Ngongo,
Inawezekana hujaona mchango wangu humu.
Kwa nini mimi nikulazimishe wewe kuhusu historia ya wazee wangu?
Nikulazimshe kwa kisa gani na ndiyo iwe nini?
Historia ya Gerezani katika uhuru wa Tanganyika ni ya pekee sana.
Mimi simlazimishi mtu yeyote wao wenyewe wanaposikia niko uwanjani
wanafika kwa khiyari zao kwani wanajua kuna kitu cha maana watajifunza.
Kama hivi wewe ulivyonkaribisha mimi hapa kwenye jamvi.
Je, kuna mtu kakulazimisha kuniita?
Umeniita kwa kuwa ndani ya nafsi yako unajua kuwa mimi najua.
Na hakika Alhamdulilah naijua historia ya wazee wangu na wengi wamethibitisha
hili.
Uzi huu nimeuona na nimeeleza niyajuayo kuhusu Kassanga Tumbo.
Kassanga Tumbo ana nafasi ya pekee kwangu kwani yeye na babu yangu
Salum
Abdallah ndiyo walikuwa waasisi wa Tanganyika Railways African Union (TRAU)
mwaka wa 1955.
Pekua utaona mchango wangu.
Hii ni ziada kwako kukuthibitishia kuwa hii historia iko ndani kwetu.
Mtaa wa Kanoni Tabora Isevya mwisho wa mtaa unaelekea Kachoma katika miaka
ya mwanzoni 1960 kulikuwa na nyumba mbili nzuri sana zinatazamana.
Nyumba hizi zilikuwa moja ya babu yangu na nyingine ya
Kassanga Tumbo.
Kadoda,
Katika lugha ya Kiswahii kudoda ni kuharibika.
Mathalan unga ukiingia maji na hauwezi kusongwa ugali tunasema ''umedoda,''
Unasema natokwa na ''povu.''
Povu linitoke mdomoni kwa kisa gani?
Hapa katika mchango wangu kuhusu
Kassanga Tumbo nimeeleza pamoja
na historia ya babu yangu
Salum Abdallah.
Je, lipo povu?
Naetokwa ni mishipa ya shingo si mimi.
Mtafute na jiangalie wewe binafsi.
Mohamed Said: GEREZANI NA HARAKATI ZA UHURU WA TANGANYIKA SIASA KATIKA MJI WA DAR ES SALAAM MIAKA YA 1950