Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Posts
34,181
Reaction score
41,563
Wakurugenzi,

Nilibahatika kuzaliwa kijiji kimoja na Chritopher Kasangatumbo, alikuwa si mbinafsi mjamaa wa kweli, nilibahatika kumjua nikiwa kijana mdogo sana pale kijijini kwetu ipole, alikuwa mzee mpole na kwenye hekma sana; kwenye misiba alikuwa anatumia muda mwingi kutuelimisha, nakumbuka alituambia mambo ya demokrasia na dhana nzima ya vyama vingi kipindi nipo darasa la tatu; sikuielewa philosophy yake hadi nilipofika kidato cha sita na kukutana na kitu kinaitwa vyama vingi (1995) hapo ndipo nikafungua macho na kujua ni nini hasa Kasangatumbo alimaanisha those days.

Kuna tetesi kwamba wale wote waliohoji au kwenda tofauti na mawazo ya mwalimu walipata ban; yule mzee Kasangatumbo alifanyiwa visa vingi sana hadi kufikia kuibiwa ngombe zake zote, Pamoja na kuishi uingeleza lakini hakuwa na mali yoyote ile mbali ya ngombe zisizozidi therathin alizorithi kutoka kwa wazazi wake. Nilibahatika kusoma na watoto wake, nakumbuka hata viatu hawakuwa navyo; tulienda shuleni pekupeku pamoja ingawa wenzangu waliyaonja maisha ya Uingeleza.

Mzee alikuwa mjamaa wa kweli na hilo halina ubishi, tatizo ni kwamba je alikorofishana vipi na mwalimu? Mimi na wewe hatujui, kuishi kijijini ilikuwa ni moja ya adhabu alizopewa toka juu. Kuna kipindi pale Tabora mjini Bendera ya taifa ilikuwa inashushwa, yeye hakusimama, akakamatwa kupelekwa kituo kikuu, pale kituoni akawaambia mapolice kwamba hawezi kuongea ya yeyote yule pale isipokuwa mwalimu tu. Police hawakumpa nafasi hiyo bali wakamsweka ndani - habari zikamfikia mwalimu ikulu na mara moja akawaambia wamfungulie aende zake - hizo zilikuwa moja ya story zake tukiwa kwenye misiba pale kijijini kwetu.

Kuna siku nilikuwa nimepanga foleni kwa ajiri ya kupata vitu adimu (sukari, sabuni), kwa wale mnaokumbuka yale maduka ya RTC basi watoto tuliambiwa twende mapema ili wakati duka linafunguliwa saa 9 basi tupate vitu hivyo; mida ya saa kumi duka linafunguliwa foleni ikiwa ndefu sana, nikamwona Kasangatumbo anafika eneo la duka, akatuambia tumsikilze dk tano, pale nakumbuka alituambia tutapanga foleni hizo hadi tutakapoamua kuwa na demokrasia ya vyama vingi - pale sikuelewa kitu kwamba hiyo demokrasia ndiyo italeta maduka mengi? I was young by age anyway. (9)

Inaendelea post #2 chini...

cc Ngongo, JingalaFalsafa, Mzee Mwanakijiji, Ogah, Mohamed Said, Nguruvi3, Mchambuzi, WOWOWO, Mkandara, Jasusi, Gembe, Phillemon Mikael, Mwanagenzi, Rutashubanyuma, Augustine Moshi, Pasco,
 
Kuna kipindi cha miaka ya themanini magari 3 aina ya Land-rover 109 yalikuja kijijini kwetu na kwenda moja kwa moja hadi kwake, watu wale wakaingia ndani wakaongea mambo mengi, sisi by the time tukiona gari linaingia kijijini lazima itakuwa ni msiba, lakini haikuwa hivyo; gari zile zikaondoka. Mara msiba ulipotekea tena mzee akafunguka akatuambia aliitwa na Mwalimu ili aende kupewa kazi ya kuongoza shirika la Reli - yeye akasema Shirika wameliua wao then wananipatia mimi - siwezi. Mimi kipindi hicho pamoja na utoto wangu sikumwelewa huyu mzee; kuna wakati mimi na marafiki zangu tukimwona amekaa nje ya nyumba yake akisikiliza radio (BBC) tulikuwa tunahisi kasoma hadi kachanganyikiwa - tulikuwa watoto hatukujua mambo mengi.

