Bila kujua falsafa ya Kasanga & Kambona na wangineo waliompa.ushauri mwalimu kuhusu namna ya kuijenga Tanganyika mpya; basi hata wewe utasema jamaa walikuwa ni wahaini tu sababu hujui content za maudhui yao.
Jiulize toka 1961 hadi 1985 je aifa limesogea? Je toka 1985 hadi 2018 taifa limesogea? Kushangilia ununuzi wa ndege moja kama sikukuu ya kitaifa; is that you call it nation achievement.
Fuso,
Napenda niseme machache kuhusu
Kassanga Tumbo.
Mwaka wa 1955 babu yangu
Salum Abdalah alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Tanganyika Railway African Union (TRAU) na
Kassanga Tumbo akiwa Katibu.
TRAU si kwa bahati mbaya kuwa ilifuatana na TANU katika kuuundwa kwani huyu
Mwenyekiti wake alikuwa na historia ndefu ya siasa kuanzia African Association.
TRAU na TANU ilipigana bega kwa bega dhidi ya ukoloni wa Muingereza na kwa
hali hii
Salum Abdallah na
Kassanga Tumbo walikuwa pamoja.
Mwaka wa 1960
Salum Abdallah na
Kassanga Tumbo waliongoza mgomo wa
wafanyakazi wa reli uliodumu kwa siku 82.
Mgomo huu ulisimamisha kila shughuli za reli kuanzia gari moshi, mabasi na meli.
Mgomo ulifanikiwa sana na mwishowe serikali ya kikoloni ilikubali madai yote ya
TRAU.
Baada ya uhuru mwaka wa 1961
Mwalimu Nyerere alimteua
Kassanga Tumbo kuwa
Balozi wa Tanganyika Uingereza.
Kassanga Tumbo hakukaa Uingereza akajiuzulu ubalozi akarejea Tanganyika na kuunda
chama cha siasa, Tanganyika Democratic Party, (TDP).
Mwaka wa 1958 kutokana na Uchaguzi wa Kura Tatu baadhi ya wanachama wa TANU
wakajitenga na kuanzisha chama cha Kiislam, All Muslim National Union of Tanganyika,
(AMNUT).
Waislam walikikataa chama hiki kwa iyo hakikupata nguvu.
Wakati
Kassanga Tumbo anarudi Tanganyika kutoka Uingereza baada ya kujiuzulu
ubalozi, Kassanga Tumbo aliingia mazungumzo ya kuunganisha chama chake TDP
na AMNUT.
Hii ilikuwa mwaka wa 1963.
Mwaka 1964 askari wa Tanganyika Rifles waliasi na na baada ya Waingereza kumaliza
uasi ule ikapita kamata kamata na
Salum Abdallah na
Kassanga Tumbo walikamatwa
na kuwekwa kizuizini pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.
Huu ukawa ndiyo mwisho wa TRAU na vyama vingine vya wafanyakazi ikaundwa NUTA.
Yako mengi lakini kwa sasa naomba kusimama hapa.