Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

Huyu ndiye Christopher Kasanga Tumbo (RIP) - Mwanasiasa Machachari

nafikiri baadaye ikawa order arudi kwao kijijini, na ndiyo maana anakarudi ipole; ni kweli alikuwa kama tu aliyechanganyikiwa na hakuna na marafiki pale kijijini alikuwa mpweke sana na muda wa kuongea na wanakijiji ulikuwa kwenye misiba tu. Na kila utakapomwona lazima awe na radio yake ndogo maskioni na mara nyingi tulikuwa tukisogelea tunasikia habari za kiingeleza, nafikiri alikuwa nasikiliza BBC

Mzee huyu alikuwa anachunga ngombe kutwa nzima juani, mavazi duni sana, kiujumla hali ya miasha yake ilikuwa vigumu kuielezea.
Nasiki walikuwepo wengi wa aina hii? Wakabaki wale wa Gerezani tu, katika historia. Na huyu si alikuwa mpambanaji mzuri wakati wa kutafuta uhuru? Mbona sijamwona katika kitabu chochote kile.

Nasiki walikuwepo wengi wa aina hii? Wakabaki wale wa Gerezani tu, katika historia. Na huyu si alikuwa mpambanaji mzuri wakati wa kutafuta uhuru? Mbona sijamwona katika kitabu chochote kile.
wakongwe wanasema historia ya nchi hii imechakachuliwa sana, hata mimi ukiniuliza sijui lolote zaidi ya hitoria ya mwalimu tu ndiyo iliyoandikwa kwenye vitabu vingi, wengine hamna kitu - hata sasa ukiniambia nimuelezee Oscar Kambona, siwezi zaidi ya kukwambia akikuwa katibu mkuu wa Tanu (tena hii nimesimuliwa tu) kisha akatimkia uingeleza kufanya nini na kwa nini mimi hapo sijui kitu.

Ni kweli historia kubwa inayofahamika ni ya nyerere Mohamed Said angeacha udeen wake anayoyandika yangekuwa na maana sema yeye kastiki na wazee wake wa kkoo....bado kuna historia nzuri kule mkoa wa ziwa magharibi inafaa kusimuliwa

Last edited by a moderator:
Kasanga Tumbo aliwahi kusimama kupingana na Mwalimu katika Uchaguzi Mkuu 1960 au 1961 (siko sahihi na miaka hapa).

Nakumbuka Kasanga Tumbo alijiuzulu ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza na kurudi nchini kuanzisha chama kilichoitwa Peoples Democratic Party (PDP). Alitaka kupata jukwaa la kupinga Nyerere kuwaita wahaini waliompinga. Lakini, chama cha PDP kilipigwa marufuku muda mfupi tu na Tumbo akatupwa kizuizini na serikali!

Kasanga Tumbo alipowasili toka London, aliitisha mkutano na vyombo vya habari na kusema alilipwa Paundi 60,000 ili kuweza kumpindua Mwalimu Nyerere, nahisi hapa ndipo alipochemsha na kujikuta hawezi kukwepa mkono wa dola.

Nashauri wakongwe kama mzee Edwin Mtei na Jasusi watusaidie hapa
Informer,
Naikumbuka hii sana. Tuliposoma kwenye magazeti kuwa Kassanga Tumbo amesema amelipwa hela na Uingereza kumpindua Nyerere tulijua huyu jamaa ataishia detention. Na kweli muda haukupita akawekwa detention. Mimi nadhani tatizo la watu kama marehemu Tumbo ni kwamba alikuwa na akili sana na alijiona kuwa na akili sana na watu aina hii mara nyingi wana matatizo ya kutojua kitu cha kusema hadharani. Kuna mwingine yule aliyemfuata Mwalimu baada ya masomo na kusema kazi anayostahili kupewa ni ile aliyo nayo Mwalimu, sasa mtu kama huyu kweli utasema ana akili timamu?

Tusubiri toleo lijalo la Moh.

Nasiki walikuwepo wengi wa aina hii? Wakabaki wale wa Gerezani tu, katika historia. Na huyu si alikuwa mpambanaji mzuri wakati wa kutafuta uhuru? Mbona sijamwona katika kitabu chochote kile.