Christopher Kasanga Tumbo na Chief Addullah Fundikira ndiyo walikuwa watu wa kwanza kabisa kuunda chama 1992 (UMD) Union for Multi-Party Democracy baada tu ya kuruhusu mfumo wa vyama vingi nchini. Chama kilikuwa kwa nguvu sana hasa kanda ya ziwa na Tabora wa ujumla!! lakini cha ajabu hakikufika hata 1995 kwenye uchaguzi mkuu wa kwanza kikawa kimesambaratika vibaya sana nafikiri ikikuwa kazi ya ki-itifaki.

Kijiji alichozaliwa Kasangatumbo (Ipole) kimekuwa na mizizi ya upinzani toka miaka hiyo, CUF wamekuwa wakitawala wakibadilishana na CCM, lakini uchaguzi mdogo juzi juzi CDM imechukua kata hiyo; si toka mbinguni lakini ni mizizi ambayo mzee kasangatumbo aliitengeneza. wazee na hata vijana /watoto wa wakati huo nikiwemo mimi tunakumbuka mchango wa Christopher kasangatumbo - ingawa hakuna historia yoyote iliyoandikwa juu ya maisha yake.

Ameondoka akiwa maskini ingawa alitoa mchango mkubwa kwa taifa hili - Kuhusu ungomvi na mwalimu hakuna anayejua ila aliishi Kijiji cha Ipole akiwa amekuwa-grounded na system, hakuwa na ruhusa kutoka mkoani Tabora bila kibali toka kwa mwalimu na pass ya kusafiria ilibebwa - pia hakuruhusiwa kufanya mikutano yoyote ile -- kwa ujanja wake alitumia misiba pale kijijini kutueleza falsafa ya demokrasia

sisi wanakijiji wa ipole hatuwezi kumchukia mwalimu kwa namna yoyote ile, lakini kama ungebahatika kuona maisha ya mwanasiasa huyu live basi ungeungana na mimi kusikitika kwamba hakuna hata kipande cha historia kilichoandikwa juu yake kwa vizazi vijavyo.

Kuna mdogo wake aliingia kwenye siasa, nafikiri kuna kipindi alikuwa CDM sijui yupo wapi siku hizi? ile miaka hiyo ya themanini kuna pia mdogo wake mweingine alikuwa anafanya shirika la viatu BORA, hata yeye sina habari zake, huu ni ukoo wa ki-chief kwa pale IPOLE na ndiyo maana ukimuuliza mtu yeyote aliyezaliwa hapo anaweza kukupa mengi juu ya hii familia.

kwa sasa ukoo huu ni kama umesambaratika, hata ile nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa bati ambayo Kasangatumbo aliishi pamoja na familia yake akiwemo marehemu mama yake mzazi ilishaanguka kitambo. huwa nikienda likizo nyumbani nikiangalia masalia ya ile nyumba nakumbuka yote haya niliyowajuza leo, kweli yanasikitisha.

Wenye Kumbukumbu nzuri mwanasiasa huyu baada ya mambo kuwa magumu kimaisha na hali ya afya yake kuzolota basi alifuatwa na watu wa system na kweli for the first time akarudi CCM. hakudumu sana CCM mauti yakamkuta. Kipindi kile sikuweza kuhudhuria mazishi yake kwani nilikuwa chuo.

Sisi wana Ipole tutamkumbuka milele, kwani huu ukoo ni wa ki-chief na yeye alikuwa ni kamanda kweli kweli.

