Kikubwa nilichokiona kwenye bandiko lako hapo juu ni kwamba una tamani sana kuishi maisha ya ndoto zako, siku zote kumbuka kwamba siyo kila ndoto ina uhalisia, wanaume unaoishi nao huko mtaani, kazini au popote pale ktk maisha halisi ndio sawa sawa na sisi wa huku mitandaoni (ndio sisi sisi) hakuna tofauti kikubwa tu ni kwamba hujafanikiwa kukutana nasi sote ktk maisha yako halisi na kuzifaham sifa na tabia zetu. Ushauri wangu kwako ni huu 'jiweke huru kupendwa na kupendeka ktk mazingira uliyopo, kila mwanaume ni mume ila mwanamke bora ndiye mwenye uwezo wa kumfanya mume huyo kuwa Mume bora kwake, ukiendelea na mawazo yako hayo utasubiri sana mama hku mitandaoni hakutoshi kuweka uhalisia wote wa maisha yetu, tuna nafasi ndogo tu inayo tufanya tufahamike na kufahamiana kidogo tu kulingana na nafasi, kumbuka hakuna aliye mkamilifu,kujihesabia ukamilifu sana pia ni tatizo, all the best lady.