Informer,

Naikumbuka hii sana. Tuliposoma kwenye magazeti kuwa Kassanga Tumbo amesema amelipwa hela na Uingereza kumpindua Nyerere tulijua huyu jamaa ataishia detention. Na kweli muda haukupita akawekwa detention. Mimi nadhani tatizo la watu kama marehemu Tumbo ni kwamba alikuwa na akili sana na alijiona kuwa na akili sana na watu aina hii mara nyingi wana matatizo ya kutojua kitu cha kusema hadharani. Kuna mwingine yule aliyemfuata Mwalimu baada ya masomo na kusema kazi anayostahili kupewa ni ile aliyo nayo Mwalimu, sasa mtu kama huyu kweli utasema ana akili timamu?

Lakini mkuu hili la kumuweka mtu detention huoni kama mwalimu alikosea...nafkiri vichwa kama kasanga ,tuntemeke hawakufaa kuwa treated namna ile....

Lakini mkuu hili la kumuweka mtu detention huoni kama mwalimu alikosea...nafkiri vichwa kama kasanga ,tuntemeke hawakufaa kuwa treated namna ile....
Yo Yo,
Kumbuka hii ni miaka ya 60. Ben Bella amepinduliwa Algeria na watu waliokuwa karibu naye. Nkrumah hivyo hivyo. Mwendawazimu yeyote angeweza kwenda kukamata RTD na bunduki na kujitangaza amepindua serikali. Kwa Kassanga Tumbo kusema hadharani kuwa amepewa hela na Uingereza kumpindua Nyerere lilikuwa si jambo dogo hata kidogo.

Nasikia nyie TYL kazi yenu kubwa ulikuwa kupopoa mawe viongozi wa upinzani. Kama pale Morogoro mlivyompopoa Chief Kunambi, mtoto wa mzee kingalu, mkamfukuza hadi nyumbani. Kuna wazee Morogoro bado wanajua hizi habari. Naona sasa zinajirudia kwa kuhujumu CDM.

Mkuu mie si mmoja wao,mie ni kamanda mkuu,jaribu kunisoma!

Nasikia nyie TYL kazi yenu kubwa ulikuwa kupopoa mawe viongozi wa upinzani. Kama pale Morogoro mlivyompopoa Chief Kunambi, mtoto wa mzee kingalu, mkamfukuza hadi nyumbani. Kuna wazee Morogoro bado wanajua hizi habari. Naona sasa zinajirudia kwa kuhujumu CDM.
mkuu what is TYL, i can guess Tanganyika Youth Leaque -- ilikuwa jeshi wakati wa mkoloni or something to do with usalama wa taifa wa mkoloni? hapa mneniacha kidogo.

mkuu what is TYL, i can guess Tanganyika Youth Leaque -- ilikuwa jeshi wakati wa mkoloni or something to do with usalama wa taifa wa mkoloni? hapa mneniacha kidogo.

Ni TANU Youth League,hii ilikuwa Jumuiya ya Vijana wa TANU,kama ilivyo leo UVCCM

Kuna historia ya Tanzania imefunikwa!Kuna akina Tumbo ,Mapalala etc.
Ningefurahi mtu siku moja aandike kitabu kuhusu wapinzaniwa kwanza wa udikteta wa Nyerere(Chama kimoja).

Wengi nasikia waliwekwa kizuizini ama Kilwa au huwezi kutoka kijijini kwako.

Kama unajua hiyo story ya hawa waliowekwa kizuizini hasa kisiwani ,labda mlikuwa majirani au watoto.
Akina Kasela Bantu,Tumbo ,Chief Makwaia wote wamesahaulika kabisa.

CCM inavyofanya sasa ni matokeo ya ukoministi wa chama kimoja!Rafiki zetu wa China mpaka sasa wana chama kimoja,
uhuru wa magazeti hakuna.Hata kuabudu!Falun Gong wanapata tabu huko.
Ila Wachina kama utaiibia serikali ,utakipata cha moto.Drug dealersni kupigwa risasi.

Hakuna EPA ,Richmond etc

Lakini mkuu hili la kumuweka mtu detention huoni kama mwalimu alikosea...nafkiri vichwa kama kasanga ,tuntemeke hawakufaa kuwa treated namna ile....

