Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Huyu ndiye rubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa baba Christopher na mama Diana Mwakasege.

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).

Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.

Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe na rubani mwenzio msaidizi (First officer) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.

Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunakuombea kwa safari ya Zanzibar na baadae Mwanza na Chato. Wewe pamoja na team yako yote (cabin crew). Hakika wanawake mnaweza. #TheFutureIsFemale #GenderEmpowerment

MALISA GJ

Sent from my CPH1803 using JamiiForums mobile app
 
Sasa kuna nini cha ajabu hapo? Mpaka leo hii karne ya 21 bado mnashangaa Mwanamke kuendesha ndege??
 
Wakuu Habarini

Kuna post zimekuwa zikisambaa mitandaoni zikimuonyesha mmoja wa marubani ambaye ni mtoto wa Mwl Mwakasege, na kila mtu akizumzungumzia lake + kumpongeza kwa ndoto zake.

Huyu ni mmoja wa marubani wawili waliorusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa Mwalimu Christopher na mama Diana Mwakasege.

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).

Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.

Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe kama Senior First officer na rubani mwenzio (kiongozi) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.

Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunawaombea kwa safari ya Zanzibar, Mwanza na Chato. Wewe pamoja na cabin crew yote. Hakika wanawake mnaweza.
FB_IMG_1616477378899.jpg
 
Siyo kweli kwamba Anna ameajiriwa na ATCL, isipokuwa ameajiriwa na Wakala wa Ndege za serikali TGFA yenye dhamana ya kusafirisha viongozi wakuu kwa njia ya anga lkn pia yenye dhamana ya kusimamia mikataba ya ukodishaji ndege kwa ATCL kwa niaba ya Serikali.

ATCL na TGFA nadhani waliingia mikataba kadhaa ikiwa ni pamoja na ushirikiano kwenye suala la manpower hasa aviation engeering na Operations kwa maana ya Pilots na Cabin crew.

Ukiacha kusukuma hiyo Dash8-Q400 (De haviland) ambayo ni kama zile Bombardier, ni senior 1st Officer anayesukuma Fokker 50 na Gulf stream yaani Ndege ya Mh. Rais.

Kwa pilots wa kike pia yupo pia Joanitha Boman ambaye nae anasukuma ngoma kama hizo.

"Wanawake tunaweza"
 
Huo ndio uzuri wa kuzaliwa kwenye pesa. OVAAAAA!!!

Mkiwa maskini, hata wazazi waombe vipi, ni kama maombi yao hayafiki vile
Wangapi wamezaliwa kwenye pesa wakaishia kuwa mashoga wanahonga wanaume wawabandue?
Wangapi wamezaliwa kwenye pesa wakaishia kuwa mateja?
NB:-
Sio kila Mchungaji ni mwombaji, ndio maana wachungaji wengine shetani anawapiga kikamilifu
 
Back
Top Bottom