Huyu ndiye Hashim Dogo, Msanii bora wa Hip Hop Afrika

Huyu ndiye Hashim Dogo, Msanii bora wa Hip Hop Afrika

View attachment 739483

Hashimu Dogo ameacha muziki lakini bado watu wanamuhitaji, tofauti na wasanii wengine wengi wapo kwenye game lakini hawana attention kama yeye.

Nimekutana naye Msasani leo Ustadhi Hashim, hataki tena kufanya muziki. Yeye kwa sasa amekuwa ustadhi swala tano!
HipHop waachieni wenyewe Wamarekani. Wekeni nguvu nyingi kwenye Singeli itawatoaa.
 
Roho 7 n mc wa kawaida sana ,watu wengi wanapenda beats za ngoma zake Ila kiuwezo na mfananisha na kina stamina
We jamaa hujuagi wachenguaji wakali,ule uzi wako eti sugu ni wa kawaida sana anashindwa hata na country boy(mpaka lipstick)...hapa eti unamfananisha roho7 na stamina!!!???
Yani hata ukimleta mtoto mdogo umsikilize nyimbo za hao jamaa ataona tofauti
 
Afadhari useme wewe...anatuletea wasanii ambao hip hop ilishawashinda
 
Mziki wa hip hop ukiachilia mbali wanaoghani kwa kingereza, mtu hawezi penda wimbo kama haelewi lugha unless upende beat na mtu anavyodondoka.
Kuna msanii wa hip hop Uganda anaitwa Fiki Fameika kule ni msanii mkubwa kwa sasa ana trend sana. Niko kwenye group flani la waganda full kumsifia kumpost yani kumpa kila sifa ana wimbo unaitwa kutama umechukua tuzo kibao kule.
Siku moja nikasema ngoja nikatazame huu wimbo dah yani niliona hakuna analoimba.
Ndipo nikajua kwanini ni ngumu wasanii wetu wa hip hop kuwa bora afrika

Nadhani wengi tunashindwa elewa kuwa.. “KILA MTU ANAWEZA KURAP, ILA SIO KILA ANAYERAP ANAFANYA HIPHOP”
 
Back
Top Bottom