FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Unaonesha umekurupuka bila kuusoma uzi. Upitie tena.Angekuwa Muislamu Mzee Said Mohamed angeanza kumjadili kwa kina Sana kwa sifa kibao!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unaonesha umekurupuka bila kuusoma uzi. Upitie tena.Angekuwa Muislamu Mzee Said Mohamed angeanza kumjadili kwa kina Sana kwa sifa kibao!
Huyo mwalimu wenu kisingizio Cha kuficha ukatili na tamaa ya madaraja huwa ni kupinduliwa tu!?..kambona,titi Mohammed,kasanga tumbo,kasela bantu,fundikira nkHivi waliompa paundi 60,000 ili ampindue Mwl. walihitaji nini kama mrejesho endapo angefanikiwa
The dark side of Julius NyerereMsome Mwijage kitabu chake (vitabu vyake) kinauelezea udhalim aliofanyiwa wakati wa utawala wa Nyerere.
Yeah, pia kuna kingine alitowa kinaitwa "Julius K Nyerere: Servant of God or Untarnished Tyrant?"The dark side of Julius Nyerere
Mtoa mada anasema kuwa Christopher Kassanga Tumbo mwenyewe alisema kuwa alipewa kiasi hicho cha pesa ili ampindue mwalimu. Je waliompa pesa walitaka wafaidike nini kupitia pesa walizotoa ?Huyo mwalimu wenu kisingizio Cha kuficha ukatili na tamaa ya madaraja huwa ni kupinduliwa tu!?..kambona,titi Mohammed,kasanga tumbo,kasela bantu,fundikira nk
Porojo hizoMtoa mada anasema kuwa Christopher Kassanga Tumbo mwenyewe alisema kuwa alipewa kiasi hicho cha pesa ili ampindue mwalimu. Je waliompa pesa walitaka wafaidike nini kupitia pesa walizotoa ?
Dah!...taifa letu limepitia mengi sana.nafikiri baadaye ikawa order arudi kwao kijijini, na ndiyo maana anakarudi ipole; ni kweli alikuwa kama mtu aliyechanganyikiwa na hakuwa na marafiki pale kijijini, alikuwa mpweke sana na muda wa kuongea na wanakijiji ulikuwa ni wakati wa misiba tu. Na kila utakapomwona lazima awe na radio yake ndogo maskioni na mara nyingi tulikuwa tukisogelea tunasikia habari za kiingeleza, nafikiri alikuwa nasikiliza BBC
Mzee huyu alikuwa anachunga ngombe kutwa nzima juani, mavazi duni sana, kiujumla hali ya miasha yake ilikuwa vigumu kuielezea.
Yeah, lakini historia ya nchi imemuweka pembeni kabisa same as Kambona.Kasanga tumbo rip Mzee na heshima nyingi sana Kwa Wana mageuzi wakweli wote
Hakuna Mjamaa anayehubiri Demokrasia, ukikutana naye wa hivyo basi tambua kuwa huyo ni Mamluki, ni Kibaraka na mshenga wa wakoloni.Wakurugenzi,
Nilibahatika kuzaliwa kijiji kimoja na Chritopher Kasangatumbo, alikuwa si mbinafsi mjamaa wa kweli, nilibahatika kumjua nikiwa kijana mdogo sana pale kijijini kwetu ipole, alikuwa mzee mpole na kwenye hekma sana; kwenye misiba alikuwa anatumia muda mwingi kutuelimisha, nakumbuka alituambia mambo ya demokrasia na dhana nzima ya vyama vingi kipindi nipo darasa la tatu; sikuielewa philosophy yake hadi nilipofika kidato cha sita na kukutana na kitu kinaitwa vyama vingi (1995) hapo ndipo nikafungua macho na kujua ni nini hasa Kasangatumbo alimaanisha those days.
Kuna tetesi kwamba wale wote waliohoji au kwenda tofauti na mawazo ya mwalimu walipata ban; yule mzee Kasangatumbo alifanyiwa visa vingi sana hadi kufikia kuibiwa ngombe zake zote, Pamoja na kuishi uingeleza lakini hakuwa na mali yoyote ile mbali ya ngombe zisizozidi therathin alizorithi kutoka kwa wazazi wake. Nilibahatika kusoma na watoto wake, nakumbuka hata viatu hawakuwa navyo; tulienda shuleni pekupeku pamoja ingawa wenzangu waliyaonja maisha ya Uingeleza.
