Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Mathematics Mbona unaicha?
 
Natambua sana Umahiri na Uweledi wa Mwanadada Ana T. Mwakasege (Mtoto wa Mwalimu wa Kiroho Mwakasege ) hasa katika Suala zima la Kurusha Ndege (kuwa Rubani) tena sasa akiwa ni wa Shirika letu la ATCL.

Kinachonishangaza sasa tu ni kuona katika Mitandao mbalimbali Picha inayotamalaki (trend) sasa ni ya Kumuonyesha huyu Dada Ana Mwakasege ambaye bado ni Co - Pilot ( Rubani Msaidizi ambaye katika Cockpit hukaa upande wa Kulia) akisifiwa kuwa ndiyo amerusha Ndege iliyobeba Mwili wa Hayati Rais Dkt. Magufuli kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma huku Rubani Mwandamizi (Mkuu) ambaye Kicheo ndiyo huwa Captain (ambaye katika Ndege huwa anakaa upande wa Kushoto) kule katika Cockpit yao.

Tokea Mheshimiwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan ameapa nimeanza kuona Kirusi fulani kama cha Kijeuri au Cha Kushindana au cha Kututambia Sisi Wanaume kwamba kwakuwa Mpini wa Ikulu umeshikwa na Mwanamke basi Wanaume tutawakoma na tujiandae Kisaikolojia.

Mheshimiwa Rais wangu Mama Samia Suluhu Hassan na Wewe ukijiroga tu ukaingia katika Mfumo huu wa Kijeuri ambao Wanawake Wenzako wanataka Kukuingiza watakuponza na huenda hata ukakosa Ushirikiano wa kutosha kutoka Kwao (Kwetu) Wanaume ma hatimaye Uongozi ukakushinda na ukapigwa Zengwe la maana na ukapakimbia Mwenyewe hapo Ikulu.

Wewe ni Rais wa Tanzania na siyo Rais wa Wanawake wote nchini Tanzania. Ni Kakirusi ka Kipuuzi kama siyo ka Kipumbavu naona kanaanza tu Kujizolea Umaarufu na kuwavimbisha Vichwa Wanawake. Pamoja na Samia ndiyo Rais na ni Mwenzenu Kijinsia, ila mkiwa na Sisi Wanaume mkizingua au mkituzingua tu hata Kuachika mtaachika vile vile.

Imeisha hiyo!
 
Ninauliza tu, Ameolewa?
 
umezungumzia tishio la kupanda juu
Na mwenzako kauliza eti ameolewa? kwa Mnyakyusa naona tabia na mila hataziacha bado mwanamume atakuwa juu kwake.

Kuna jamaa yangu kaoa mwaka jana, lakini miezi hiyo alikuwa akimfuatilia (Kumchumbia si kirasmi) kwa hiyo naona hajaolewa
 
Ndoto yangu kabla sijaujua ukweli wa mambo..nilipokuja kutajiwa kuwa angalau niwe na M150 nikaona si baht yangu acha tu niwe abiria wa kawaida[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…