Hapa umekosea, kwanza aya hazifasiriwi kwa mawazo binafsi, sababu kila kitu mtume alikiacha wazi, yaani mtume ameishi miaka yake yote akifasiri Qur'aan.
Huwa kuna sababu za aya kushuka, na ukisoma katika tafsiri ya Ibn Kathir, anaelezea sababu ya kuopolewa mwili wake ukiwa maiti,( ndiyo maana akatumika tamko "mwili" hata katika kiswahili hutumika mara nyingi kuonyesha kuwa mtu ni maiti tayari.) ni baada ya wana wa Israeli kuwa na shaka juu ya kifo chake, ndiyo maana ikashuka aya hiyo, na kuelezea tukio la kuopolewa mwili wake na kweli wakasadikisha ya kuwa yule ni Firaun.
Kwahiyo aya hufasiriwa na mtume, wewe rejea vitabu vya tafsiri upate faida usiweke maoni yako sababu lazima utakosea kama ulivyo kosea hapa.