Mzee alikuwa mjamaa wa kweli na hilo halina ubishi, tatizo ni kwamba je alikorofishana vipi na mwalimu? Mimi na wewe hatujui, kuishi kijijini ilikuwa ni moja ya adhabu alizopewa toka juu. Kuna kipindi pale Tabora mjini Bendera ya taifa ilikuwa inashushwa, yeye hakusimama, akakamatwa kupelekwa kituo kikuu, pale kituoni akawaambia mapolice kwamba hawezi kuongea ya yeyote yule pale isipokuwa mwalimu tu. Police hawakumpa nafasi hiyo bali wakamsweka ndani - habari zikamfikia mwalimu ikulu na mara moja akawaambia wamfungulie aende zake - hizo zilikuwa moja ya story zake tukiwa kwenye misiba pale kijijini kwetu.
Kuna siku nilikuwa nimepanga foleni kwa ajiri ya kupata vitu adimu (sukari, sabuni), kwa wale mnaokumbuka yale maduka ya RTC basi watoto tuliambiwa twende mapema ili wakati duka linafunguliwa saa 9 basi tupate vitu hivyo; mida ya saa kumi duka linafunguliwa foleni ikiwa ndefu sana, nikamwona Kasangatumbo anafika eneo la duka, akatuambia tumsikilze dk tano, pale nakumbuka alituambia tutapanga foleni hizo hadi tutakapoamua kuwa na demokrasia ya vyama vingi - pale sikuelewa kitu kwamba hiyo demokrasia ndiyo italeta maduka mengi? I was young by age anyway. (9)
Inaendelea post #2 chini...
cc Ngongo, JingalaFalsafa, Mzee Mwanakijiji, Ogah, Mohamed Said, Nguruvi3, Mchambuzi, WOWOWO, Mkandara, Jasusi, Gembe, Phillemon Mikael, Mwanagenzi, Rutashubanyuma, Augustine Moshi, Pasco,
Mmm, sasa huu uzi unakuja vizuri, kama kuna mwanahabari makini achukue mambo hapa, awatafute wazee waliobakia na kuoanisha hizi taarifa, ili tuboreshe historia yetu. Swali je kwa nini vyama vingi vilifutwa Tanganyika? Vilikuwa vingapi? Na viongozi wake walikuwa ni nani?
Nakumbuka siku ile tulipokua ikulu tukizungumzia mustakabali wa vyama vingi Tanganyika, mara Mtemvu na Julius walipokwidana. Mmoja akisema "By the way did you call me another Shombe in Afrika" Mkutano ukavunjika na vyama vingi vikalwakatariwa. Chipaka sijui bado anakumbuka? maana ndio alikuwa muamuzi wa mechi.
Umenikumbusha kitu kwenye wimbo huo "TANU jabela mitwe" wengine wakidai TANU imewahi kufanya mauaji ya waasi wake kwa kuwakata vichwa, kuna ukweli wowote? Wimbo huo ulimaanisha nini?Kama vile amenikumbusha enzi za campaign ya kudai Uhuru WA Tanganyika miaka ya 1950 hadi 1960,Historia ya Kasanga Tumbo na akina Chief Fundikila WA pale Itetemya Kipalapala iko wazi,MWL.Nyerere hakutaka malumbano ya vyama Bali waungane kupambana ukoloni,mkutano WA Tabora WA Tanu,wimbo unaosema Ehe Sasi jabela mitwe haaa !
Fuso,Yeah, lakini historia ya nchi imemuweka pembeni kabisa same as Kambona.
Uko sahihi kwa maana halisi ya mjamaa ambayo tafsiri yake hasa ni mkomunisti. Ukomunisti hauendani na demokrasia. Ni socialists ndio wanatambua na kuzingatia demokrasia. Bila shaka, Tumbo alikuwa socialist. (huwa inachanganywa na ujamaa).H
Hakuna Mjamaa anayehubiri Demokrasia, ukikutana naye wa hivyo basi tambua kuwa huyo ni Mamluki, ni Kibaraka na mshenga wa wakoloni.
Kwamba hakusema ?Porojo hizo
Chumvi za waleta story..pound maana yake alipewa na waingereza, waingereza wampindue Nyerere ili iweje wakati alikua mtu wao!!?Kwamba hakusema ?
We ni msukuma/ mnyamwezi au umejisikia kuandika, mitwe ni vichwa, kubela mitwe ni kufanya nini?Uongo mtupu huu, tafsiri ya huo wimbo ni "Tanu yajenga nchi", ni lugha ya kinyamwezi.
Pascal Mayalla JokaKuu Mohamed Said
kubela mitwe ni kuvunja vichwa.We ni msukuma/ mnyamwezi au umejisikia kuandika, mitwe ni vichwa, kubela mitwe ni kufanya nini?
Na ukizingatia baada ya kunusurika kupinduli na jeshi la nchi na kulivunja,aliikabidhi nchi chini ya jeshi la Uingereza kwa karibu mwaka mzima wakati ikiundwa JWTZ.Chumvi za waleta story..pound maana yake alipewa na waingereza, waingereza wampindue Nyerere ili iweje wakati alikua mtu wao!!?