Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Huyu ndiye binti wa Mwl Mwakasege ambaye ni mmoja wa marubani aliyerusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli

Nakubaliana naww wanawake hawajui sis wanaume bado ni vichwa pia hawaelew kua hata huyu rais ana mume na watoto hivyo bado anatimiza majukumu yake kama mke.akina Joyce kilia wameachika kwenye ndoa zao saiz anawafunza jeuli wenzie waliokwenye ndoa
 
Relax mzee unataka kuwekena ligi na wanawake, Wewe ni mwanaume Wanajua uwezo wetu hakuna sababu ya kujisifia apa
 
Ndo nawashangaa hawa Majuha. Urubani hata kama form four hujapata cheti kuna baadhi ya vyuo wanakuchukua baada ya katest kadogo
Kurusha ndege sio kazi,kazi ni kupata leseni yake tu ndicho kinachotushinda hapa bongo,lakini kwa mbele kusomea urushaji na kupata leseni yake ni ize sana,
 
Mleta mada kichwa kibovu kwani Co pilot huwa hana uwezo wa kuendesha hiyo ndege? unaelewa maana ya Co Pilot wote marubani wenye leseni moja ya Kurusha ndege za abiria za injini mbili na zaidi
Sheria haziruhusu ndege ya injini mbili kuwa na rubani mmoja Lazima wawe wawili
 
Nadhani watu wanajiuliza inakuaje binti wa kitanznia anaweza kufanya mambo makubwa kiasi hicho
 
Aaah! Kwa dozi za safari hii ya vyuma kukaza wanawake Hawa wezi kuthubutu maana naona single mother wengi ndoa Chache na waliendelea wataisoma vizuri hata hao watoto watajizalisha wenyewe.
 
Halafu huu Uzi mods wataufuta soon maana likija jeshi LA wokozi hatotoka mtu
 
Hawa wanaotuonyesha sehemu zao za Siri 💋💃🧜🤔hadhalani ndio tuwaogope?
 
Ebu walokole mkuke hapa!
Kipindi kile Mlituambia mwalimu mwakasege alikuwa na mtoto mmoja tuu wa ndani ya ndoa yule dogo aliye fariki kwa ‘kuchanganywa’ na pisi kali, sasa ina maana huyu ‘ruban’ alimzaa ujanani au umataifani?? namheshim sana Mwl Mwakasega ila namba ufafanuzi??
 
Yaani ushamba wa kitanzania Kenya kuna wanawake 150 full pilots. 22 wapo na international flights. Kweli tuko nyuma sana.
 
Wakuu Habarini

Kuna post zimekuwa zikisambaa mitandaoni zikimuonyesha mmoja wa marubani ambaye ni mtoto wa Mwl Mwakasege, na kila mtu akizumzungumzia lake + kumpongeza kwa ndoto zake.

Huyu ni mmoja wa marubani wawili waliorusha ndege iliyobeba mwili wa Rais Magufuli. Anaitwa Anna Tusajigwe Mwakasege. Ni binti wa pili wa Mwalimu Christopher na mama Diana Mwakasege.

Anna alipata maono ya kuwa rubani akiwa darasa la 3 tu. Baba yake akampeleka uwanja wa ndege angalau kuona ndege "live" badala tu ya kuziona angani tu. Alipofika darasa la 5 baba yake alitembeza uwanja mdogo wa ndege Arusha ambapo alipata nafasi ya kuongea na marubani kuhusu ndoto yake, nao wakampa ushauri masomo ya kusoma ili aweze kuifikia ndoto hiyo.

Alijifunza urubani Afrika kusini, na siku anarusha ndege kwa mara ya kwanza baba yake hakulala usiku huo (hii ni story ya wakati mwingine).

Lakini kwa sasa Anna ni miongoni mwa marubani wa shirika la ndege ATCL. Kabla ya kujiunga na ATCL alifanya kazi mashirika mengine makubwa ya ndwge kama SAA na kupata uzoefu wa kuendesha ndege kubwa kama Boeing 747, Boeing 777 na Airbus A340.

Hongera Anna kwa kuaminiwa kuendesha ndege iliyobeba mwili wa Rais. Umeweka alama kubwa kwa taifa hili, ambayo haitafutika kirahisi. Mara zote tutakapokumbuka kifo cha JPM tutakumbuka kuwa wewe kama Senior First officer na rubani mwenzio (kiongozi) ndio mlipata neema ya kubeba mwili wake.

Najua si kazi rahisi kuendesha ndege ukiwa na majonzi ya kumpoteza Rais wako lakini umeaminiwa na umeweza. Tunawaombea kwa safari ya Zanzibar, Mwanza na Chato. Wewe pamoja na cabin crew yote. Hakika wanawake mnaweza. View attachment 1732239
Nini chakushangaza!
Yaani kila kitu ni MSHANGAO Tu, uko dunia gani
 
Back
Top Bottom