Ni Marijani Rajabu pekee ndio mara nyingi huchukuliwa kama nembo ya muziki wa dansi nchini. Mfano unaweza kumsikia mzazi anamwambia mtoto wake "wewe unaimba nini bwana mbona mziki wenyewe haueleweki, watu tumewaona kina Marijani Rajabu na tukacheza mziki haswa, sasa wewe sijui unaimba nini hapa". Au utasikia mtu anasema "eti na wewe nae msanii, unataka kuwa kama Marijani Rajabu nini".

Pia Marijani ni kati wa wasanii ambao ndimbo zake zimekuwa zikirudiwa na wasanii mbali mbali wenye majina makubwa mfano Lady J dee aliirudia - Siwema, mkongwe Mr Paul aliirudia -Zuwena, wengine wamerudia Jojina nk. Wenye kumjua jabali huyu wanasema kwamba 80% ya nyimbo zake ni visa vya kweli vilivyomtokea yeye, rafiki zake au ndugu zake. Mfano kuna mdogo wake alitoka Marekani kufika bongo akawa anajifanya yeye matawi ya juu basi jabali hakumchelewesha akamtungia nyimbo fasta fasta, dogo alipogundua hilo kwa aibu akaomba msamaha kwa familia yao kwa yote aliyokuwa akiyafanya baada ya kutoka ughaibuni.

Pia Siwema, Sadiki, masudi, Zuwena, Mwanameka, Jojina na nyingine nyingi ni visa vya kweli vilivyotokea ktk jamii afu mwamba huyo akavitolea nyimbo ili kunyoosha mambo.

Nyimbo ya mwanamkiwa nayo inasemekana ni kisa cha kweli kilichotokea katika familia ya jirani yake ambae alifiwa na mkewe na kuowa mke mungine, mwanamke yule akaanza kumtesa mtoto, ndo Jabali kuona vile akamtolea jirani huyo nyimbo kumuonya juu ya kumtesa mtoto yatima.

Marijani Rajabu nyimbo zake zimekuwa ni elimu tosha kwa wazee na vijana mbali mbali. Kila sehemu aliyogusa aliacha ujumbe unaoeleweka. Akiimba mapenzi utafaidika na ujumbe uliopo ndan ya mapenzi, akiimba usia utafaidika usia huo, akiimba maisha utafaidika na alichoimba, kifupi hakuwa kushindwa katika kufikisha ujumbe wake katika jamii.

Babu yang aliwahi niambia kwamba kama huyu mwamba angesomea uchumi na kufikia kuitwa dokta au profesa wa uchumi basi angetoa mchango mkubwa wa uchumi kwa watanzania kupitia taalum yake aliyojifunza maana alikuwa mtu wa watu na kwa bahati nzuri alijaaliwa utu. Kwa wasiomjua 👇

Marijani alizaliwa tar 3 March 1955, Kariakoo, wilaya ya Ilala, jijini Dar. Na alifariki tar 23 March 1995 jijini Dar es salaam.
Marijani ameacha alama kubwa ktk tasnia ya mziki nchini Tanzania. Pichani ni baadhi ya vibao vyake vilivyotamba miaka hiyo.

Mwaka 2016 aliwahi kupewa tuzo ya mwanamuziki bora wa muda wote na aliekuwa raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania mh Jakaya M. Kikwete katika kutambua mchango wake wa tasnia ya muziki hapa Tanzania, maana nyimbo zake zilitumika mpaka kufundishia shule na nyingine kuelekezwa katika maswali ya mitihani ya shule.
RIP Majirani Rajabu aka jabali la mziki.
View attachment 2343089View attachment 2343090View attachment 2343093
Sasa hapa huyu gwiji WA zilipemdwa kila zama na kitabu chake
 
Sasa hapa huyu gwiji WA zilipemdwa kila zama na kitabu chake
Ni kweli kila zama na kitabu chake, lakini huyu ameacha alama ambayo inaenziwa kwa namna fulani.

Hata wimbo wa zuwena wa Diamond ume copy kutoka katika wimbo wa zuwena wa Marijani Rajabu. Hapo bado sijazungumzia wakongwe wengi walio copy nyimbo zake zikawatoa.

Hata Bob Marley ni zilipendwa, lakini kazi yake iliacha alama inayokumbukwa mpaka leo.
 
Ahh! Mashairi ya Mzee Marijani Rajabu..... sio mchezo. Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi. Bahati kazaliwa ndani ya nchi isiyothamini vipaji vya watu wake.
Kweli mkuu, wenzetu wa Congo mwaka jana walizindua sanamu la kumuenzi Francoo, na kuliweka katikati ya jiji la Kinshasa. Ila sisi hatuna wazo la kuwaenzi wanamuziki wetu hata mmoja.
 
Dah nimezaliwa miaka ya katikati ya 90 na 2000 na nimetoka kapa kabisa!

Au nami mtaniita kizazi cha akina mondi?
 
Kweli mkuu, wenzetu wa Congo mwaka jana walizindua sanamu la kumuenzi Francoo, na kuliweka katikati ya jiji la Kinshasa. Ila sisi hatuna wazo la kuwaenzi wanamuziki wetu hata mmoja.
Nakubaliana na wewe kabisa. Tanzania ni nchi ya ajabu sana. Mzee Marijani alikuwa mtu wa msimamo na mwenye kujiheshimu. Wakati wanamuziki wenzake wanakimbila bendi za siasa kama Juwata, Vijana Jazz na Mlimani Park, yeye hakufuata huo mkumbo. Alijiamini sana. Uchawa ilikuwa mwiko kwake.

Alipenda kua mowanamuziki huru na anaejitegemea. Bahati mbaya, finali haikuwa njema kwake. Utu uzima, ufukara na mabadiliko ya muziki wa dansi vileta mitihani mikubwa sana kwa wanamuziki wa dizaini yake.

Mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi.
 
Kwa TZ unaweza kuwa na elimu na bado usiwe msaada kwa taifa zaidi ya kuwa fisadi wa kalamu, pia nae akute angekufa kifo cha kuacha maswali kama Sokoine tu
 
1. Marijani Radjab
2. Bitchuka
3. Maneti
4. Shaban Dede
5. Muhidin Gulumo
6. Tx Moshi
7. Mbaraka Mwinshehe
2: Hassan Rehani Bichuka
3: Hemed Maneti
5: Muhidin Ngurumo


Kuna

Nico Zengekala
Cosmas Chidumule


Ama kweli mziki wa zamani kwa sisi vijana wa 90s unatumbusha mbali sana. Baba yangu alikua na kanda za kaseti nyingi sana za Juwatta Jazz Band, hadi ilipokua Ottu Jazz Band na mwisho Msondo Ngoma Music Band. Pia kaseti za DDC Mlimani Park ambayo nadhani ilikua rival band na hii Ottu Jazz Band. Ahhhh i miss the old days.​
 
Back
Top Bottom