Huwezi kusema Mwalimu alikosea katika hili.Kiongozi mzuri ni yule anayechukua hatua za makusudi pale anapoona maslahi ya taifa yanatishiwa. Utawezaje kuvumilia mtu aliyehongwa na Wazungu tena Waingereza (Wakoloni wetu) kuja kuhujumu Taifa?

Hata hivyo, katika hatua za mwanzo za ujenzi wa Taifa mambo kama haya hayakosekani maana Mwalimu alianza kujenga taifa katika mazingira ya man power ndogo sana hivyo kuruhusu man power hiyohiyo ndogo kugeuka kikwazo kwa sera na mipango ya Taifa changa isingekuwa busara.Mkono wa chuma ni muhimu katika kujenga taifa changa vinginevyo tusingefika hapa tulipo.

Hiki cha Mwalimu ndicho kinakosekana sasa. Kwamba kuna watu wanatuhuma za wazi kabisa za kulihujumu Taifa na kubaka rasilimali zake na hakuna hatua zozote zinazochukuliwa ni jambo la kuudhi na kusononesha sana. Mwalimu angekuwepo vizuizi vingetumika na haya ya pembe za ndovu, magogo yetu kufyekwa, madini kuchotwa, hazina ya fedha kukaushwa nk. yasingekuwepo abadan.

Me miss you Mwalimu Nyerere-R.I.P

Licha ya kusema alipewa fedha kupindua serikali, Kasanga Tumbo (ni mara chache tulikuwa tunasikia jina lake la kwanza, Christopher, ingawa nalo lilijulikana) alikuwa na uhusiano na viongozi wa maasi ya jeshi, Colito Barracks, 1964. Victor Mkello pia alikuwa na uhusiano huo. Kuna mengi bado yamefichwa lakini Kasanga Tumbo na Mkello walikuwa wanatafuta njia ya kutumia maasi hayo kumuondoa Nyerere madarakani na kuunda serikali yao. Kulikuwa na viongozi wengine katika shirika la wafanyakazi na nje ya shirika hilo waliotegemea kuwa viongozi katika serikali ya Kasanga Tumbo na Victor Mkello viongozi hao wawili wangefanikiwa kumuondoa Nyerere. Inasemekana hata Nyerere aliamini kulikuwa na uhusiano kati ya waasi na viongozi hao wa wafanyakazi. Walikuwa siyo viongozi wa kuaminika.

Kwahiyo tofauti kati ya Nyerere na Kasanga Tumbo haikuwa ni ya mfumo wa vyama tu: tuwe na chama kimoja au vyama vingi vya siasa.

Jaribuni kumshawishi Mzee Lusinde atuambie yaliyotokea wakati ule wa maasi. Anajua mengi. Wengine waliojua nini kilitokea - Kawawa, Kambona na Bomani - wameisha tuondoka. Lakini kuna wengine ambao bado ni hai. Kuna mambo mengi pia ambayo Sarakikya anayajua kwa undani. Mwingine ni Mzee Kahama.

Kuhusu Kasanga Tumbo na vitisho vyake kwamba alipewa fedha Uingereza kumpindua Nyerere, pamoja na uhusiano wake na waasi wa jeshi na kujaribu kutumia maasi hayo kuunda serikali yake pamoja na Victor Mkello na viongozi wengine, amshukuru Nyerere hakuwa kama viongozi wengine. Katika nchi zingine za Kiafrika na hata nje ya bara letu, ungekuwa ndiyo mwisho wake wakati ule. Hata kaburi lake msigejua liko wapi.

Ni muhimu tujue historia yetu. Lakini mara nyingi maswali ya aina hii yanapoulizwa, kuna wale ambao wanajaribu kupindua ukweli au kutumia historia hiyo kumshambulia na kumlaumu Nyerere bila kuangalia upande mwingine kwa nini aliamua alivyoamua kuhusu mambo mbali mbali pamoja na yale yanayohusu usalama na umoja wa taifa letu. Alikuwa na mapungufu yake. Alifanya makosa kama binadamu wengine. But he shouldn't be blamed for everything that has gone wrong in our country since independence. Apportion guilt accordingly.

Back
Top Bottom