Huyu ndiye aliyemtukana Rais Kikwete na sasa anatukana Marais wenzake

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
9,524
Reaction score
13,682
Je, ni kitu gani kinampa ujasiri wa kuwadharau Marais wa nchi zingine?

Inafahamika uwezo wa kijeshi hana lakini ana mbwembwe nyingi na kamdomo kwa wingi.

Je, si wakati muafaka kumpa kipigo cha mbwa koko ili afunge mdomo wake?

Sasa hivi anawashambulia na kuwaua walinzi wa amani, je anastahili kuendelea kuwa Rais wa nchi ambayo ni mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki?

Your browser is not able to display this video.

View attachment 3223446
 
Ngoma ikilia sana jua ikaribu kupasuka. Ajitahidi sana awe na mwisho mwema
 
Kama hana uwezo si wampige?
Uwezo anao ndio maana anawapiga mrwara wanatulia
 
Acheni kumuonea wivu huyu jamaa, ameprove kua inawezekana kua mzalendo kwa nchi yako.
Sina hakika kama alimtukana, alimwambia ukweli tu.
Define uzalendo maana
1. Anaongoza Nchi kwa mkono wa Chuma yoyote anaongea Chochote anapotezwa

2. Wananchi wake ni masikini wa kutupwa.

Huo uzalendo kwa Nchi yake ni upi ikiwa Raia hawana furaha ama Mali. Chochote jeshi lake inachopambania ni mdomo wake na si wa wananchi wake.
 
Kama kigezo ni umaskini hakuna nchi Haina masikini.
 
Mi naona kama Kagame yupo sahihi. Kwanini wamuhusishe na ugonvi wa nchi ya Congo. Amesema na ni kweli wale M23 sio Wanyarwanda. Wale ni Watutsi na Wahutu wa huko Congo. Uwepo wa jeshi la Rwanda maeneo ya mipakani ni kwa ajili ya ULINZI.
DRC iimarishe ulinzi wa nchi yake ktk mashariki ya Congo. Inaonekana mashariki ya Congo hakuna serikali ni vikundi vya wababe tu ambao ni vibaraka wa mataifa mbalimbali.
 
Kwanini TZ tusianzishe kakikosi ketu ka wahuni kawe kanatuletea madini adhimu duniani?
 
Kwamba Mataifa yote yanamsingizia Kagame kwa faida ya nani? Kwamba wale wanajeshi wa Rwanda wanaofia Congo ni M23?
 
Tupe tofauti ya anachofanya kagame rwanda na inachofanya ccm Tz.
 
Keyboard warriors na nyie watoto wa 2000 mnapenda vita sana. Siku mkiipata mtakua mabalozi wa kutoa elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…