"Hakuna dola ambayo ilipambana na raia wake dola hiyo ikashinda"
Mh. Christopher Kasanga Tumbo: (RIP)
 
Such stories are key katika kuandika historia ya taifa

thanking you for sharing!
Ukweli ni kwamba histori ya Tanganyika imechakachuliwa sana na Baba CCM yaani Tanu, yapo mengi kama haya. Na miaka 20 ijayo yanaweza yasipatikane tena. Maana wale wazee waliokuwepo wakati huo wanaishia. Namkumbuka Zuberi Mtemvu, Michael Sanga, Patric Kunambi, Kasela bantu, Lifa Chipaka, Kassim Hanga, Oscar Kambona, Aboud Jumbe, Mwamwindi the Great, NK. Ni vizuri kujua upande wa pili wa historia.
 
Da ila me simlaumu ticha wala katumbo. Ukichungulia upande wa mwalimu unaweza kuta alilinda maslahi yake na taifa letu changa la tanganyika!

Katumbo nae anaweza akawa alikua na maono yake ambayo nyerere aliona yatamuatarishia uongozi wa taifa na sifa zote alizo jikusanyia yeye kama kiongozi wa taifa.

Siwezi kumchukia Mwl. Katika maisha yangu kwani mwarimu alinikomboa na kuwa huru mungu amesha wapatanisha wazee wetu huko walipo.
 
Na kwanini Saida Karoli aliwhi kuwaimba huyu na Kasela-Bantu?
 
Kasanga Tumbo aliwahi kusimama kupingana na Mwalimu katika Uchaguzi Mkuu 1960 au 1961 (siko sahihi na miaka hapa).

Nakumbuka Kasanga Tumbo alijiuzulu ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kurudi nchini kuanzisha chama kilichoitwa Peoples Democratic Party (PDP). Alitaka kupata jukwaa la kupinga Nyerere kuwaita wahaini waliompinga. Lakini, chama cha PDP kilipigwa marufuku muda mfupi tu na Tumbo akatupwa kizuizini na serikali!

Kasanga Tumbo alipowasili toka London, aliitisha mkutano na vyombo vya habari na kusema alilipwa Paundi 60,000 ili kuweza kumpindua Mwalimu Nyerere, nahisi hapa ndipo alipochemsha na kujikuta hawezi kukwepa mkono wa dola.

Nashauri wakongwe kama mzee Edwin Mtei na Jasusi watusaidie hapa
 
Mmm, sasa huu uzi unakuja vizuri, kama kuna mwanahabari makini achukue mambo hapa, awatafute wazee waliobakia na kuoanisha hizi taarifa, ili tuboreshe historia yetu. Swali je kwa nini vyama vingi vilifutwa Tanganyika? Vilikuwa vingapi? Na viongozi wake walikuwa ni nani?

Nakumbuka siku ile tulipokua ikulu tukizungumzia mustakabali wa vyama vingi Tanganyika, mara Mtemvu na Julius walipokwidana. Mmoja akisema "By the way did you call me another Shombe in Afrika" Mkutano ukavunjika na vyama vingi vikalwakatariwa. Chipaka sijui bado anakumbuka? maana ndio alikuwa muamuzi wa mechi.
 
Mmm, sasa huu uzi unakuja vizuri, kama kuna mwanahabari makini achukue mambo hapa, awatafute wazee waliobakia na kuoanisha hizi taarifa, ili tuboreshe historia yetu. Swali je kwa nini vyama vingi vilifutwa Tanganyika? Vilikuwa vingapi? Na viongozi wake walikuwa ni nani?
yes mkuu, mwanahabari anaweza kwenda pale ipole kuna wazee waliobakia wana mengi mengi zaidi ya haya niliyoandika mimi, from there kizazi kijacho hata sisi pia tutajua mengi zaidi juu ya mwanasiasa machachari.
 
Mkuu wangu Kongolo nakupongeza sana kwa kutuletea habari za wazee wako wa Ipole(Tabora).

Maisha na harakati za kisiasa za Marehemu Christopher Kassanga Tumbo zinatufunza jambo moja muhimu sana kwamba Mwl J K Nyerere alikosana/tofautiana na wanasiasa wenzake bila kujali rangi,kabila au dini au ukanda. Ni vyema tukaelewana kwamba misingi ya minyukano hiyo ilitokana na tofauti za kisiasa na si chuki za kikabila au kidini.

Natarajia michango maridhawa toka kwa waheshimiwa Jasusi, JokaKuu, sweke 34, Mzee Mwanakijiji, Mohamed Said, Ritz, THE BIG SHOW, Nguruvi3, Mwita Maranya .........
 
Kasanga Tumbo aliwahi kusimama kupingana na Mwalimu katika Uchaguzi Mkuu 1960 au 1961 (siko sahihi na miaka hapa).

Nakumbuka Kasanga Tumbo alijiuzulu ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kurudi nchini kuanzisha chama kilichoitwa Peoples Democratic Party (PDP). Alitaka kupata jukwaa la kupinga Nyerere kuwaita wahaini waliompinga. Lakini, chama cha PDP kilipigwa marufuku muda mfupi tu na Tumbo akatupwa kizuizini na serikali!

Kasanga Tumbo alipowasili toka London, aliitisha mkutano na vyombo vya habari na kusema alilipwa Paundi 60,000 ili kuweza kumpindua Mwalimu Nyerere, nahisi hapa ndipo alipochemsha na kujikuta hawezi kukwepa mkono wa dola.

Nashauri wakongwe kama mzee Edwin Mtei na Jasusi watusaidie hapa
yes mkuu picha sasa inakuja, nafikiri baada ya hapa ndiyo akawa grounded kijijini Ipole. na ratiba zake zikawa ni kuchunga ng'ombe wake kila siku asubuhi mpaka jioni.

Pia huko machungani alikuwa analima bustani ya nyanya, mchicha nk -- mimi na marafiki zangu kuna kuna muda tulienda kwenye bustani yake na kudokoa nyanya tunakula akiwa hayupo (so bad)
 
angekuwa ni mzaliwa wa gerezani kariakoo na mtoto wa kiislamu hakika magijwi sampuli ya Mohamed Said povu lingewatoka kumjadili na kuandika historia yake.bahati mbaya yeye hakuwa mzaliwa wa gerezani kariakoo,alikuwa ni mzaliwa wa ipole tabora na mkristu.
Sijakuelewa, hebu funguka zaidi.
 
Huyu mzee alipotoka kizuizini, alikuwa anaishi maeneo ya Ubungo kwa mdogo wake. Alikuwa akisikia watu wanaongea siasa tu alikuwa anatoka nduki. Hivi walimfanya nini?
nafikiri baadaye ikawa order arudi kwao kijijini, na ndiyo maana anakarudi ipole; ni kweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na hakuwa na marafiki pale kijijini, alikuwa mpweke sana na muda wa kuongea na wanakijiji ulikuwa ni wakati wa misiba tu. Na kila utakapomwona lazima awe na radio yake ndogo maskioni na mara nyingi tulikuwa tukisogelea tunasikia habari za kiingeleza, nafikiri alikuwa nasikiliza BBC

Mzee huyu alikuwa anachunga ngombe kutwa nzima juani, mavazi duni sana, kiujumla hali ya miasha yake ilikuwa vigumu kuielezea.
 
Mkuu kadoda11 nime mmention Mohamed Said aje huku ajionee mwenyewe asifungwe na siasa za Gerezani na kutulazimisha ni siasa za Tanganyika.

angekuwa ni mzaliwa wa gerezani kariakoo na mtoto wa kiislamu hakika magijwi sampuli ya Mohamed Said povu lingewatoka kumjadili na kuandika historia yake.bahati mbaya yeye hakuwa mzaliwa wa gerezani kariakoo,alikuwa ni mzaliwa wa ipole tabora na mkristu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom